Thursday, October 20, 2011

Aliyekuwa kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi auwawa.

Aliyekuwa kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi 69 auwawa. Picha hapo chini hapo zinaonyesha enzi ya uhai wa kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi, akiwa kama kiongozi wa Libya na kukutana baadhi ya viongozi tofauti duniani hadi mwisho wa uhai wake ambapo alitawala Libya kwa miaka 41.

Muammar Gaddafi akiongea jijini Tripol ka mara ya mwisho kabla ya jiji la Tripol kuangushwa.
Sura inayo onekana inaaminika ya kuwa sura ya Muammar Gaddafi akiwa amezingirwa.
Mwili wa Muammar Gaddafi ukionekana baada ya kifo chake.
Muammar Gaddafi akiaga katika mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa.
Muammar Gaddafi akiongea wakati wa mkutano wa umoja wa Mataifa.
Muammar Gaddafi akiwa na baadhi ya viongozi wa jumuia ya nchi za Kiarabu.
Muammar Gaddafi akiwa na viongozi tofauti wa dunia.
Muammar Gaddafi akiwa akisalimiana na rais wa Marekani Baraka Obama.
Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza akiwa na Muammar Gaddafi enzi za uhai wake.
Rais wa Ufaransa, Nicolas Sarkozy akisalimiana na Muammar Gaddafi alipo tembelea Ufaransa.
Muammar Gaddafi akisalimiana na Vladimir Putin.
Enzi za uhai wake Muammar Gaddafi alikuwa mgeni wa heshima katika nchi tofauti duniani.
Muammar Gaddafi na waziri Mkuu wa Itali wakiwa wameshikilia bunduki wakati walipo kutana.
Gordon Brown wakati akiwa waziri mkuu wa Uingereza alikutana na Muammar Gaddafi pia.
Nelson Rolihlahla Mandela - Madiba alikuwa rafiki mkubwa wa Muammar Gaddafi.
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Condoleeza Rice alitembelea nchi Libya ili kuimarisha ushirikiano na serikali ya Muammar Gaddafi.
Muammar Gaddafi akiwa na rais wa Venezuela Hugo Chavez.
Muammar Gaddafi akiwa na Robert Mugabe, viongozi ambao wamekuwa shubiri kwa nchi za Magharibi.
Muammar Gaddafi alikutana na rais wa Syria Bassad al Assad.
Rais wa Palestina Mahamoud Abbas akikabilishwa na Muammar Gaddafi.
Hayati kiongozi wa Palestina Yasir Arafat alikuwa mshiriki mkuu wa hayati kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi.
Muammar Gaddafi siku alipo tangaza rasmi kuwa kiongozi wa Libya baada ya kuung'oa utawala wa kifalme wa Idris.
Tripol, Libya - 20/10/2011. Kiongozi na rais Muammar Gaddafi wa Libya aliyetolewa madakani kwa nguvu za kijeshi ameuwawa baada ya kukimbia na kukaa mafichoni kwa muda mrefu tangu kuanza kwa vita nchini humo.
Waziri Mkuu wa muda wa serikali ya Libya Mahmoud Jibril alisema " Muammar Gaddafi ameuwawa na ni furaha kwa Walibya wote, kwani tulikuwa tunaingojea siku hii kwa hamu."
Rais wa Marekani Baraka Obama alisema " uhuu ni muda wa Walibya baada ya kuangushwa kwa Muammari Gaddafi na tutakuwa pamoja na Walibya katika kuijenga nchi yao."
Waziri Mkuu wa Uingereza ambaye aliongoza katika kampeni ya kumg'oa Muammar Gaddafi alisema " ni siku ya kukumbukwa na wale wote waliopata kuteswa na waliouwawa Kanali Gaddafi."
Naye Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema " ni historia ya kukumbukwa na kuonya ya kuwa Walibya watakuwa na wakati mgumu katika kujenga nchi yao."
Kwa mujibu wa habari zilizo patikana zinasema ya kuwa Muammar Gaddafi, aliuwawa katika mashambulizi kwenye eneo alilo kuwa ameweka makao yake baada ya kukimbia jijini Tripol kutokana na kuzisiwa nguvu na jeshi la serikali ya mpito kwa masaada wa jeshi la NATO.

No comments: