Friday, December 20, 2013

Rais Vladmir Putin aonyesha huruma yake. 
 

Moscow, Urusi -20/12/2013. Rais wa Urusi Vladimir Putin ametoa msamaha kwa aliyekuwa bilionea ambaye alikuwa amefungwa kwa makosa ya rushwa na kukiuka matumizi ya usambazaji wa pesa wa nchi ya Urusi.
 
Mikhail Khodorkovsky, ambaye amekaa jela miaka 10, baada ya kuhukumiwa kwenda jela mwaka 2003 aliachiwa huru leo kutoka katika gereza lililopo katika mji wa Karelia km 1,000 toka jiji la Moscow, baada ya rais Putin kutoa msamaha kutokana na sababu za kibinadamu na kiutu.
 
Akithibitisha kuachiwa na kuwasili Ujerumani, aliyekuwa waziri wa mambo ya nje Hans-Dietrich Genscher amesema " Mikhail Khodorkovsky amewasili katika jiji la Berlin kwakutumia ndege binafsi na mimi ndo nimemchukua toka kiwanja cha ndege."
 
Kuachiwa kwa Khodorkovsky kumekuja baada ya jitihada za Kansela  Waujerumani Angela Markel kukubalika na rais Putini ambapo kila walipo kutana aliomba serikali ya Urusi kumwachia Mikhail Khodorkosky.
 
 
Edward Snowden azidi kuziumbua Marekani na Uingereza.
 
 
London Uingereza - 20/12/2013. Sakata la shirila la kijasusi la Uingereza  na mshirikiwa wake Marekani kugundulika kuwa walikuwa wanachunguza na kusikiliza mazungumzo na mawasiliano ya simu na mtandao yamefichuliwa kwa mara nyingine tena.
 
Magazeti ya The Guardian Uingereza, The New York Time Marekani  na Der Spiegal la Ujerumani yameandika zaidi ya  majina 1000 ya watu wambao walikuwa wakuchunguzwa, kufuatiliwa nyendo zao kimtandao na kusikilizwa simu zao na  mashirika ya kijasusi ya NSA ya Marekani na GCHQ ya Uingereza  kinyume cha sharia za kimataifa.
 
Magazeti hayo yameandika kuwa "NSA na GCHQ wamechunguza nyendo za viongozi umoja wa Ulaya, mashirika ya haki za binadamu, waziri mkuu wa Izrael na pia zaidi ya nchi 60  hasa viongozi wa Afrika na familia zao, na pia  shughuli zinazo endeshwa na Umoja wa Mataifa na viongozi wake."
 
Kutolewa kwa ripoti hizi mpya ambazo chanzo chake ni raia wa Marekani Edward Snowden ambaye alikuwa mfanyakazi wa NSA na  kwa sasa yupo ukimbizini nchini Urusi, kumekuja baada ya ile kashfa ya kuwa mashirika hayo kwa pamoja yalikuwa yanashirikiana kusiliza mazungumzo ya  Kansela wa Ujerumani Angela Markel na kuleta mtafaruku wa kidiplomasia kati ya nchi hizo.
 
 
 Chama tawala Afrika ya Kusini njia panda na washirika wake.
 
Pretoria, Afrika ya Kusini - 20/12/2013. Moja ya chama kikuu  cha wafanyakazi nchini Afrika ya Kusni kimetangaza kutounga mkono chama tawaza cha ANC - (African National Congress) wakati wa uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika 2014. 
 
NUMSA ambacho ni chama cha wafanyakazi wa viwanda vya vyuma,  ambacho kinawanachama zaidi ya 3,00,000, kimetoa azimio hilo wakati wa mkutano wa wanchama hao uliyofanyika hvi karibuni jijini Johannesburg.
 
Kiongozi wa chama hicho Irvin Jim  alisema  "NUMSA inajitoa katika kuunga mkono ANC, kwani chama cha ANC kimekuwa hakifanyi jitihada ya kupambana na rushwa na kupunguza umasikini na ufukara kwa wanachi wake na pia kukiuka ilani ya chama."
 
NUMSA imekuwa bega kwa bega na ANC tangu mwaka 1994, na hivi miaka ya karibuni imekuwa ikivutana na ANC kwa kudai ya kuwa chama cha ANC hakitekelezi kazi zake vizuri na kuwa kinatizama sana upande wa uchumi huria ambao haunufaishi watu walio wengi nchi Afrika ya Kusni.
 
ANC imekuwa na wakati mgumu katika sera zake kukuza uchumi chini Afrika ya Kusini, kutoka na na msukumo nguvu uchumi wa kuleta mabadiliko kuruhusu kuwepo na uchumi huria, jambo ambalo vyama vingi vya wafanyakazi vimekuwa vikiupinga mfumo huo.
 
 
Jela maisha ukiwa shoga nchini Uganda.
 
 
Kampala, Uganda - 20/12/2013. Bunge la Uganda limepitisha musuada ambao utakuwa wa kifungo cha maisha kwa mashoga wa kiume na wakike katika kura zilizo pigwa bungeni humo leo.
 
Uamuzi wa bunge la Uganda kupigia kura ya ndiyo ya kupitisha adhabu ya kukaa jela maisha, imekuja maada ya adhabu ya awali ya kunyongwa ambayo ilipingwa vikali na wana harakati wa kimataifa wa kutete haki za mashoga.
 
Msemaji wa bunge la Uganda amesema "Ushoga  ulikuwa ni haramu tangu enzi za serikali ya kikoloni nchini Uganda na kama tukiachia tabia hii itatualibia jamii nzima ya Waganda."
 
Sheria ya kuukataza  ushoga nchini Uganda  ilipitishwa kwa mara ya kwanza nchini humo mwaka 2009 ambapo spika wa bunge Rebeka Kadaga alisema "kupitishwa kwa sheria ya kupinga ushoga ni zawadi nzuri ya Krismasi kwa Waganda."
 
Wabunge wa Uganda wamekuwa wakidai yakuwa kanisa la Kievanjilisti la asili ya kuutoka Marekani limekuwa likiunga mkono ushoga na linakampeni ya kuusambaza ushaoga barani Afrika, madai ambayo wakuu wa kanisa hilo kutoka Marekani walikanusha.
 
Hata hivyo musuada huo utakuwa sheria baada ya rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museni kusaini kuwa sheria.
 
 
Baraka Obama aonya kuhusu mapigano nchini Sudani Kusini.
 
Juba, Sudani ya Kusini - 20/12/1213. Rais wa Marekani amezitaka pande zote zinazo pigana nchini Sudani Kusini kusimamisha mapigano haraka iwezekenavyo.
 
Baraka Obama alionya kwa kusema kuwa " Inabidi pande zote zinazo pigana nchi Sudani ya Kusini kucha mara moja vita, kwani vinaweza kuleta maafa makubwa kwa jamii na hatimayake kuwa vita vya wenyewe kwa wenyewe."
 
" Kitendo cha kutumia siraha ili kuweza kupata nguvu za kisiasa ndani ya nchi ni kitendo kibaya, na kila upande lazima wasikilize busara za kimataifa." Alimalizia rais Obama.
 
Wakati amani nchini Sudani ya Kusini imevurugika, mwanajehi wa umoja wa Mataifa kutoka nchi Indi amefariki dunia na mmoja kujeruhiwa, baada ya kushambuliwa ya wapiganaji wanao muunga mkono mpinzani wa serikali ya  ambaye alikuwa makamu wa rais Riek Machar kwa  kushambulia ngome ya makazi ya wafanyakazi wa umoja wa mataifa katika mji wa Bor.
 
Hadi kufikia sasa, zaidi ya watu 500 wamesha potea maisha yao wakiwemo wanajeshi 100, tangu mapambano yalipo anza, baada ya serikali ya rais Salva Kiir kudai ya kuwa imegundua mbinu za kutaka kuipindua serikali, zilizo kuwa zimepangwa na makamu wa rais Riek Machar, ambaye mmpaka sasa ajulikaani mahaali alipo.
 
 
Rwanda kupeleka majeshi yake Afrika ya Kati.
 

Kigali, Rwanda - 20/12/2013.Serikali ya Rwanda imekubali ombi la umoja wa Afrika kupeleka wanajeshi wake katika nchi ya Afrika ya Kati ili kusaidia kurudisha amani.

Akithibitisha hayo, kwa kutukia mtandao wa twiter, waziri wa mambo ya nje wa Rwanda, Louise Mushikiwabo aliandika " Rwanda iliombwa kuchangia wanajeshi nchini Afrika ya Kati, na wanajeshi wa Rwanda wapo katika matayarisho kuwasili jiji Bangui mapema iwezekanavyo"

Uamuzi wa Umoja wa Afrika kuomba msaada kwa jeshi la Rwanda umekuja baada ya ya hali ya amani katika nchi ya Afrika ya Kati kuwa mbaya zaidi, ambapo imefikia kuwa ugomvi wa kidini, kati ya  kundi linalo julikana kama Anti-Balaka la Wakristu kuanza kushabuliana na kundi la  Kiislaam la Seleka.

Kuchafuka kwa amani katika nchi ya Afrika ya Kati, kumesababisha zaidi ya watu 6,00,000 kukimbia makazi yao na huku kati yao 2,00,000 wakiokea jiji Bangui.

No comments: