Friday, October 7, 2011

Tunu ya tunzo la amani yazawadiwa kwa wanawake watatu kwa pamoja.

Tunu ya tunzo la amani yazawadiwa kwa wanawake watatu kwa pamoja.

Oslo, Norway - 07/10/2011. Kamati inayo simamia na kuchagua watu wa kutunukiwa zawadi ya amani duniani, ya Nobel wamewachagua wanawake watatu kwa pamoja kama washindi wa tuzo hiyo.
Wanawake waliotunukiwa ni rais wa Liberia ellen Johnson Sirleaf, Bi,Tawakul Karmal wa Yemen na mwanaharakati wa kutetea amani nchini Liberia Bi Leyhmah Gnowee.
Mwenyekiti wa kamati ya kutoa tunzo ya Nobel Thorbjorn Jagland alisema " kupewa tunzo kwa wanawake hawa ni ishara yakuwa amani ya dunia itafanikiwa ikiwa tutapata wanawake wenye moyo kama hawa dunia nzima ambao watashiriki katika kuleta maendeleo kwenye nyanja zote kijamii na kiuchumi."
" Hii ni ishara kubwa ya mkuwa ukandamizwaji wa wanawake lazima ukomeshwe, kwani wanauwezo sawa kama wanaume."
Uamuzi huo wakuwatunukia wanawake hao, umekuja kutokana na jitihada walizo zionyesha katika nafasi zao bila kutumia vurugu au kusababisha kuvurugika kwa amani.
Bi Ellen Johnson, amepewa tunzo hiyo kwa kuwa rais wa kwanza mwanamke katika bara la Afrikana Bi Tawakul Karman kuwa mmoja wa kiongozi katika kuleta demokrasi chini Yemen.
Uamuzi wa kusimasha mashambulizi Libya upo chini ya wakuu wa Jeshi wa NATO
Washington, Marekani - 07/10/2011. Serikali ya Marekani inaamini ya kuwa NATO imekamilisha kazi yake nchini Libya, na maamuzi ya jeshi la anga bado yanaangaliwa kwa makini kutegemea hali halisi.
Waziri wa ulinzi wa Leon Panetta alisema " swala zima la Libya litategemea hali ya usalama wa raia na kung'olewa kwa Muamar Gaddafi, vilevile kama serikali ya mpito inaweza leta usalama nchini humo."
"Uamuzi upo chini ya wakuu wa jeshi."
Tathmini hiyo ya hali ya Libya imetolewa wakati waziri wa ulinzi wa Marekani amefanya mazungumzo na viongozi washiriki wake NATO.
Tumeshindwa kuleta usalama na amani nchini Afghanistan asema rais Hamid Karzai.
Kabul, Afghanistan -07/10/2011. Rais wa Afghanistan amekubali yakuwa jeshi la US, NATO na waserikali yake wameshindwa kudumisha usalama na amani nchi Afghanistan japo ni miaka 10 imepita.
Rais Hamid Karzai alisema, " matatizo yanaanzia nchini Pakistani, wengi ya wapiganaji wa Talibani wanatokea Pakistani na serikali ya nchi Pakistani hajatilia mkazo katika kupambana na Talibani."
"US, NATO na majirani zetu Pakistan kwa kushirikiana walitakiwa toka mwanzo kung'oa mizizi ya Talibani, lakini hakukua na ushirikiano katika jambo hili."
Vilevile rais Hamid Karzai alihaidi kuachia madaraka ifikapo mwaka 2014 naameanza kuandaa njia kwa yoyote atakaye kuja badala yake.
Vita vya Afghanistan vimetimiza miaka 10 siku ya leo tangu kuanza ambapo jeshi la Marakani NATO na washirika wake walipo anzisha mashabulizi zidi ya Taliban kwaka 7/10/2001.

No comments: