Sunday, October 16, 2011

Baraka Obama atuma jeshi kumsaka Joseph Koni.

Malawi ya mpokea rais wa Sudan licha ya kutafutwa na mahakama ya kimataifa. Blantyre, Malawi - 16/10/2011. Rais wa Sudan ambaye anatafutwa na mahakama ya kimataifa inayoshughulikia makosa ya ukikwaji wa haki za binadamu, amewasili nchini Malawi kwa ziara ya kiserikali. Omar Al- Bashir ambaye alishitakiwa katika mahakama ya Uhollanzi, yupo nchini Malawi ili kudumisha uhusiano wa karibu na nchi hiyo. Msemaji wa mahakama ya kutetea haki za binadamu iliyopo nchini Uhollanzi Elise Kepper, alisema "Malawi kamanchi mwanachama wa mahakama hii , ni lazima watimize masharti kwa kumkamata Omar Al Bashi ambaye anatakiwa na mahakama kujibu mashitaka yanayo mkabili." Kesi zidi ya rais, Omar Al Bashir, ilifunguliwa mwaka 2009 na mahakama ya kimataifa ya Hague nchini Uhollanzi kufuatia uchunguzi ulionyesha ya kuwa serikali yake ya Sudani ilihusika katika ukiukwaji wa haki za binadamu katika eneo la Darfur na kutaka akamatwe tayari kufikishwa mahamani ili kujibu mashitaka zidi yake. Baraka Obama atuma jeshi kumsaka Joseph Koni. Kampala, Uganda - 16/10/2011. Rais wa Marekani, Baraka Obama ametuma wanajeshi wapatao 100 ili kusaidiana na jeshi linalo mtamfuta kiongozi wa kundi la Lord's Rasistance Army. Katika barua iliyopatikana ikulu ya Washington ilisema " rais Obama ameruhusu idadi ya wanajeshi wapatao 100, ili kushiriki katika kumsako wa kumsaka Joseph Koni ambaye ni kiongozi wa kundi la LRA." Koni na kundi lake wana pingana na serikali ya Uganda kwa upanda wa kaskazini mwa nchi hiyo na kushutumiwa kuhusika katika vitendo ambavyo vinakihuka haki za binadamu tangu aanzishe vita vya kuipinga serikali tawala ya rais Yoweri Musen kwa miaka 10 sasa. Luis Moreno Ocampo kuchunguza mauaji ya Ivory Coast. Abidjan, Ivory Coast - 16/10/2011. Mkuu wa mashitaka wa mahakama ya kimataifa ya kutetea haki za binadamu iliyopo nchi Uhollanzi amewasili nchini Ivory Coast tayari kwa kuanza uchunguzi zidi ya ukiukwaji wa haki za binadamu wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe. Luis Moreno Ocampo, ameanza kazi hiyo baada ya makahama ya kimataifa kumpa ruhusa kuendelea na uchunguzi ili kujua ukweli kama kulikuwa na ukiukwaji wa haki za binadamu wakati kundi la rais wa sasa Alassane Ouattara lilipo kuwa linapambana na kundi la rais aliyetolewa madarakani kwa nguvu za kijeshi Laurent Gbagbo. Akiongea mara baada ya kuwasili nchini Ivory Coast Luis Moreno Ocampo alisema " katika uchunguzi wetu tuta kutana na makundi yote yaliyo husika katika vita na wale wote walio athirika na vita hivyo ili kupata ukweli zaidi." Kuwasili kwa Moreno Ocampo kumekuja kufuatia ripoti ya shirika la kutete haki za binadamu kuripoti ya kuwa kulikuwa na ukiukwaji wa haki za binadamu wakati wa makundi ya Gbagbo na Ouwattara yalipo kuwa yanapambana baada ya matokeo ya uchaguzi mkuu wa Ivory Coast. Serikali ya Kenya yaamua kupambana kundi la Al Shabaab katika mipaka yake Nairobi, Kenya - 16/10/2011. Jeshi Kenya limeanza msako wa kuwasaka wapiganaji wa kundi la Al Shabaab waliopo mpakani na nchi hiyo. Alfred Mutua ambaye ni msemaji wa serikalialisema," serikali ya Kenya imeamua kufanya hivyo ili kulinda mipaka yake tayari kupambana na kundi la Al Shabaab, kundi ambalo limekuwa likihusika katika utekaji wa nyara wa raia wa kigeni wanao tembelea nchini Kenya, na tunayo haki ya kujilinda na mashambulizi ya aina yoyote na jeshi la Kenya lipo tayari kuwatafuta wale wote waliohusika na ushambulizi na utekaji wa nyara." Matamko ya serikali ya Kenya kupambana na Al Shabaab yamekuja huku kundi hilo likiwa linaendelea kupambana na serikali ya Somalia na kufanya amani kuwa tete nchini Somalia.

No comments: