Rais wa Sudan ya Kusini akubali suruhu.
Juba, Sudan ya Kusini - 27/12/2013. Rais wa Sudani ya Kusini Salva Kiir amekubali kusimamishwa mapambano ya kivita kati yake na kundi ambalo linaunga mkono mpinzani wake Riek Machar ambaye alikuwa makamu wake wa urais.
Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya na waziri mkuu wa Ethiopia Hailemariam Desalegn waliweza kumshawishi rais Kiir kukubali kusimamishwa kwa vita baada ya kukutana na kujadiliana katika mji mku wa Juba.
Akiongea baada ya rais Kiir kukubali kusimamishwa kwa vita , rais Uhuru Kenyatta amaesema " nimefurahishwa na kitendo cha rais Kiir kukubali kusimamisha vita, kwani nafasi iliyopo ni finyu, na naomba ijulikane kuwa IGAD haitaruhusu kuona rais aliyechaguliwa kihalali anatolewa madarakani kwa nguvu"
" Na nawaomba Riek Machar na rais Salva Kiir kuhakikisha amani inarudi nchini Sudani ya Kusini kwani vita siyo suruhu ya kuleta maendeleo ya nchi." Aliongeza rais Uhuru Kenyatta.
Jitihada za kusimamisha vita nchini Sudan ya Kusini zinasimamiwa na (Inter-Government Authority on Develoment -IGAD) ikiwa na nia ya kusimamia uongozi bora na kuhakikisha kuondoa migogoro ya kisiasa katika nchi zilizopo Afrika ya Mashariki na Kati.
Mvutano kati ya Udugu wa Kiislam na serikali waiweka amani ya Misri njia panda.
Kairo, Misri -27/12/2013. Waandamaji wanaounga mkono kundi la Undugu wa Kiislaam ( Muslim Brotherhood) wamepambana polisi katika matukio tofauti yaliyo tokea nchi Misri tangu kutangazwa kuwa kudi hilo ni kundi la kigaidi nchi Misri.
Katika maandamano hayo watu watatu wamepoteza maisha jiji Kairo, na wengine kujeruhiwa vibaya wakati polisi wa kuzuia ghasia walipo pambana na waandamanaji, na zaidi ya watu 265 wamekamatwa kutokana na vurugu hizo,
Tangu kutolewa madarakani kwa nguvu kwa rais Mohammed Morsi, hali ya amani na utulivu imechafuka nchini Misri, na hii inatokana na wanachama wanaounga mkono kundi la Undugu wa Kiislaam kutaka rais Mohammed Morsi arudishwe madarakani na pia wanapinga kitendo cha serikali kukitangaza cha chama cha Udugu wa Kislaamu kuwa cha kigaidi.
Saada al Hariri alia na Hezbollah.
Mohamad Bahaa Chatah 62, aliuwawa baada bomu kulipuka katikati ya msafara wake wakati alipo karibia ofisi za majengo ya serikali ambapo alikuwa njiani keelelea kwenye mkutano wa kuipinga Syria uliyokuwa ukiongozwa na Saad al Hariri
Mlipuko huo pia uliharibu majengo na kusababisha baadhi kushika moto na kuungua vibaya.
Akiongea kuhusu mauaji ya Chatah, Saada al Hariri alisema " watu walio muua Chatah ni wale ambao wanataka haki isitendeke kufuatia kuwepo na kesi inayotarajiwa kuanza kwenye koti ya kimataifa mjini Hague Uholanzi mapema mwezi January 2014."
Mohamad Chatah, alikuwa mkosoaji mkuu wa serikali ya Syria, amekuwa akipinga na kulaumu kundi la Hezbollah kwa kushirikiana na rais Bashar al Assad katika vita vinavyo endelea nchi Syria.
Kifo cha Chatah kimekuja wiki tatu kabla ya kuanza kesi zidi ya baadhi ya wanachama wa Hezbullah ambao wanasadikiwa kuhusika katika mauaji ya mwaka 2005 ya waziri mkuu wa Lebanoni Rafik al Hariri ambaye ni baba wa Saad al Hariri,
1 comment:
http://pay4shares.com/?share=111024
Post a Comment