Sunday, October 9, 2011

Wapalestina wamlaumu Yony Blair.

Dolla Million 10 zatolewa kwa kichwa cha kiongozi wa Al Qaeda

Washington, Marekani - 09/10/2011. Serikali ya Marekani imetangaza zawadi ya dolla za Kimarekani Million 10, kwa mtu atakaye toa habari za mahali alipoa Ibrahim"Awwad Ibrahim" Ali al Badri ama maarufu kwa jina Abuu Dua.
Zawadi hiyo ya donge nono imetolewa ili kuwezesha kukamatwa kwa Abuu Dua, ambaye ni kiongozi wa kundi la Al Qaeda nchini Irak.
Abuu Dua ambaye alitangaza ya kuwa atalipa kisasi kutokana na kitendo cha jeshi la Marekani kumwua aliyekuwa kiongozi wa kundi la Al Qaeda Osama bin Laden.
Kundi la Abuu Dua limedai kuuhusika na mauaji yaliyo tokea hivi karibu nchini Irak katika mji wa Masul.
Wapalestina wamlaumu Tony Blair.
Brussels, Ubeligiji - 09/10/2011.Viongozi wasimamizi wa maswala ya Wapalestina na Waizrael wamekutana ili kujadili mbinu ya kuzishawishi pande hizo kurudi kwenye meza ya mazungumzo.
Viongozi hao kutoka Marekani, Umoja wa Ulaya na Urusi walikubaliana kwa pamoja kufanya kila jitihada ili Wapalestina na Waizrael warudi katika mazungumzo tayari kwa kumaliza mgogoro uliyopo kati ya pande hizo mbili na kuleta amani ya kudumu.
Catherine Ashton ambaye ni mkuu wa maswala ya kigeni ya umoja wa Ulaya alisema " uongozi wa kamati ya kusimamia kutatua matatizo kati ya Wapalestina na Waizrael, watawaalika viongozi viongozi wa pande zote mbili ili kuanza mazunguzo."
Hata hivyo uongozi wa Wapalestina umesema "hautarudi kwenye mazungu hadi hapo serikali ya Izrael itakapo simamisha ujenzi wake katika maeneo iliyo yachukua kwanguvu na kukubali kufuatia makubaliano ya mipaka ya mwaka 1967."
Nayo serikali ya Izrael imesema " haina haja ya kuwekwa masharti ili kuanza mazungumzo kama inavyo daiwa na Wapalestina."
Mohamed Shtayyeh ambaye in mmoja wa viongozi wa ngazi ya juu katika serikali ya Wapalestina ametamka kwa kusema " inabidi Tony Blair ajiudhulu wadhifa wake kwani anaonekana kutokuwa na mwelekeo wa usawa,kwa kupinga maombi ya Wapalestina kutambulika na umoja wa mataifa kuwa kama taifa."
"Amekuwa akutumia wadhifa wake kuzishawishi nchi za Ulaya kupinga maombi ya Wapalestina, hivyo nasikitika inabidi ajitoe." aliongezea Shtayyeh.

No comments: