Thursday, March 7, 2013

Korea ya Kaskazini yatishia kuishambuli Marekani.

Kambi ya Raira Odinga yalalamikia matokeo ya uchaguzi. 


Nairobi, Kenya - 07/03/2013. Uchaguzi mkuu wa urais nchini Kenya umeanza kuingia dosari baada ya kambi ya mgombea wa kiti cha urais Raila Odinga kudai ya kuwa kuna walakini kutokana na matokeo ya uchguzi huo yanavyo tolewa.
Kalonzo Musyoka ambaye ni makamu wa Raira Odinga katika uchaguzi huo wa rais nchini Kenya alisema "tunaushaidi ya kuwa matokeo ya uchaguzi yanayotolewa yana wizi ndani yake kwani kuna matokeo mengine yameonyesha  kura zimezidi zaidi ya waliojiandikisha."
"Na hatutaki maandamano kwani tupo ndani ya serikali ya shirikisho na niwajibu kufuata sheria."
Hadi kufikia sasa kambi ya Uhuru Kenyatta inaongoza kwa kura nyingi za urais zidi ya Raila Odinga na imepinga madai hayo ya kambi ya upinzani.
Hata hivyo kamati inayoshughulikia na kusimamia uchaguzi huo imezitaka kambi zote kusubiri matokeo ya mwisho, kwani nijambo la kushangaza kanza kulalamikia matokeo wakati bado kura bado zinahesabiwa.

Muuaji wa wapinga ubaguzi  wa Afrika ya Kusini afariki dunia.


Pretoria, Afrika ya Kusini - 07/03/2013. Kachero aliyekuwa wa serikali ya kibaguzi ya Afrika ya Kusini na ambaye alihusika katika kupanga mauaji ya wale wote waliyokuwa wanapingana na serikali ya kibaguzi amefariki dunia.
Dirk Coetzee 57, ambaye alikuwa akifanya mipango na mauaji hayo kwa kushirikiana na baadhi wa waafrika wa Afrika ya Kusini kwa kuwaingiza nchini Afrika ya Kusini kisiri na kuwapa kazi ya kuwakamata Waafrika wenzao na kuwaleta katika shamba la Vlakplaas mahali ambapo mauaji yalifanyika.
Dirk Coetzee alitubu hayo mara baada ya kurudi nchini Afrika ya Kusini na kutoa mfano kwa kutaja majina  ya  mauaji aliyo yafanya na kusema  "nilihusika katika mauaji ya wanachama wa ANC na wale wote waliokuwa wanapinga serikali"
Hata hivyo Coetzee alisamehewa makosa yake kwenye baraza la  ukweli na maridhiano  mwaka 1997 ambapo baadhi ya watu waliofanya makosa na mauaji katika serikali ya kibaguzi ya Afrika ya Kusini walisamehewa pia.

Aliyekuwa wazirimkuu wa Itali kwenda jela.


Milan, Itali - 07/03/2013. Aliyekuwa waziri mkuu wa Itali amehukumiwa kwenda jela mwaka mmoja, baada ya kukutwa na hatia ya kurekodi mazunguzo yaliyokuwa yakifanyika katika mahakama kinyume na sheria mwaka 2006.
Silvio Berluscon 78, ambaye alishawahi kuiongoza Itali kama waziri mkuu, amehukumiwa kifungo hicho baada ya habari za kurekodi mazungumzo hayo kuvuja kutoka kwenye chombo cha habari ambacho kinasimamiwa na Paolo ambaye ni kaka ya Berlusconi.
Hata hivyo Silvio Berlusconi amekata rufaa zidi ya hukumu hiyo na kudai ya kwa kusema " hii ni mbinu za kutaka kunimaliza kisiasa na za kipendeleo."
Hivi karibuni Silvio Berlusconi alirudi kwenye uringo wa siasa na chama chake FrozaItalia kupata kura nyingi katika uchaguzi uliyofanyika hivi karibuni.

Maelfu wakusanyika kumuaga rais Hugo Chavez.


Karakas, Venezuela - 07/03/2013. Maelfu ya Wavenezuela wamakusanyika katika barabara kuu katika jiji la Karakas, ili kumuaga kwa mara ya mwisho aliyekuwa rais wa nchi hiyo Hugo Chavez.
Huku wakilia na kusema ya kuwa kazi aliyo ianza Hugo Chavez wataiendeleza, maelfu ya watu hao walikusanyika kuanzia  hospital ya kijeshi ambayo rais Hugo Chavez alikuwa amelazwa na hadi katika kambi ya kijeshi, ambapo mwili wake utaifadhiwa hadi siku ya Ijumaa 08/03/2013 tayari kwa mazishi.
General, Jose Ornella, ambaye alikuwa pamoja na hayati rais Hugo Chavez alieleza kuwa  rais Chavez amefariki kwa ugonjwa wa moyo, na kabla ya kifo chake alisema   "nisingependa kufa na msinieche nikafa" na hayo ndiyo maneno yake ya mwisho.
Rais, Hugo Chavez 58, alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa salatani, ambapo alikuwa katika harakati za matibabu nchini Kuba.
Viongozi mbali mbali na hasa wale walio kuwa karibu na Hugo Chavez wanatarajiwa kuhudhulia mazishi yake, na badhi ya viongozi wa karibu ni rais Cristina Kirchner wa Algentina, Evo Morales wa Bolivia na Jose Mejica wa Uruguay wamesha wasili nchini Venezuela tayari kwa mazishi ya kiongozi rafiki yao mpendwa.

Korea ya Kaskazini yatishia kuishambuli Marekani.


Pyong Yang, Korea ya Kaskazini - 07/03/2013.Serikali ya Korea ya Kaskazini  imetishia kuishambulia Marekani ikiwa kunamashambulizi yoyote yatakayofanywa kwenye nchi yake.
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya nchi ya Korea Kaskazini  hambaye hakutajwa jina lake alisema"inavyo elekea ni kwamba Marekani ipo mbioni kuanzisha vita zidi ya yetu na huenda vikawa ni vya kunyuklia, na kwa minajili hiyo tunayo haki ya kujibu mashambulizi kwa njia itakayo tumiwa na adui yetu, ili kulinda nchi yetu."
Onyo hilo kutoka Korea ya Kaskazini limekuja  baada ya Marekani na Korea ya Kusini kupanga kufanya pamoja mazoezi ya kijeshi hivi karibuni.
Korea ya Kaskazini ilifanikiwa katika jaribio la kinyuklia lililo fanywa hivi karibuni na kufanya jumuia ya kimataifa kujadiliana ili vikwazo viongezwa kwa nchi hiyo.

No comments: