Friday, March 8, 2013

Mwili wa Hugo Chavez kuhifadhiwa kwa kumbukumbu.

Mwili wa Hugo Chavez kuhifadhiwa kwa kumbukumbu.

 Picha hapo juu inaonyesha tangu kuzaliwa kwa rais wa Venezuela Hugo Chavez hadi alipo fariki dunia na mambo ambayo alipitia na kufanya.
 
 Wengi walilia kwa uchungu kiasi cha kuchanganyikiwa , kuto kuamini na kuzimia  wakati wa mazishi ya kumwaaga rais Hugo Chavez.

Picha hapo juu ni za marais tofauti ambao wamekuwepo katika mazishi ya kumuaga hayati rais Hugo Chavez. 

 
 Picha hapo juu yaonyesha baadhi ya watu walikuja kumwaga marehemu rais Hugo Chavez, na wengine wakilia kwa uchungu.

Karakas, Venezuela - 08/03/2013.Maelfu wamekusanyika katika mazishi ya aliyekuwa rais wa Venezuela Hugo Chavez aliyefariki dunia hivi karibuni.
Viongozi kutoka mataifa mbalimbali 55 wameudhuria mazishi yao na huku wanachi wa Venezuela wakizidi kuja mahali ambapo mwili wa hayati  rais Hugo Chavez umelazwa.
Makamu wa rais  Nicolas Maduro alisema" serikali imeongeza siku saba zaidi za kuaga mwili wa Hugo Chavez, ili kumpa fursa kila mwananchi wa Venezela kuweza kuja kumuaga kwa mara ya mwisho rais wetu mwana mapinduzi na alipigania haki zetu sote."
"Vile vile mwili wa hayati rais Hugo Chavez utahifadhiwa katika eneo ambalo mapinduzi ya kijeshi ya kutaka kumtoa madarakani ya mwaka  2002  kushindwa na eneo hilo litaitwa kumbukumbu ya mapinduzi." alisema
Inakadiriwa zaidi ya watu million mbili huenda wakahudhulia kumuaga hayati rais Hugo Chavez.
Kuhifadhiwa mwili huo  kwa hayati Hugo Chavez kunafanana  wanamapinduzi wengine  kama,  Lenin wa Urusi, Ho Chi Mihn wa Vietnam na Mao Zedong wa China. 
Rais wa Urusi Vlamdir Putin katika kukumbuka huusiano kati ya Venezuela na Urusi alisema" Hugo Chavez alikuwa mtu shujaa na mtu ambaye alikuwa mwaminifu na mwangalifu katika kila jambo alifanyalo na kupanga kwa makini.
"Kiukweli alikuwa anataka kuendeleza kuinua maisha ya wananchi wake, amekuwa kinara katika ukumbozi  wa Latin Amerika, na wakati yupo hali alikuwa kama Simon Bolivar, Fidel Castro na Che Guevara." Aliongezea rais Putin.
Kufuatia kifo cha rais Hugo Chavez, makamu wa rais Nicolas Maduro, ataapishwa kuchukua kiti cha urais na ambapo anatarajiwa kuitisha uchaguzi mkuu wa urais katika kipindi cha siku 30 baada ya kifo cha rais kwa mujibu wa katiba ya Venezuela.

Kadinali aliyekuwa akisubiriwa awasili Vatican.
 
Vatican City, Vatican - 08/03/2013. Makadinali wote  wamewasili Vatican City, tayari kwa kuanza ibada ya kumchagua atakaye kuwa kiongozi mkuu wa kanisa Katoliki duniani.
Kadinali Jean Baptiste Phan Minh Man kutoka Vietnam aliwasili akiwa wa mwisho jana na kukamilisha ya makadinali 115 ambao watahusika katika kumchagua Papa - mkuu wa waumini wa kanisa la Katoliki.
Kuwasili kwa Kadinali huyo kutoka Vietnam, kutawezesha kupangwa tarehe maalumu ya kuanza ibada ya uchaguzi huo.
Uchaguzi wa mkuu mpya wa kanisa la katoliki, umekuja baada ya Papa Benedikt XVI kujiudhuru wadhifa wake huo kutokana na sababu za kiafya.

Korea ya Kaskazini yasimamisha mkataba wa amani na jirani yake.

PyongYang , Korea ya Kaskazini - 08/03/2013. Korea ya Kaskazini imesimamisha makubaliano ya amani kati yake na Korea ya Kusini baada ya umoja wa mataifa kuongeza vikwazo kwa nchi hiyo.
Habari kutoka kwa shirika la habari la Korea ya Kaskazini zilisema " tunasimamisha mkataba wa amani na Korea ya Kusini na shambulizi lolote la kushambulia nchi yetu litajibiwa kwa vishindo."
Kutangazwa kwa habari hizi kulikuja baada ya kiongozi wa nchi hiyo Kim Jong Un, kutembelea kambi ya jeshi ambayo ilifanya mashambulizi mwaka 2010, katika kisiwa cha  Yeonpyeong ambacho kinamilikiwa na Korea ya Kusini, na kuwataka kuwa tayari kwa vita.
Kufuatia kauli hiyo, Korea ya Kusini, imefanya mkutano wa dharula ili kujadili hali ya usalama wa nchi hiyo.
Korea ya Kaskazi imewekewa vikwazo zaidi na  umoja wa mataifa, baada ya kufanya jaribio la siraha ya nyukia hivi karibuni.

Walinzi wa UN bado mateka kwa wapinzani wa serikali ya Syira.

Golan Heights,Izrael - 08/03/2013. Wapiganaji wanaopingana na serikali ya Syria wamekataa kuwaachia walinzi wa amani wa umoja wa mataifa walio wateka nyara sikumbili zilizo pita.
Walinzi hao 21, waliopo chini ya umoja wa mataifa wa  kulinda amani katika eneo la Golani Height amabo wanatokea Philippine, walitekwa nyara na wapiganajihao katika eneo la Golan Height, eneo  ambalo walinzi hao wa umoja wa mataifa huwa wanalilinda baada ya eneo hilo kuwahi kuleta mzozo kati ya Izrael na Syria.
Wapiganaji hao waliamua kuwateka nyara Waphillipines hao, ikiwa ni  njia moja ya kutaka jeshi la serikali ya Syria kuacha kushambulia maeneo ambayo wapiganaji hao wanayashikilia karibu na Golan Height.
Tangu kuanza kwa vita vya wenye kwa wenye nchini Syria, mamia ya watu wameuwawa, wengine kuikimbia nchi na baadhi ya nchi kuwaondoa raia wake ambao walikuwa wanafaya kazi nchini humo.

1 comment:

Anonymous said...

We absolutely love your blog and find almost all of your post's to be what precisely I'm looking
for. Do you offer guest writers to write content in your case?
I wouldn't mind writing a post or elaborating on many of the subjects you write concerning here. Again, awesome web log!

Feel free to visit my web blog; trapan