Sunday, October 9, 2011

Wanachi wa Kenya wamuaga mama Wangari Maathai kwa mara ya mwisho.

Wananchi wa Kenya wamuaga mama Wangari Maathai kwa mara ya mwisho.





Nairobi, Kenya - 09/10/2011. Maelfu ya wanchi wa Kenya wakiongozwa rais Mwai Kibaki na waziri mkuu Raila Odinga wameungana pamoja katika bustani ya uhuru ili kumwaga mama Wangari Maathai 71, kwa mara ya mwisho, kabla ya kufanywa mazishi ya uchomwaji kama alivyo agiza.
Rais Mwai Kibaki alisema " Wangari Maathai alijitolea katika kujenga taifa na njia bora ya kumbumbuka ni kuendeleza kazi ailiyokuwa anaifanya."
Wangari Maathai alikuwa mwanamke mwafrika wa kwaza kuzawadiwa tunzo ya Nobel kutokana na juhudi zake za kujenga mazingira kupitia kitengo alicho anzisha kijulikanacho the Green belt Movement.

No comments: