Friday, December 13, 2013

Mazungumzo ya Irani na nyuklia yaingia dosari.

Tehran, Iran 13/12/201. Iran imesimamisha mazungumzo ya kinyuklia na nchi  sita kubwa duniani baada ya  Marekani kuiwekea vikwazo Iran.

"Umuzi wa Marekani kuyaongeza makampuni 19 ya kutoka Iran katika vikwazo vya kibiashara,kumeelezwa na Tehran kama ni ujumbe unao onyesha kuwa  juhudi za mazingumzo ya Iran na mpango wake wa kujadili maendeleo yake ya kinyuklia ni bure." Alisema Abbas Araghchi ambaye ni  makamu wa waziri wa mambo ya nchi za nje wa Iran.
 
Hata hivyo msemaji wa serikali ya Marekani Jay Carney  amesema kuwa "kitendo cha kuwekewa vikwazo makampuni 19 ya  Iran hakikuvunja mkataba wa Novemba 24"

Mazungumo kati ya nchi sita, China, Uingereza, Fransa, Germani, Urusi na Marekani kuitaka Iran kuachana na mpango wake wa kuendelea kuzalisha  nguvu za kinyuklia ulikuwa umesha fikia katika kipindi cha kukubaliana, baada ya mazungumzo ya Novemba 24, ambapo Iran na nchi sita ziliafikiana kimsingi kufikia makubaliano.

Rufaa ya Victoire Ngabire yakataliwa.

Kigali, Rwanda - 13/12/2013. Maakama ya rufaa jiji Kigali, imetupilia mbali rufaa ya maombi ya aliyekuwa kiongozi wa chama cha upinzani nchini humo Victorie Ngabire.

Kufuatia kukataliwa kwa rufaa hiyo, Victoire Ngabire ataendelea kutumika kifungo cha miaka 15 jela, baada ya kukutwa na hatia na makama jiji Kigali kwa kosa la kuchonganisha makabila, na vilevile kueneza chiki za mauaji ya kimbari yaliyo fanyika  Rwanda 1994.

VictoireNgabire mama mwenye watoto watatu na mume, alikamatwa mwaka mwezi Oktoba 2010, kwa kosa la kudai ya kuwa pia wale "Watutsi walio husika katika kuua wa Hutu nao washitakiwe."

1994, dunia nzima ilishikwa na mstuko, baada ya mauaji ya watu zaidi ya 800,000 kuuwawa, kutokana na visa vya kikabila kati ya  Watutsi na Wahutu, na Wahutu walio wengi waliuwawa.

Victoire Ngabire 45 ambaye alirudi nchi Rwanda kama kiongozi wa chama cha  Nguvu za Muungano wa Demokrasia Unified Democratic Force (UDF) baada ya kukaa nje ya nchi kwa muda wa miaka 16.

Kim Jong Un ammgeuka mjomba wake.

Pyong Yang, Korea ya Kaskazini - 13/12/2013. Mjomba wa kiongozi na aliyekuwa mkuu wa pili katika uongozi wa jeshi na madaraka yote wa Korea ya Kaskazini amenyongwa kwa mujibu wa shirika la habari KCNA la nchi hiyo.

"Jang Song Thaek, ambaye anadaiwa kwa kukutwa na hatia ya kutaka kupindua serikali, kula rushwa na kuvunja miiko ya serikali." Liliripoti shirika hilo la habari la Korea ya Kaskazini KCNA.

Kunyongwa kwa Jang Song Thaek, kumetamfsiliwa kuwa ni moja ya myumbo wa kiungozi, kwani inaaminika kuwa " Jang Sing Thaek ndiye aliye simamia na kumsaidia  kiongozi wa sasa Kim Jong Un hadi kuweza kuwa imara katika uongozi aliyo nao sasa.

Jang Song Thaek, alikuwa ni mtu wa karibu wa kiongozi wa Korea ya Kaskazini marehemu Kim Jong Il ambaye ni baba wa kiongozi wa sasa Kim Jong Un.

M23 na serikali ya DRC Kinshasa wasaini mkataba wa amani.



Kinshasa, DRC - 13/12/2013. Serikali ya DRC imetiliana sahii makubaliano ya kusimamisha mapigano na kundi la waasi M23 linalo pingana na serikali ya Kinshasa.

Mkataba huo wa makubaliano ambao umewekwa sahii jijini Nairobi Kenya, na kukubaliana  yakuwa wale wapiganaji wa M23 wataaungana na  wanajeshi wa jeshi la serikali na vilevile kusalimisha siraha na vifaa vyote vya kivita ambavyo vilikuwa vinatumika na kundi la M23.

Akisisitiza baada ya kutiliana sahii ya amani, msemaji wa serikali ya DRC, Lambert Mende amesema "katika mkataba huu ni kwamba wale wote walio husika katika uvunjaji wa hali za binadamu, na kutakiwa kujibu mashitaka kwa mujibu wa sheria za kimataifa za kulinda haki za binandamu hawata husishwa na wala kupewa msamahaa kama tulivyo kubaliana."

M23, ni kundi la wapiganaji wa kijeshi, ambao wanaaminika wengi wao wanaasili ya Kitutsi,  na wamekuwa napigana na serikali ya Kinshasa, kwa madai ya kuwa  serikali ya DRC haiwatendei haki.

No comments: