Tuesday, October 25, 2011

Mazishi ya Muammar Gaddafi yafanyika jangwani kisili.

Jiji la Nairobi la kubwa na mlipuko wa bomu kwa mara ya pili.

Nairobi, Kenya -25/10/2011. Mlipuko mwingine wa bomu umelipuka katikati ya jiji la Nairobi siku moja baada ya bomu kulipuka ndani ya ukumbi wa starehe.
Mlipuko huo ambao umetokea kwenye kituo cha basi umesababisha watu 12 kuumia na kuleta wasiwasi mkubwa ndani ya jiji la Nairobi
Mkuu wa Polisi Matthew Iteere alisema " Polisi bado wanafanya uchunguzi na kwani mpaka sasa hakuna ushaidi ya kuwa mashambulizi hayo ni ya kundi la Al-Shabab."
Jiji la Nairobi limepata mlipuko wa pili, baada ya ofisi za kibalozi za Kimarekani kutoa onyo kwa rais wake juu ya usalama katika jiji la Nairobia.
Wakati huo huo serikali ya Kenya itashirikiana na serikali ya Ufaransa katika kupambana na kundi la Al-Shabab.
Msemaji wa jeshi la Ufaransa Kanal Thiery Burkhard alisema " tutaoa misaada ya vifaa vya kivita na ndege zetu zitasaidia kuwasafirisha wanajeshi wa Kenya kwenye mpaka na Somalia."
Hata hivyo Kanal Thiery Burkhard alikanusha kauli ya jeshi la Kenya ya kuwa ndege za jeshi la Ufaransa zilifanya mashabulizi nchini Somalia.
Serikali za Izrael na Misri kubadilishana wafungwa.
Tel Aviv, Izrael - 25/10/2011. Serikali ya Izrael na Misri zimekubaliana kubadilishana wafungwa.
Habari kutoka ofisi ya waziri mkuu zimesema " Izreal itawaachia Wamisri 25 ambao ilikuwa inawashikilia nayo serikali ya Misri itamwachia Muizrael ambaye inamshikilia."
Muizrael Ilan Grapel ambaye anashikiliwa nchini Misri anashutumiwa kwa kuwa mpelelezi, na alikamatwa mapema mwaka huu June 12.
Hata hivyo serikali ya Izrael ilikanusha madai yakuwa Ilan Grapel mwenye uraia wa nchi mbili Izrael na Marekani ni mpelezi.
Kubadilishana wafungwa na Misri kumekuja siku chache baada ya serikali ya Izrael kukubali kunadilisha wafungwa na Hamas, kitendo ambacho kilipelekea kuachiwa kwa askari wa Izrael Girad Shalit ambeye alikuwa anashikiliwa na kundi la Hamas.
Mazishi ya Muammar Gaddafi yafanyika jangwani kisili.
Sirte, Libya - 25/10/2011. Aliyekuwa kiongozi na rais wa Libya Muammar Gaddafi ambaye alitolewa madarakani na baadaye kuuwawa amezikwa kwenye jangwa kisili siku chache baada ya kifo chake.
Serikali ya mpito ya Libya imesema " tumeamua kumzika kisili ili kuepuka watu kufanya kaburi lake kama sehemu ya kishujaa au kumbukumbu."
"Vilevile alifanyiwa maombi na kiongozi wa kidini yeye pamoja na mwanaye pamoja na aliyekuwa msaidizi wake."
Mazishi ya Muammar Gaddafi, mwanae na msadizi wake yalifanyika mapema alfajiri 05:00 sehemu ambayo haitakuwa raisi kwa watu kupafahamu na wale wote waliohusika katika mazishi walikula kiapo ya kuwa awatatoa siri ya kuonyesha alipo zikwa kiongozi huo aliye tawala Libya kwa miaka zaidi ya 40.

No comments: