Monday, October 24, 2011

Bomu la lipuka katika ukumbi wa starehe jijini Nairobi.

Mtoto wa Gaddafi ahaidi kulipiza kisasi.

Al Rai, Syria TV Station - 24/10/2011. Mtoto waaliyekuwa kiongozi wa Libya amehaidi kuendelaza mapambano na serikali ya mpito ya Libya na kulipiza kisasa kwa niaba ya wale wote waliopoteza maisha katika kipindi cha miezi 8 ya harakakati za kuung'oa utawala wa baba yake marehemu Muammar Gaddafi.
Saif al-Islam aliseme kupitia TV iliyopo nchini Syria " tutaendelea kupambana, mimi ni Mlibya nipo Libya tayari kupambana na kulipiza kisasi na tutahakikisha tulalinda mali asili ya Libya zidi ya wavamizi na waasi wa nchi."
Mtoto huyo wa marehemu kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi ambaye aliuwawa wakati hivi karibuni, inasemekana ameteuliwa kuwa kiongozi kushika madaraka aliyo yaacha baba yake ya chama cha kitabu cha kijani, na vile vile kuungwa mkono na viongozi wa kabila la kwao ambao wamehaidi kupambana bega kwa bega na Saif Al-Islam zidi ya serikali ya mpito.
Mpaka sasa hivi haijulikani mahali Saif Al-Islam alipo, japo inasadikiwa ya kuwa yupo katika maeneo ya jangwa ndani ya Libya.
Wakati huohuo, shirika la kutetea haki za binadamu, limedai uchunguzi zaidi unabidi ufanyike baada yakujulikana ya kuwa wafuasi wa kiongozi wa zamani wa Muammar Gaddafi waliuwawa wakati jeshi la upinzani lilipo ingia mjini Sitre.
Maiti za watu hao wapatao 53 zilipatikana ndani ya hotel na huku mikono yao ikiwa imefungwa.
Habari zinasema wengi ya watu walio uwawa walikuwa wafanyakazi wa serikali ya Muammar Gaddafi.
Shirika hili limedai haya nimauaji ya kiana nainaelekea kulikuwa na ukiukwaji wa haki za kibinadamu.
Bomu la lipuka katika ukumbi wa starehe jijini Nairobi.
Nairobi, Kenya - 24/10/2011. Watu kumi na mbili wameumia vibaya baada ya bomu kulipuka ndani ya ukumbi wa kuchezea musiki jijini Nairobi.
Msemaji wa Polisi wa Kenya Charles Owini alisema " mpaka sasa bado tunafanya uchunguzi na tutatoa habari kamili baada ya uchunguzi wa tukio hilo."
Mlipuko huo umekuja baada ya ofisi za Marekani nchini Kenya "kuwaonya raia wa nchi yake kama wanapanga mpango wa kuja kutembelea wafikilie kwa undani kwani hali ya mashambulizi inaweza tokea wakati wowote."
Kwa mujibu wa habari hizo zilisema ya kuwa mashambulizi yanaweza tokea katika maeneo wanayofikia watalii na kumbi za starehe.

No comments: