Wednesday, January 4, 2012

Marekani na Iran bado wavuta juu ya Ghuba Strait Hormuz.

Makundi ya upinzani yatupiana risasi Tripol Libya.

Tripol, Libya - 04/01/2012. Makundi yaliyo saidia katika  kuuong'oa utawala wa aliyekuwa kiongozi wa Libya yametupiana risasi jijini Tripol.
Makundi hayo Misrate Brigade na jeshi la Tripol  yalitupia risasi katika mtaa wa Saeedi na kusababisha vifo vya watu sita na wengine kujeruhiwa.
Kwa mujibu wa habari zinasema mapiganio hayo yalianza wakati mmoja wa wapiganaji wa Misrata kukamatwa kwa kushukiwa kuiba."
Kufuatia vurugu hizo serikali ya mpito NTC ya Libya imetuma wasuruhushi na walinzi zaidi ili kutuliza ghasia hizo.
Serikali ya mpito ya Libya  National Transitional Council NTC imekuwa na wakati mgumu katika kuimarisha ulinzi kutoka na nakuwepo makundi tofauti ambayo yanamiliki maeneo tofauti.

Marekani  na Iran bado wavuta juu ya Ghuba Strait Hormuz.



Washington, Marekani - 04/01/2012. Serikali ya Marekani imetangaza kuendelea na shughuli zake za ulinzi katika Ghuba zilizo karibu na Iran japo Iran imetoa onyo ya kuwa inafanya mazoezi ya kijeshi kwenye eneo hilo
George Little msemaji wa idara ya ulinzi  Pentagon alisema melikebu za kijeshi la Marekani zitaendelea na kazi zake za ulinzi kama kawaida na zinafanya kazi kwa kutumia sheria za kimataifa."
Majibu hayo ya Marekani yamekuja baada ya Iran kutoa onyo huku ikiendelea mazoezi ya kijeshi katika Ghuba ya Strait Hormuz.

No comments: