Tuesday, October 4, 2011

Askofu Desmond Tutu aishambulia serikali ya Afrika ya Kusini.

Askofu Desmond Tutu aishambulia serikali ya Afrika ya Kusini.

Cape Town- Afrika ya Kusini - 04/10/2011. Askofu mstaafu wa kanisa la Anglikani la Afrika ya Kusini Desmond Tutu ameishabulia na kulaani kitendo cha serikali ya Afrika ya Kusini kuchelewecha kumpa visa kiongozi wa Watibeti Dalai Lama.
Akiongea na waandishi wa habari Askofu Tutu alisema " siamini kama yaha yanaweza tokea hapa nchini kwetu, serikali ANC imekuwa ya kibaguzi (Apartheid) inatia aibu, na nitaombea ianguke, kwani kuwa na watu wengi wanao uunga mmkono siyo sababu ya kutokuanguka."
Kufuatia ucheleweshaji wa viza, Dalai Lama ameamua kufuta safari yake ya kwenda Afrika ya Kusini ambapo alitarajiwa kusherekea miaka 80 ya kuzaliwa kwa Askofu Desmond Tutu na kupewa tuzo ya amani ya Mahatma Gandhi.
Hata hivyo habari kutoka serikali ya Afrika ya Kusini zinasema " hatukumyima viza Dalai Lama, bali tunafuata utaratibu wa kutoa viza kisheria."
Wakati huohuo uongozi wa serikali ya Afrika ya Kusini umedai kufuatialia kwa ukaribu yote yaliyoongelewa na Askofu Tutu.
Waandamanaji maeneo jengo la hisa la Wall Street.
New York, Marekani - 04/10/2011. Mamia ya waandamanaji wamekusa nyika karibu na jengo kuu ambamo biashara za hisa huwa zinafanywa, kwa kudai myumbo wa uchumi unasababishwa na biashara hizo.
Jengo hilo maaraufu kwa jina Wall Street, lilivamiwa huku waaandamanaji wakiwa na na mabango yanayo laani biashara hiyo.
Mmoja wa waandamanaji hao alisema " wanaiba mabilioni, wanatumia pesa zetu za kodi kwa kulipia hasara zilizo letwa na babenki ya hisa, hivyo umefika wakati wa wananchi kudai haki zao."
Kufuatia maandamano hayo watu wapatao 700 walikamatwa na polisi kwa kuzuia barabara katika daraja la Brookln na maeneo mengine.

No comments: