Tuesday, December 31, 2013

Jeshi la serikali la rais Salva Kiir lazidiwa nguvu.

Jeshi la serikali la rais Salva Kiir lazidiwa nguvu.


Bor, Sudani ya Kusini - 31/12/2013. Wapiganaji wanao pingana na  serikali ya Sudan Kusini, wa mekamata  mji wa Bor, baada ya kupambana vikali na  wajeshi wa serikali na kulizidi nguvu.

Akiongea baada ya kuukamata mji huo,  Moses Ruai ambaye ni msemaji wa jeshi la upinzani amesema " Mji wa Bor upo mikononi mwetu, na hivyo makao makuu wa jimbo la Jonglei ni yetu pia."

Wakati mapambano yanaendelea, kiongozi wa upinzani  na ambaye jeshi lake limetwaa mji wa Bor Riek Machar amekataaa kukutana na rais Salva Kiir ili kufanya mazungumzo ya kuleta amani ambayo yalitarajiwa kufanyika jijini Addis Ababa Ethiopia hii karibuni.

Hata hivyo kwa upande wa serikali, waziri wa mambo ya nchi za nje wa Sudan ya Kusini, Barnaba Marial Benjamin, amesema " mpango wa Riek Machar kushirikiana na kugawana madaraka na rais Salva Kiir haupo tena, na hii ni kutokana na kuwa Machar ni kiongozi wa jeshi linalotaka kupindua serikali halali ya wanchi wa Sudan ya Kusini."

Tangu kuanza kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe,  kwenye nchi changa ya Sudan ya Kusini na ambayo ilipata uhuru wake 2011, watu wapatao 1000 wamesha poteza maisha yao, wengi kujeruhiwa na mali nyingi kuharibiwa kutokana na vita hivyo.

No comments: