Tuesday, October 11, 2011

Hamas na Izrael wakubaliana kuachiwa wafungwa.

Hamas na Izrael wakubalia kuachiwa wafungwa.

Gaza, Palestina - 11/11/2011. Kiongozi wa kundi la Hamas ametangaza ya kuwa Wapalestina waliofungwa katika jela za Izrael wataachiwa kwa kubadilishana na askari wa Izrael aliye kamatwa mwaka 2006.
Khaled Meshaal alisema " Wapalestina wapatao 1,000 wataachiwa na askari wa Izrael Gilad Shalit ataachiwa huru, ikiwa ni moja ya msharti yaliyofikiwa kwa pamoja na serikali ya Izrael na Hamas."
"Na haya ni moja ya mafanikio ya kujivunia kwani kati ya watu watakao achiwa ni pamoja na wale waliohukumiwa vifungo vya maisha na waliokaa jela za Izrael kwa muda mrefu." alisema kiongozi huyo wa Hamas,
Waziri mkuu wa Izrael Binyamin Netanyahu aliwashukuru watu wote walioshiriki katika mikutano hiyo kwa kupitia mtando wa twiiti kwa jitihada zao katika mpango wa kuachiwa Gilad Shalit.
Habari zilizo patikana zinasema, jitihada hizo zilifanywa na nchi za Syria, Katar, Ujerumani na Misri nchi wenyeji wa vikao vyote.
Siku za nyuma Izrael na Hamas wamekuwa wakibishana katika jitihada za kubadilishana wafungwa na kuachiwa huru kwa Gilad Shalit.
Walaiberia wafanya uchaguzi mkuu wa urais.
Monrovia, Liberia 11/10/2011. Maelfu ya Walaiberia wamepiga kura ili kumchagua rais atakaye waaaongoza kipindi kingine cha miaka mitano.
Rais aliyekuwa anaongoza kwa kipindi cha miaka mitano iliyo pita, na mshindi wa zawazi ya Nobel ya mwaka 2011, Bi Ellen Johnson Sirleaf alipiga kura katika jimbo lake, huku wapinzani wake wakuu Winston Tubman na mchezaji bora wa mpira wa miguu George Weah kwa pamoja wakiungana katika jitihada za kutaka kushinda kura ili kuiongoza Liberia.
Baada ya kumaliza kupiga kura yake Ellen Johnson Sirleaf alisema " nitakubaliana na matakwa ya Wanchi wa Liberia kama nikikosa kuchaguliwa kuwaongoza tena."
Liberia nchi ambayo ilikumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe kwa muda mrefu na ambavyo vilimalizika mwaka 2003, na kufanya uchaguzi wa kwanza mwaka 2005, ambapo rais aliye maliza muda wake Bi Ellen Johnson Sirleaf alichaguliwa kuwa rais wa nchi hiyo na kuwa rais wa kwanza mwanamke katika bara la Afrika.
Kipindupindu bado tishio barani Afrika.
Geneva, Uswis - 11/01/2011. Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia maswala ya watoto UNICEF rimeripoti ya kuwa watoto zaid ya 2,000 walipoteza maisha na wengine 85,000 kudhulika na ugonjwa wa kipindupindu tangu mwazo mwa mwaka huu 2011 hadi sasa.
Msemaji wa UNICEF Maxime Mercado alisema " Wananchi Waishio Kusini mwa jangwa la Sahara wameathiriwa kwa kiasi kikubwa na ugonjwa wa kipindupindu, hivyo ipo haja ya mbinu mbadala kufanyika ili kuutokomeza ugonjwa huo."
"Nchi za Kameroon, Chad, Jamuhuri ya Kongo, Ghana, na Nigeria zimeathiriwa kwa kiasi cha asilimia 90 kulinganisha na nchi nyingine ishirini ambazo zilikubwa na ugonjwa huo katika bara la Afrika." alimalizia msemaji wa UNICEF
Uginjwa wa kipindupindu unasabalishwa wadudu wajulikanao kama vibrio ambapo wadudu hawa hupenda kukaa kwenye maji na vyakula vichafu tayari kumdhuru binadamu atakaye kunywa au kula chakula chenye wadudu hao.
Dalili za ugonjwa wa kipindupindu ni kutapika na kuharisha kwa mfurulizo hadi kuishiwa nguvu.

No comments: