Friday, October 21, 2011

Kifo cha Muammar Gaddafi kuchunguzwa na mazishi ya lipangwa kufanyika kisiri.

Kifo cha Muammar Gaddafi kuchunguzwa na mazishi yalipangwa kufanyika kisiri.

Tripol, Libya - 21/10/2011. Uongozi wa serikali ya mpito ya Libya (NTC) ,umesimamisha mazishi ya aliyekuwa rais na kiongozi wa nchi hiyo Muammar Gaddafi, baada ya shirika la kutetea haki za binadamu kutaka uchunguzi ufanywe juu ya kifo cha kiongozi huyo.
Uamuzi wa kutaka uchunguzi ufanyike umekuja baada ya video na picha zilizo onyeshwa kwenye mitandao ya kuwa Muammar gaddafi alikamatwa akiwa mzima, lakini baadaye alionekana amekufa, jambo ambalo linaleta utata katika kifo chake.
Rupert Colville msemaji wa shirika la kutetea haki za binadamu alisema " inasikitisha na ukiangalia kwa ujumla matukio yenyewe kwani yamekwenda kinyume na sheria za haki za binadamu."
Serikali ya mpito ya Libya (NTC) imekubali uchunguzi ufanyike kuhusu kifo cha Muammar Gaddafi, baada ya hapo mwanzo kusema ya kuwa aliuwawa wakati wa mapambano.
Hata hivyo habari kutoka ndani ya serikali ya mpito ya Libya (NTC) zinasema " mazishi ya Muammar Gaddafi yalikuwa yamepangwa kufanyika kwa siri, na inaaminika ya kuwa kulikuwa na mpango wa kumzika baharini, ili kuepusha watu wasifanye kaburi lake kama sehemu ya kumbukumbu na kuabudiwa hapo baadaye jambo ambalo limekuwa likipingwa na baadhi ya viongozi ndani ya (NTC)."
Mwili wa Muammar Gaddafi umehifadhiwa katika mji wa Misrata tayari kwa mazishi.
Mapambano yazidi kati Al-Shabaab na jeshi la Muungano wa Afrika.
Mogadishu, Somalia - 21/10/2011. Uongozi wa Muungano wa Afrika umekanusha ya kuwa miili iliyo kuwa inaburutwa na kundi la Al-shabaab ni ya wanajeshi wanao linda amani nchini Somalia.
Habari za kukanusha tukio hilo limekuja baada ya kundi la Al-Shabaab kudai " yakuwa miili ya watu waliyokuwa wakiburuza ilikuwa ni ya askari wa Umoja wa Afrika ambao waliwauwawa wakati wa mashabulizi kati yao."
Hata hivyo, Muungano wa Afrika umesema " wanajeshi wake kumi wameuwawa na baadhi kujeruhiwa wakati wa mapambano na kundi la Al-Shabaab."
Nchi ya Somalia imekuwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe tangu kuangushwa kwa aliyekuwa rais wa nchi hiyo Muahamad Siad Barre
Kundi la ETA la Uispania latangaza kusimamisha mashambulizi.
Madrid, Uispania - 21/10/2011. Kundi lilinalo pingana na serikali ya Uispania la ETA limetangaza kusimamisha mashambulizi na kuweka siraha chini.
ETA kundi ambalo limekuwa likilaumiwa kwa kuhusika milipuko ya mabomu na mauji iliyokuwa ikitokea tangu kundi hilo lianza upinzani zidi ya serikali, lili tangaza rasmi ya kuwa linaweka siraha chini na kusimamisha vitendo vyote vya mashambulizi.
Kundi hili ambalo lilikuwa linapigania kujitenga kutoka serikali kuu ya Uispania na kuwa nakutaka kujulikana kana eneo huru la Baskeu (Basque).
Waziri mkuu wa Uispania Jose Luis Rodriguez Zapatero alisema " hii ni furaha kwa wananchi wa
Uispania na nimwanzo wa ushindi katika kukuza demokrasi nchini Uispania."
Suruhisho la amani la Uispania limekuja kutokana na juhudi za kimataifa zikiongozwa na aliye kuwa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan na aliyekuwa kiongozi wa chama Sinn Fein cha Ireland ya Kaskazini Gerry Adams.
Wabunge wa chama cha David Cameron wataka kura ya maoni juu Uingereza na Muungano wa nchi za Ulaya.
London, Uingereza - 21/10/2011. Wabunge wa chama cha Konzevativi cha Uingereza amba cho kinatawala kwa katika serikali ya shirikiasho wametishia kujitoa ikiwa waziri mkuu hatabadilisha msimamo wake katika swala juu ya jumuyia ya muungano wa Ulaya.
David Cameron, amekuwa na wakatio mgumo, baada ya wabunge wapatao 70 kutaka bunge kupiga kura ya maoni kuhusu kushiriki kwa Uingereza katika jumuiya ya nchi za Ulaya.
Habari kutoka ofisi ya waziri mkuu numba 10 Westminster jijini London zinasema "wabunge kutoka chama cha Konzevativi wamelazimishwa kwa mujibu wa sheria kupiga kupinga muswada kuhusu Uingereza katika kushiriki kwake kwenye jumuiya ya Ulaya."
Swala la kutaka kupigwa kura kuhusu ushiriki wa Uingereza katika jumuiya ya Ulaya umekuja kutokana na msukumo wa baadhi ya viongozi kudai ya kuwa jumuiya ya Ulaya imekuwa ikilazimisha baadhi ya sheria kutekelezwa nchi Uingereza, jambo ambalo wanahisi kama jumuia hiyo inamadaraka makubwa na kuhatarisha uwezo wakujiamualia mambo kwa Waingereza.

No comments: