Wednesday, December 11, 2013

Matumizi ya Bangi yahalishwa nchini Uruguay.

Mwili wa Nelson Rolihlahla Mandela kuonyeshwa kwa mara ya mwisho.


Pretoria, Afrika ya Kusini - 11/12/2013.Familia, ndugu na jamaa pia  maelfu ya watu wamajipanga mstari ili kumuaga na kumona kwa mara ya mwisho aliyekuwa rais wa kwanza mweusi waAfrika ya Kusini Nelson Mandela katika jengo  serikali - Union Building lililopo jijini Pretoria.

Mwili wa marehemu Nelson Mandela ulikuwa umewekwa wazi kwa wanchi, wazalendo na watu kutoka mataifa tofauti ili kutoa heshima zao za mwisho. Mwili wa Nelson Mandela utaonyeshwa kwa watu kwa muda wa siku tatu.

Kufuatia kitendo cha watu kuruhusiwa kuona mwili wa  Nelson Mandela kwa mara ya mwisho, watu kadhaa waliishiwa nguvu huku wakilia na wakati huohuo wengine kuzimia.

Mwili wa hayati rais wa kwanza wa Afrika ya Kusini Nelson Mandela utapelekwa kupumzishwa Qunu katika mji wa Umtatha.

Matumizi ya Bangi yahalishwa nchini Uruguay.


Montevideo, Uruguay, - 11/12/2013. Bunge la Senete la Uruguay limepitisha kwa kura nyingi uamuzi wa zao la bangi kuwa halali. Kura ambazo 16 kati ya 29 ziliunga mkono uhalali wa  kulima bangi na kuwa inatumika bila kuwa kosa la jinai nchini humo.

Kufuatia kukubali kwa wabunge wa senete, rais wa Uruguay Jose Mujic atasahini muswaaada huo kuwa sheria.

Mmoja  kati ya wabunge waliopiga kura ya kukubali uhalali za zao la bangi Seneta Roberto Conde amesema " uamuzi wa bunge kupitisha  muswaada huu, ni kwa sababu ambazo hazikuweza kuzuilika.

Bangi ni moja ya zao amblo linatumika na watu wakila lika, na inaeleweka kuwa inamadhara madogo sana katika jamii."

Hata hivyo shirika la kupambana na madawa ya kulevya limepinga vikali kitendo cha bunge kukubali kuruhusu matumizi ya bangi kwa kusema "nikinyume na makubaliano ya mwaka 1961 ambapo Uruguay ni mwanachama."

Uruguay imingia katika  kundi la nchi kama  Netherlands na Spain ambazo sheria za matumizi ya bangi zinruhusu matumizi ya zao hilo kwa matumizi ya mtu binafsi.




No comments: