Saturday, March 9, 2013

Uhuru Kenyatta ashida uchaguzi wa rais Kenya.

Uhuru Kenyatta ashida uchaguzi wa rais Kenya.


Nairobi, Kenya - 08/03/2013. Makamu wa waziri mkuu wa Kenya amechaguliwa kuwa rais wa nchi hiyo baada kupata kura nyingi zaidi ya mpinzani wake.
Uhuru Kenyatta ameshida uchaguzi huo kwa kupata kiasi cha kura za asilimia 50.07% kutoka kwa wapiga kura 6,173,433,  kati ya wapiga kura 12,330,028  waliojiandikisha  kupiga kura.
 Kamati iliyo simamia uchaguzi huo imesema "86% ya watu  ndiyo waliopiga kura  kutoka idadi ya wapiga kura wote walio jiandikisha na hakuna wizi uliotokea na tunaomba wagombea wote waheshimu matokeo ya uchaguzi."
Baada ya kutangazwa uchaguzi huo, kambi iliyo simamia uchaguzi na kuhakikisha ushindi wa Uhuru Kenyatta imetoa ujumbe kwa kusema "tunawashukuru Wakenya wenzetu kwa kukubaliana na mipango yetu na ujumbe wetu."
Hata hivyo kambi ya mgombea aliyeshindwa uchaguzi huo Raila Odinga imesema "hatukubaliani na matokeo hayo na tupo mbioni kufuata sheria ili kupinga matokeo hayo ya kura."
Uhuru Kenyatta atakuwa rais wa nne, tangu Kenya kupata uhuru mwaka 1963 na atafuata nyayo za marehemu baba yake Mzee Jomo Kenyatta ambaye alikuwa rais wa kwanza wa Kenya.
Kenya imekuwa ikiangaliwa na jumuiya ya kimataifa ni kwa jinsi gani mpango mzima wa kupiga kura utakavyo kwisha, hii inatokana na vurugu zilizo tokea wakati na baada ya uchaguzi wa rais mwaka  2007-8, ambapo watu zaidi ya 1000 walipoteza maisha yao na mali nyingi kuharibiwa napia kusabaisha hasara kwa jamii nzima ya Kenya.

Rais Nikolas Maduro kufuata nyayo za hayati Hugo Chavez.


Karakas, Venezuela - 08/03/2013. Makamu wa rais wa Venezuela ameapishwa kuchukua kiti cha urais kilicho achwa wazi na hayati rais Hugo Chavez.
Nicolas Maduro aliapa kwa kusema " na apa kuwa mwaminifu na kufuata nyayo za komredi Hugo Chavez, kuhakikisha ya kuwa kazi aliyo ianza tunaitimiza kufuatia katiba na kwa kushirikiana na wananchi wa Venezuela, Mungu nisaidie."
Hata hivyo kiongozi wa chama cha upinzani nchini humu, Henrique Kaplies kupitia msemaji wake amesema " tunapinga kuapishwa kwa Nikolas Maduro kuwa rais kwani inakwenda kinyume na sheria."
Baada ya kuapishwa, rais Nikolas Maduro alisema " uchaguzi mkuu unahitajika ufanyike mapema iwezekanavyo ili kutimiza katiba inavyo sema."
Wavenezuela bado wapo kwenye maombelezi baada ya kifo cha rais wao Hugo Chavez kilichotokea hivi karibuni.

Vatican yatangaza siku rasmi ya kuanza ibaday ya kumchagua Papa.


Vatican City, Vatican - 08/07/2013. Baraza la kamati ya Makadinali limechagua siku rasmi ya kuanza ibada ya kumchagua mkuu mpya wa kanisa Katoliki duniani.
Habari zinasema uamuzi huo ulichukuliwa siku ya Ijumaa usiku baada ya kuwasili kwa Kadinali 115 ambaye alikuwa akisubiriwa.
Siku ya Jumanne wiki ijayo itakuwa siku rasmi ya kuanza ibada ya kumchagua Papa- mkuu wa kanisa Katoliki duniani lenye waumini wapatao 1.2 billioni,
Ibada hiyo ya kumchagua mkuu mpya wa kanisa Katoliki inafanywa, baada ya Papa Benedikt XVI kujiudhuru wadhifa wake huo mwisho wa mwezi Februari mwaka huu 2013.

Makao makuu ya soka yachomwa moto nchini Misri.


Kairo, Misri - 08/03/2013. Mamia wa watu wenye asira wamevamia makao makuu ya  ya shirikisho la soka la Misri kufuatia uamuzi wa mahakama kuwahukumu azabu ya kifo mashabiki 21 kutokana na vurugu zilizo tokea mwaka 2012.
Watu hao wenye hasira wengi wakiwa wapenzi na washabiki waliunguza jengo la ofisi hiyo ya shirikisho la soka ikiwa ni moja ya kupinga  adhabu iliyo tolewa na mahakama kwa mashabiki wa soka walio husika katika vurugu na kusabaisha vifo wakati timu za Al - Masry na Al-Ahly ya Kairo zilipo kutana kwenye mechi iliyofanyika kwenye mji wa Port Said.
Hata hivyo mahakama iliwaachia watu 25 ambao hawakukutwa na hatia.
Misri imekuwa ikikimbwa na maandamamo ya kila mara tangu kufanyika mapinduzi ambayo yalimn'goa madarakani rais Husni Mubaraka Februari 2011.

1 comment:

Anonymous said...

You're so awesome! I do not believe I have read through anything like that before. So good to discover another person with a few unique thoughts on this topic. Really.. thanks for starting this up. This site is one thing that's needed on the web, someone
with some originality!

Here is my website: tarpaulin