Tuesday, October 18, 2011

Shirika la Afya la Dunia kumpambana na malaria kwa hali na mali.

Waizrael na Wapalestina wabadilishana wafungwa.

Tel Aviv, Izrael - 18/10/2011. Wanchi wa Izrael wameshangilia kwa hari na raha baada ya askari aliyekuwa amekamatwa na kundi la Hamas kuachiwa huru.
Gilad Shalit, ambaye alikamatwa na kundi la Hamas mwaka 2006, ameachiwa baada ya kufikiwa makubaliano kati ya serikali ya Izrael na kundi la Hamas katika kubadilishana wafungwa.
Baada ya kuachiwa Gilad Shalit alisema " nilijua ipo siku nitaachiwa ingawa sikujua itakuwa lini, na tumaini yakuwa huu utakuwa mwazo wa kuleta amani kati ya Waizrael na Wapalestina."
Kuachiwa kwa Gilad Shalit, kumetokea wakati huo huo serikali ya Izrael imewachia zaidi ya Wapalestina 477 ambao ilikuwa inawashikilia na wengine zaidi ya 600 wataachiwa hapo baadaye kutokana na makubaliano yaliyowe kwa kati ya serikali ya Izrael na kundi la Hamas.
Jambo ambalo limefurahiwa katika Ukanda wa Gaza na West Bank wakati walipokuwa wanawapokea Wapalestina waliochiwa kutoka katika jela za Izrael.
Shirika la Afya la Dunia kupambana na malaria kwa hali na mali
Geneva, Uswisi - 18/10/2011. Idadi ya watu wanao poteza maisha kutokana na ugonjwa wa malaria umepungua kwa asilimia 20, kwa mujibu wa ripoti ya shirika la afya la Umoja wa Mataifa (WHO).
Katika ripoti hiyo WHO imesema "kufanikiwa kupungua kwa kuenea kwa ugonjwa wa malaria kumetokana na ufuatiliaji wa ukaribu katika kupambana na ugonjwa huo na tunamatumaini kuuangamiza kabisa katika baadhi ya nchi ifikapo 2015."
Shirika la afya duniani lilianza kupambana na ugonjwa wa malaria tangu 1955 ambao umepoteza maisha ya watu wengi hasa katika nchi zilizopo Kusini mwa Sahara.
Hillary Clinton afanya ziara ya ghafla nchini Libya.
Tripol, Libya - 18/10/2011. Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani amewasili nchini Libya kwa ziara ya kiserikali.
Hillary Clinton aliwasili nchini Libya ili kuongea na viongozi wa serikali ya mpito na kutaka kujua maendeleo yaliyofikiwa tangu kuangushwa kwa Kanali Muammar Gaddafi.
Waziri Hillary Clinton akiwa ziarani Libya alisema "
Nina furaha kusimama hapa kuona wananchi wa Libya wakiwa huru na kwaniaba ya Marekani napenda kuwapa pongezi."
"Ningetumaini kama Gaddafi angekamatwa au kuuwawa na Walibya wakawa huru siku zote."
"Na naimani serikali ya mpito itawaunganisha Walibya wote ili kuijenga upya Libya." Alimalizia kwa kusema waziri Hillary Clinton.
Ziara ya Hillary Clinton nchini Libya imefanyika bila kutangazwa kwenye vyombo vya habari.

No comments: