Wednesday, October 19, 2011

Misaada kwa nchi za Afrika kusimamishwa miaka michache ijayo.

Vladimir Putin ahaidi kuimarisha uchumi wa Urusi kimataifa.

Moscow, Urusi - 19/10/2011. Waziri mkuu wa Urusi na ambaye anatarajiwa kugombea kiti cha urais chini humo amewahakikishiwa wanachi ya kuwa akichaguliwa atakuwa na jumukumu la kuinua uchumi.
Vladimir Putin alisema "kazi itakayo pewa kipao mbele ni ya kuinua uchumi wa Urusi kimataifa, kuimarisha misingi ya kisiasa na demokrasi."
" Sikufikilia swala la urais, lakini nilipo pendekezwa kuchukua majukumu haya ndipo nilipo jua nina wajibu mkubwa wa kuiinua Urusi kiuchumi na kuifanya kuwa nchi imara, pindipo nitakapo chaguliwa."
Waziri mkuu Vladimir Putin, alipendekezwa kugombea kiti cha urais katika mkutano mkuu wa chama tawala uliyo fanyika hivi karibuni jijini Moscow na kutangazwa rasmi na rais wa sasa Dmtri Medvedev.
Misaada kwa nchi za Afrika kusimamishwa miaka michache ijayo.
London, Uingereza - 19/10/2011. Misaada kwa nchi za Afrika itaanza kufutwa miaka michache ijayo ili nchi hizi ziweze kujitegemea kwa kila kitu katika kuinua uchumi na maendeleo ya wananchi wao.
Waziri mkuu wa zamani wa Uingereza Tony Blair aliyasema hayo katika mkutano ya kuwa " kusimamisha misaada hiyo ni nia ya baadaye ili kuzipa nafasi nchi hizo kujijenga kwa kutumia maliasili zao, kwani bila hatua kuchukuliwa nchi hizi hazitapata mwamko wa kujitegemea."
"Vilevie bara la Afrika kwa sasa lina watu wenye uwezo wa kuongoza na kujenga nchi zao kiuchumi kisiasa na kijamii kutokana na kodi na mapato yatakayo patikana katika nchi hizo."
Tony Blair aliyasema hayo wakati alipo kuwa akihutubia mkutano ulio andaliwa na shirika linalo shughulikia utoaji wa misaada kwa nchi za dunia ya tatu.

No comments: