Monday, December 23, 2013

Viongozi wa siasa nchi Nigeria wavutana.

Viongozi wa siasa nchi Nigeria wavutana.

Lagos, Nigeria - 23/12/2013.Mvutano kati ya rais wa sasa wa Nigeria Goodluck Jonathan  na rais mstaafu wa nchi hiyo Olusegun Obasanjo umefikia hatua nyingine baada ya malumbano ya chini kwa chini ambayo yamekuwa yakiendelea kwa muda sasa kati ya viongozi hao.

Mvutano huo umewekwa wazi na  rais Goodluck Jonathan baada ya kuamua kujibu barua iliyotumwa na aliyekuwa rais wa nchi hiyo Olugun Obasanjo kwa kuandika "baba Obasanjo, nasikitika saana kwa kunishutumu mimi na serikali yangu kuwa inafanya kila njia kuwauwa baadhi ya wanasiasa na kuna watu 1000  ambao wanafuatiliwa na wafanyakazi wa usalama ambao wamefundishwa kuuwa wale wote wanao onekana kuenda kinyume na serikali."

"Napenda kuualifu kuwa hayo unayo sema na kuandika siyo kweli, na nimeagiza uchunguzi ufanywe ndani ya serikali na pia mashirika ya kutetea haki za binanadamu niemaagiza yahusishwe katika uchunguzi huu ambao unania ya kuweka ukweli bayana.

Hali ya kutoelewana kwa viongozi hao kulianza baada ya rais mstaafu Obasanjo kumtaka rais Goodluk Jonathan kutogombe tena kiti cha urais, baada ya kupoteza viti 37 katika bunge la wawakilishi  kutoka na  wabunge 37 wa chama cha PDP kukuacha chama hicho na kujiunga na chama cham APC.

Rais Goodluck Jonathan na rais mstaafu Olugun Obasanjo wote ni wanachama wa PDP na wameweza kupata viti vya urais kupita chama cha PDP. 

Kwa mara ya kwanza Walibya wakubwa na mauaji ya kujitolea muhanga.

Tripol, Libya - 23/12/2013. Watu saba wamefariki baada ya muuaji wakujitolea muhanga kujilipua karibu na kizuizi kilichopo km 30 kutoka  jiji la Tripol.

Hii ni mara ya kwanza kwa  mauaji ya kujitolea muahanga  kutokea nchini Libya tangu kuangushwa kwa  utawalawa Muammar Gaddafi 2011.

Habari kutoka idara ya usalama ya nchi zinasema " hali imezidi kuwa siyo nzuri hasa katika swala la kiusalama, na hali ya kiusalama ya miji wa Benghazi na Tripol imekuwa katika hali tete kila kukicha "

Tangu kuangushwa kwa utawala wa Muammar Gaddafi, Libya imekuwa na vikundi tofauti vya kijeshi ambavyo vimegawanyika kutokana na kutoa afikiana baada ya vita vya kuipindua serikali kwa msaada wa Uingereza, Ufaransa na chini ya NATO jambo ambalo limekuwa likiangaliwa kuwa huenda likaleta mzuko wa kuanza vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Libya.

Mgunduzi wa AK-47 afariki dunia.



Moscow, Urusi - 23/12/2013. Mgunduzi wa siraha ya aina ya AK-47 ambayo imekuwa maarufu na kuwa moja ya siraha kipenzi  kimapambano amefariki dunia.

Mikhail Kalashnikov 94, amefariki dunia na kuacha historia ambayo itakuwa akikumbukwa  kwa muda mrefu kwa umairi wake wa kugundua siraha ambayo hadi leo inaleta  changa moto katika matumizi yake sehemu mbali mbali duniani.

Akiongea baada ya kupata habari ya kifo Mikhail Kalashnikov, rais wa Urusi Vladmir Putin alisema " nivigumu kukubali ya kuwa  hatupo naye tena Mikhail Kalashnikov, na tumepoteza mtu muhimu katika jamii nzima ya Kirusi kwani Kalashnikov alikuwa  mzalendo aliye tetea kwa  kupigania nchi yake wakati wa maisha yake yote."Alimalizia rais Putin.

Mikhail Kalashnikov, aligundua siraha ya AK-47  mwaka 1947 baada ya kupona majeraha ya bega ambayo aliyapata wakati akiwa vitani alisema " nilipata hili wazo baada ya kuzinduka kitandani wakati nilipo kuwa nimelazwa hospital kwa matibabu."

Wakati wa uhai wake mara kwa mara Mikhail Kalashnikov, amekuwa akisema yakuwa hajutii ugunduzi wake, kwani ulisaidia kulinda  heshima ya Urusi."

Siraha ya AK-47 imekuwa ikitumika katika kila aina ya mazingira ya kivita na inasifika kwa kutokuwa na matatizo ya aina yoyote katika matumizi kama siraha nyingine,  na kwa miaka 60 sasa imekuwa ni siraha hatari duniani kutokana na umairi wake.

No comments: