Tuesday, March 12, 2013

Makama ya kimataifa yamwachia mmoja wa watuhumiwa kutoka Kenya.
 
The Hague, Uhollanzi - 12/03/2013. Mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai imefuta kesi ya mmoja ya washukiwa wa vurugu na mauaji yaliyo tokea nchini kenya kati ya mwaka 2007-8. baada ya uchaguzi mkuu na watu zaidi ya 1000 walipoteza maisha.
Francis Muthaura ambaye ni mmoja wa washitakiwa alifutiwa kesi, baada ya kushindwa kupatikana ushahidi wa kutosha.
Mwanasheria mkuu wa mahakama hiyo Fatou Bensouda alisema " hadi sasa hakuna ushaidi kamili unaweza kutumika ,kwani mashahidi hawajajitokeza japo jitihada zimetumika ili kupata ushahidi, na wengine waneshindwa kutoa ushahidi kwa kuofia maisha yao."
Baada ya kufutwa kwa kwesi hiyo ya Muthaura, mwanasheria anaye mwakilisha Uhuru Kenyatta  amesema "anabidi pia kesi zidi ya Uhuru ifutwe pia."
Kufutwa kwa kesi hiyo, kumekuja siku mbili baada ya Uhuru Kenyatta kushinda kiti cha urais wa Kenya kufuatia kura zilizo pigwa hivi  karibuni nchini humo.
 
Hali ya kidpomasia kati ya Venezuela na Marekani yaingia sura mpya.
 
 
Washington, Marakani - 12/03/2013. Serikali ya Marekani imewafukuza wafanyakazi wa kibalozi wa Venezuela ambao walikuwa wakifanya kazi nchini humo.
Uamuzi huo wa kuwafukuza wafanyakazi hao umekuja baada ya serikali ya Venezuela  kuwafukuza  waambata wa kijeshi wa Marekani waliokuwa wakifanya kazi nchini Venezuela.
Venezuela na Marekani zimekuwa na mahusiano yanayo yumba, tangu enzi za uhai wa rais Hugo Chavez ambaye aliishitumi Marekani kwa kudai ilitumia mamluki kutaka kuipindua serikali yake.
Ofisi za ubalozi za Marekani zilizopo nchini Venezuela zimekuwa wazi baada ya hayati rais Hugo Chavez kumkataa balozi aliye pendekezwa na serikali ya Marekani.
 
Malkia wa Uingereza akosa kuhudhuria siku ya Commonwealth.
 
London, Uingereza - 12/03/2013. Malkia wa Uingereza amehairisha kuhudhuria sherehe za nchi wanachama wa Commonwealth.
Malkia Elizabeth II 86, ambaye alikuwa amelazwa hivi karibuni  kutokana na kusumbuliwa na tumbo na kufanyiwa matibabu baadaye kuruhusiwa kurudi nyumbani kwa mapumziko.
Kwa mujibu wa habari kutoka Buckingham Palace makazi aishio Malkia zinasema  " Malkia Elizabeth II anaendelea vizuri."
Japokuwa Malkia hakuhudhulia sherehe hiyo, aliweza kusaini kitabu ambacho kinahusisha mamlaka na mahusiano ya nchi wanachama wa Commonwealth.
Ni miaka 20 imepita tangu Malkia Elizabeth II kushindwa kuhudhulia sikuku ya nchi wanachana wa Commonwealth,
Nchi wanachama wa umoja huo ni nchi zilizo kuwa makoloni ya Mwingereza kabla ya nchi hizo kupata uhuru.
 
Nelson Mandela atoka hospital.
 
Johannesburg, Afrika ya Kusini -12/03/2013. Rais wa zamni wa Afrika ya Kusini ameruhusiwa kutoka hospitali baada ya kumalizika kufanyiwa uchunguzi wa afya yake.
Nelson Mandela 94,  alikuwa amelazwa siku ya Jumamosi, ili kuangalia kiundani mwenendo wake wa kiafya   na  aliruhusiwa  na kurudi nyumbani.
Mwezi Desemba, Nelson Mandela, alilazwa hospital kwa wiki tatu, baada ya kuwa na matatizo katika mapafu na kufanyiwa upasuaji mdogo.
Msemaji kutoka ofisi ya rais Jakob Zuma alisema "kulazwa huko kwa Mandela, ni moja ya hatua ya kutizama afya yake, kutokana na umri aliyo nao."
Nelson Mandela mmoja wa viongozi wa Afrika ya Kusini waliopigana katika kuutokomeza ubaguzi wa rangi na kufanikisha kuleta haki sawa kwa wazalendo wa Afrika ya Kusini.





No comments: