Sunday, December 22, 2013

Mahakama ya Uingereza yatupilia mbali kesi ya mwanasiasa wa Libya.

Mahakama ya Uingereza yatupilia mbali kesi ya mwanasiasa wa Libya.


Tripol, Libya -22/12/2013.  Mahakama  jijini London imetupilia mbali kesi ya mmoja wa kiongozi waliosaidia kuung'oa utawala wa Muammar Gaddafi 2011.

Akitoa hukumu kabla ya kutupilia mbali kesi ya Belhaj imedai Jaji  Simon alisema, " kwa kuangalia mwenendo mzima wa kesi hii, matendo mengi yalitendeka Malasyia, Thailand and  Libya na ambapo ni  nje ya nchi na hivyo hayahusiki na Uingereza."

Akiongeaa baada ya  hukumu kutolewa Belhaj  alisema " Maelezo ninavyo fahamu ni kuwa ikiwa kesi hii itaendelea, wanadai kuwa itawaaibisha Marekani, navilevile itahatarisha usalama wa taifa la Uingereza."

" Lakini hata hivyo kwa kupitia mwanasheria wangu tutapambana hadi tupate ushindi na kwani haki itatendeka mwisho wa siku."

Abdul - Hakim Belhaj,ambaye kwa sasa amekuwa mmoja wa viongozi wa siasa nchi Libya, ambaye amemeushitaki uongozi wa juu wa ofisi ya mambo ya nje wa Uingereza na mkuu wa MI6, Sir Mark Allen  kwa kosa la kumkamata kwa nguvu na kumpeleka  Libya wakati wa utawala wa Gaddafi na kuteswa.

Kesi ya kuwakamata watu kwa nguvu na kuwapekeka katika maeneo ya mateso, zimekuwa zikiiandama serikali ya Uingereza, na hata baadhi ya majaji kudai kuwa sheria ilivujwa na wakuu wa usalama wa Uingereza katika kufanya vitendo hivyo.

Mkwe wa Bin Osama Bin Laden aongezewa mashitaka.

New York,Marekani - 22/12/2013. Mahakama jijini New  York katika kitongoji cha Manhattan, imemuongezea mashitaka mawili zaidi aliyekuwa mkwe wa mkuu wa kundi la Al Qaeda Osama Bin Laden.

Suleiman Abu Ghaith, ameongezewa mashitaka ya  kusaidia kimali na kutoa habari katika kundi la Al Qaeda kuweza kufanya mashambulizi yake nchini  Marekani ya Sept 11 2001.

Suleiman Abu Gaith ambaye ni mzaliwa wa Kuwait alikutwa hapo awali na kosa baada ya kuongea maneno yakuunga mkono mashambulizi ya Sept 11. kwa kusema " tunafuraha kuona wapiganaji wa Mijaidini wameweza kushambulia nchi Marekani kwa uwezo wa Mungu na mapema dunia itashuhudia kushambuliwa kwa miradi ya Marekani na Waizrael."

Mashambuzi ya Sept, 11-2001 nchini Marekani yalisababisha vifo vya watu 3000, na watu kadhaa kuumia na mali nyingi kuharibiwa baada ndege zilizo kuwa zimetekwa na magaidi wa kundi la Al Qaeda kufanya mashambulizi Trade Centre New York, Pentagon na Pennsylvania.

Suleiman Abu Gaith anatarajiwa kufikishwa mahakamani kusikiza kesi zake Februri 3, 2014.

No comments: