Monday, March 4, 2013

Wakenya kuongea kupitia kura ili kumchagua rais.

 Wakenya kuongea kupitia kura ili kumchagua rais.

Nairobi, Kenya - 04/03/2013. Wananchi wa Kenya leo wanapiga kura kumchagua rais na kuwachagua wabunge ambao wataongoza nchi kwa kpindi cha miaka mitano.
Hata hivyo katika harakati za uchaguzi huo ambao umekuja na mtazamo tofauti kwa wananchi wa Kenya. Mjini Mombasa watu kumi natatu wameuwawa akiwemo polisi baada ya kutokea vurugu katika harakati za kuandaa uchaguzi.
Kundi la Mombasa Republikan Kanseli limeshukiwa kuhusika na mauaji hayo.
Wapinzani wakubwa katika kugombea kiti cha urais ni Raila Odinga na Uhuru Kenyatta, ambo kabla ya kuanza kwa uchaguzi kura za maoni zilionyesha kuwa wapo karibu sawa.
Uchaguzi mkuu wa Kenya unawekewa jicho ng'aavu, ili kuzuia mauaji yaliyo tokea mwaka 2007 ambapo watu zaidi ya 1000 walipoteza maisha yao.

Jeshi la Nigeria lashambulia ngome ya Boko Haram

 Lagos, Nigeria - 04/03/2013. Jeshi la Nigeria limedai kuwaua wapiganaji wa kundi la Boko Haram katika mashambulizi yaliyofanywa Kaskazini mwa Mashariki ya jimbo la Borno.
Msemaji wa jeshi amesema "jeshi la serikali limeweza kuwauwa wapiganaji 20 na mauaji hayo yalifanyika karibu na kijiji cha Mongono, siraha na vifaa vingine vya kijeshi vilikutwa katika eneo hilo."
Mashambulizi hao kwa kundi la Boko Haram, yamekuja huku mkuu wa kundi hilo Abubakar Shekau akikanusha kuwepo na mpango wa mazungumzo na serikali ya Nigeria. 
Kundi la Boko Haram limekuwa likilaumiwa kwa kuleta mchafuko wa amani nchini Nigeria kwa kuhusika na mashambulizi ya kigaidi yanayo tokea nchini humo mara kwa mara.
  
Makachero waliandaliwa kumua rais wa Syria.


Beirut, Lebanon - 04/03/2013.Gazeti la  moja nchi Lebanon limetangaza ya kuwa limepata nyaraka  zinazo oonyesha mpango wa Uturuki na Ufaransa wa kutaka kumua rais wa Syria Bashar al Assad.
Gazeti hilo la habari  Asianews lina ropoti ya kuwa nyaraka hizo zinaonyesha mpango na mbinu ambazo zingetumika katika kumua rais huyo wa Syria.
Kwa  mujibu wa gazeti hilo lilisema "makachero wa Kifaransa na Wakituruki walikuwa wameshapanga mbinu zitakazo tumika katika mauaji hayo ikiwa ni kuwaajili baadhi ya maafisa wanao fanya kazi katika ofisi ya rais Bashar al Assad."
Wakati huo huo rais Bashar al Assad amesema "Uingereza ipo mbioni kuwauzia siraha waasi wa serikali ya Syria na hatutarajii ya kuwa Uingereza inaweza kuwa msuruhishi."
 Naye waziri wa mambo ya nje ya nchi ya Syria Walid al Muallem alithibitisha kuwepo kwa mpango  na kudai yakuwa "Saudu Arabia inajua mipango yote pamoja na washiriki wake.
Mapigano nchini Syria ya kutaka kumngóa madarakani rais Bashar al Assad yamekuwa yakiendelea na huku mamia ya watu kupoteza maisha yao, mali za nchi kuharibiwa vibaya na raia wengine wa Syria kuikimbia nchi yao. 

No comments: