Monday, October 10, 2011

Rais mstaafu wa Cape Verde atunzwa zawadi ya Mo Ibrahim,

Rais mstaafu wa Cape Verde atunzwa zawadi ya Mo Ibrahim.

Praia, Cape Verde - 10/10/2011. Aliyekuwa rais wa Cape Verde amechaguliwa na kama mshindi wa zawadi ya Mo Ibrahim na kuzawadia kiasai cha dola za Kimarekani Million 5.
Mstaafu rais Pedro Verona Pires amepewa zawadi hiyo kwa kuwa mtastari wambele katika kujenga nchi yake kiuchumi, kidemokrasia na kulete amani.
Kufuatiwa kutunukiwa zawadi hiyo rais mstaafu Pedro Veroana Pires alisema " nitaziwekeza pesa hizo kwenye mradi wa kuandika kitabu kuhusu historia ya Cape Verde hadi uhuru, na sina mawazo ya kuwekeza katika biashara au kitu kinacho fanana na ubiashara."
Rais mstaafu Pedro Verona Pires alikuwa mmoja ya viongozi waliopigana katika kuung'oa utawala wa Kireno kisiwani humo hadi uhuru mwaka 1975.
Habari za kuchaguliwa kwake rais mstaafu Verona Pires, zilimkuta akiwa anafanya mazoezi ya viungo.
Askofu mkuu wa kanisa la Anglikani akutana na rais Robert Mugabe.
Harare, Zimbabwe - 10/10/2011. Askofu mkuu wa kanisa la Anglikani wa Uingereza amekutana na rais wa Zimbabwe Robert Mgabe kwa mazungumzo, baada ya hotuba yake ya kuishutumu serikali ya Zimbabwe kwa kuwakandamiza baadhi ya waumini wa madhehebu ya Kianglikani.
Askafu Rowan Williams alikutana na rais Robert Mugabe kwa na kujadili hali halisi ya kidini nchini humo hasa kutokana na malalamiko kutoka kwa baadhi ya waumini wa kanisa la Aglikani wanao dai ya kuwa wananyanyaswa kutokana na uumini wao.
Akiongea Askofu Rowans Williams alisema "nimemwomba rais Mugabe atumie uwezo wake kuzuia uonevu na unyanya swaji kwa waumini wa madhehebu mengine na nimemkabidhi faili la maonevu yote yaliyo tokea na naamini atayachughulikia."
Hata hivyo habari kutoka ndani ya mkutano huo, zinasema "rais Robert Mugabe hakuwa na habari yoyote yakuwa hali hii na alimkumbusha historia ya kanisa la Aglikani ya kuwa limetokana na kanisa la katoliki."
Mkutano wa rais wa Zimbabwe na Askofu mkuu wa kanisa la Anglikani umefanyika ilikutatua matatizo yaliopo kimadhehebu nchini Zimbabwe.
Wakristu wa Kikoptik na Waislaam wenye siasa kali wapambana nchini Misri.
Kairo - Misri - 10/10/2011. Maelfu ya umini wa Kikristu wa madhehebu ya kanisa la Koptik wameilalamikia serikali ya Misri kwa kitendo cha kuwapuuza na kutowalinda waumini wa dhehebu hilo.
Malalamiko hayo yalitolewa wakati wa mazishi ya waumini wenzao ambao waliuwawa wakati wa ghasia zilizo tokea hivi karibuni.
Kiongozi mkuu wa kanisa hilo Shedua III amelaumu ghasia hizo na kuwataka waumini wa dhehebu hilo wafunge kwa muda wa siku tatu, huku wakifanya maombi ya kuwepo na amani nchini humo kwani "chuki zimekuwa waziwazi kati ya jamii ya Wamisri na kusababisha maisha ya watu zaidi ya 24 kupotes na wengine kujeruhiwa."
"Ukristu unakataa machafuko na ugomvi". Alisema mkuu huyo wa kanisa la Koptic."
Kufuatia tukio hilo, uongozi wa serikali ya Misri imeitisha mkutano wa dharula ili kujadili ni mbinu gani watafanya kuzua fujo kama hizo zi sitokee tena,

No comments: