Wednesday, December 25, 2013

Rais wa Uruguay awapa zawadi ya kufunga mwaka 2013 wanachi wake.

Rais wa Uruguay awapa zawadi  ya kufunga mwaka 2013 wanachi wake.


Montevideo, Uruguay - 25/12/2013. Rais wa Uruguay amewapa salamu za Kristmas na mwaka mpya wanchi wake wa Uruguay kwa kusaini mkataba wa kuruhusu kilimo cha bangi na matumizi yake  nchini humo.

Akithibitisha kusainiwa kwa muswada huo, Diego Canepa ambaye ni msemaji kutoka ofisi ya rais amesema " rais Jose Mujica ametia sahii kuwa sheria kuruhusiwa kulima na kuuzwa bangi nchini humo siku ya Jumatu, na hii inatokana na wabunge kupiga kura kuunga mkono muswada huo,  na sheria hii itaaanza rasmi kutumika kuanzia April 9 2014."

Rais  Jose Mujica ambaye ndiye mwanzishi wa kampeni ya kuruhusiwa matumizi ya bangi nchini humo kwa kuamini kuwa kuruhusu  kilimo cha zao hilo nchini mwake kutapunguza uharamia na biashara haramu ambayo mara kwa mara umesababisha mauaji na kupunguza amani katika jamii ya Wauruguay.

Hata hivyo shirika la ukimataifa la kupambana na madawa ya kulevya limelaani kupitishwa kwa sheria hiyo na kudai ya kuwa Uruguay imevunja sheria za kimataifa ambapo ni nchi wanachama.

Papa Fransis aomba kuwepo na amani duniani.

Vatican City, Vatican - 25/12/2013.Mkuu wa kanisa Katoliki dunia Papa Faransis ameto wito kwa kila mtu kushiriki katika kulinda na kuleta amani duniani.

Akizungumza katika misa ya kusherekea siku ya kuzaliwa kwa Yesu Kristu, Papa Fransis amesema " amani ni imekuwa ikivurugwa na watu wenye nia mbaya na pia  dunia na mazingira yake yamekuwa yakiharibiwa na watu wenye tamaa na ambao wanaleta maafa kwa jamii nzima."

Katika salamu za Kristmas, Papa Fransis pia aliongezea kwa kueleza ya kuwa nchi kama DRC Kongo, Nigeria, Sudani ya Kusini na Syria zimekuwa na migogoro ambayo imekuwa  inatakiwa iishe haraka " lakini kutokana na kukosa imani kwa wahusika  watu wamekuwa wakipoteza maisha  kila siku kitu ambacho ni kinyume na maadili a kiutu."

Papa Fransis ametimiza miezi tisa sasa tangu kutawazwa rasmi kuwa mkuu wa kanisa katoliki lenye waumini zaidi ya 1.2 billion na amekuwa akipinga vitendo vya kuvuruga amani vinavyo tokea duniani na  amekuwa akiwaagiza viongozi kwa kushirikiana na wananchi  kuhakikisha amani inakuwepo kwa kila mtu na kila jitihada zifanyike ili watu masikini wasaidiwe kuinua maisha yao.

Umoja wa Mataifa kichwa kuuma kwa Sudani ya Kusini.

New York, Marekani - 25/12.2013. Kamati ya usalama ya umoja wa mataifa imekubali kuongeza zaidi ya wanajeshi wake nchi Sudani ya Kusini kufuatia vita vinavyoenedelea katika ya wanajeshi wanao muunga mkono rais  wa sasa wa nchi hiyo Salva Kiir na mpizani wake na ambaye alikuwa makamu wa Riek Machar.

Toby Lanzer akithibitisha uamuzi huo wa UN alisema "Wanajeshi, 12.000 watakuwepo nchi Sudani ya Kusini  na  polisi 1,323 ili kuweza kulinda na kurudisha amani nchini Sudan, kwani wanajeshi na askari UN waliokuwepo hapo mwanzo walionekana kuzidiwa nguvu kutokana na vita vinavyo endelea hadi sasa nchini humo."

Kwa mujibu wa shirika la kimataifa la  kutete haki za binadamu limesema kuwa zaidi ya watu 1000 wamesha poteza maisha yao kutokana na vita hivyo na hadi sasa kuna makaburi yamegunduliwa yamezikwa watu wengi  jambo ambalo huenda likaleta mstuko mkubwa kwa jamii ya kimataifa.

Tangu kuanza vita kati ya wanajeshi wanao muunga mkono makamu wa rais wa Riek Machar na wanajeshi wa serikali ya rais Salva Kiir, maelfu ya Wasudani ya Kusini wamekimbilia katika makazi ya ofisi na maeneo yanayo tumika na umoja wa mataifa nchi humo ili kupata usalama wa masha yao.

Chama cha rais Mohammed Morsi matatani nchini Misri.

Kairo, Misri -25/12/2013. Serikali inayo ungwa mkono  na jeshi nchini Misri imetangaza imetangaza kuwa chama cha washirki na undugu wa Kiislaam ( Muslim Brotherhood)  ni chama cha kigaidi.

Akitangaza uamuzi huo, makamu wa waziri mkuu Hossam Eissa amesema ". chama cha Muslim Brotherhood ni chama cha kigaidi na kuanzia sasa tunakipiga marufuku na mtu yoyote atakaye husika na chama hicho atachukuliwa hatua  na hii  ikiwemo kushiriki katika kukichangia kipesa na kujumika katika maanadamano yatakayo pangwa na chama  hicho"

Chama hicho ambacho ndicho alichokuwa akiongoza rais Mohammed  Morsi aliyetolewa madarakani na jeshi na kushitakiwa kwa makosa  tofauti kinashutumiwa kwa kushiriki katika mashambulizi na kuvuruga amani nchini Misri, jambo ambalo chama hicho kimekanusha kushiriki katika kuchafua amani nchini humo.

Kufuatia kutangazwa kwa Muslim Brotherhood kuwa chama cha kigaidi, jeshi la Misri limepewa nguvu zaidi kutumi ikiwa wanachama cha chama hicho cha Kislaam watavunja sheria hiyo.

Edward Snowdon bado mwiba kwa shirika la ujasusi la Marekani.

Moscow, Urusi - 25/12/2013.Aliyekuwa mfanyakazi wa maswala ya kimtandao katika ofisi za kijasusi za NSA na ambaye alitoa siri za kijasusi za serikali ya Marekani na mshiriki wake  Uingereza hivi karibuni amezidi kupigilia msumari wa moto katika sekta ya ujasusi za washiriki hao.

Edward Snowden raia wa Marekani,  ambaye alikuwa mfanyakazi wa kijasusi katika maswala ya kimtandao na kwa sasa anaishi ukimbizini nchi Urusi amepigilia msumari huo wa moto kwa kusema  vitendo vya serikali kuchunguza watu wake umefikia hali ya kutisha.

"Na hata mtoto ambaye atazaliwa leo atakuwa hakuna kitu chake ambacho akijulikani, kwani serikali kwa kutumi vitu kama runinga, simu na vifaa vingine vya kisayansi ambavyo tunavitumia kila siku katika maisha yetu ndivyo vinatumika katika kuchunguza nyendo zetu za kila siku."

"Napenda kuwakumbusha kuwa kuishi kwa kuchunguzwa na serikali ni kinyume cha sheria, na nijambo ambalo serikali za Marekani na mshiriki wake wamevunja haki zetu za kibinadamu"

Edward Snowden ambaye kwa sasa amefunguliwa kesi nchi Marekani kwa kuiba nyaraka za siri za serikali akiwa kama mfanyakazi wa shirika la kijasusi la NSA nchini Marekani na kuifanya nchi hiyo kuwa na mvutano wa kidiplomasia na washiri wake wakaribu, baada ya  kutoa siri  kuwa Marekani inawachunguza raia na viongozi wa nchi tofauti duniani kinyume cha sheria.

No comments: