Thursday, October 6, 2011

Mwanzilishi wa kampuni ya Apple afariki dunia.

Mwanzilishi wa kampuni ya Apple afariki dunia.

Califonia, Marekani - 06/10/2011. Aliyekuwa mwanzilishi na mkurugenzi mkuu wa kampuni ya mtandao wa Apple amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Stev Jobs 56, ambeye ugunduzi wake wa mtandao wa simu za aina ya Apple, alifariki dunia baada ya kuungua kwa muda mrefu ugonjwa wa saratani kongosho karibu na mapafu. Kufuatia kifo chake viongozi na wanchi mbalimbali wametoa salamu zao za rambirambi kwa familia na wafanyakazi wa Apple kwa msiba uliyo wakuta.
Bill Gate alisema " Dunia imepoteza mtu ambaye ameleta mabadiliko makubwa na mabadiliko hayo yata gusa vuzazi vijavyo, na tutamkumbuka kila siku ya maisha yetu." Steve Jobs ambaye atakumbukwa milele kwa kuleta mabadiliko makubwa katika mitandao ya simu za Apple aliachia madaraka ya kuwa mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Apple mwishoni mwa mwezi wa Augustus mwaka huu, ilikupata muda wa mapumziko.
Bendera zimewekwa nusu mringoti katika ofisi zote za Apple huku watu wakikusanyika kuweka maua na kadi chini ya bendera zenye picha ya Steve Jobs, kwa kumtakia mapumziko mema milele.
Mahakama ya Hague kuchunguza vita vya Ivory Coast.
Hague, Uhollanzi - 06/10/2011.Mahakama ya kimataifa inayoshughulikia kezi zidi ya ukiukwaji wa haki za binadamu imepewa ruhusa kuchunguza kama kulikuwa na ukiukwaji wa haki za binadamu nchini Ivory Coast wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Mahakama hiyo iliyopo Hague nchini Uhollanzi ilitoa ruhusa kwa mwanasheria mkuu wa mahakama hiyo kuanza kuchunguza mwenendo mzima wa vita vilivyo tokea nchini Ivory Coast wakati makundi mawili yaliyo kuwa yakiongozwa na rais wa sasa wa nchi hiyo Alassane Ouattara na yale ya aliyekuwa rais aliyetolewa kwa kwanguvu za kijeshi Laurent Gbagbo.
Mwanasheria huyo Moreno Ocampo anatarajiwa kuchunguza mauaji yaliyo tokea ambapo inasadikiwa zaidi ya watu 3000 walipoteza maisha yao na wengi kujeruhiwa wakati wa mapambano ya makundi hayo.
Nayo mashirika ya kutete haki za binadamu yalitoa ripoti kwa kualaumu pande zote mbili kwa kuhusika na ukiukwaji wa haki za binadamu wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchi Ivory Coast.
Kanali Muamar Gaddafi aongea akiwa mafichoni.
Sirte, Libya - 06/10/2011. Rais aliyetolewa madarakani nchini Libya amewahimiza wananchi kuandamana katika mitaa yote ya nchini Libya kwa madai, Libya imeharibiwa na wasaliti kwa msaada wa majeshi ya wavamizi.
Muamar Gaddafi alisema " hali ya Libya imekuwa na halimbaya na kila kitu kimeharibiwa, hivyo ni wakati wa wanchi wa Libya kusimama na kupinga uharibifu unaofanywa na wasaliti na majeshi ya uvamizi huku, mkinyanyua bendera ya kijani kwani hii ni haki yenu na nchi ni yenu."
"Na hawa wanao jiita viongozi wa serikali ya mpito wamechaguliwa na nani?" Aliuliza Muamar Gaddafi.
Rais huyo wa Libya ambaye hajulikani yupo wapi hadi sasa, ujumbe wake ulitangazwa kwa kupitia moja ya mtandao wa habari uliopo nchini Syria.

No comments: