Saturday, January 7, 2012

Nelson Mandela kutokuwepo kwenye sherehe ya miaka 100 ya ANC chama tawala.

Jamaika kujitenga na uongozi wa Kifalme wa Uingereza.

Kingstone, Jamaika - 07/01/2012. Waziri mkuu aliyechaguliwa hivi karibuni katika uchaguzi mkuu uliyo fanyika nchini Jamaika ametangaza ya kuwa Jamaika itavunja uhusiano na Ufalme wa Uingereza na kuwa nchi huru kijamuhuri.
Waziri mkuu Portia Simpson Miller alisema " serikali iliyo chaguliwa na wananchi kwa kipindi hiki itaanza na kuiandaa Jamaika kuwa jamuhuri na kuwa na uwezo wa kujichagulia rais ambaye atakuwa raia wa Jamaika na kukata mahusiano ya kiuongozi na Ufalme wa Uingereza.
Nampenda Malkia, ni mfano kwa wanawake wote, ni mzuri kwa sura, yupo imara, anabusara katika kila jambo analo fanya, lakini nafikiri wakati umefika kwa Jamaika kuwa na uwezo wa kujichagulia uongozi wake na kujiongoza."
Uamuzi huo wa Jamaika kujitoa kuwa chini ya Ufalme wa Uingereza tangu uhuru umekuja baada ya baadhi ya Wajamaika kudai ya kuwa hakuna wanacho faidika kimsingi na Uingereza, na uhusiano umezidi kuwa mgumu hasa baada ya Uingereza kutaka Wajaimaka wapete viza kabla kuingia Uingereza.
Serikali mpya ya Jamaika ambayo itaongozwa na Portia Simpson Miller itakuwa na kibarua kigumu katika kukuza uchumi na kupambana na ukosefu wa kazi kati ya wananchi wa Jamaika ambao umefikia asilimia 13.

Kenya yatahadharishwa na mashambulizi ya kigaidi.


Nairobi, Kenya -07/01/2012. Serikali ya Kenya imepokea tahadhari yakuwa kuna mpango wa magaidi kufanya mashambulizi nchini humo.
Tahadhari hiyo ilitolewa na  Uingereza imekuja wakati jeshi la Kenya likiwa linapambana na kundi la Al Shabab lililopo nchini Somalia.
Kwa mujibu wa habari kutoka ofisi za nchi wanachama wa jumuiya ya nchi zilizo tawaliwa na Waingereza zilisema " tunaamini ya kuwa kuna mpango wa mashambulizi ambayo yamefikia hatua za kutekelezwa na na tunaiomba serikali ya Kenya kuwa katika hali ya tahadhari."
"Mashambulizi yanaweza tokea katika maeneo ya hotel za kitalii na sehemu ambazo huwa zinafanyika mikutano ya kitaifa na kimataifa."
Msemaji wa serikali ya Kenya Afred Mutua alisema " vitisho vya mashambulizi vimekuwa vikitokea kila wakati na tumekuwa katika tahadhali kila wakati na tunaaamini kundi la Al Shabab lina mpango huo."
Hata hivyo tahadhali hiyo ya mashambulizi ya kigaidi zidi ya Kenya hayakueleza kiundani kuhusu mpango wa mashambulizi hayo na ofisi za serikali za kigeni zilizopo nchini Kenya zimekuwa zikitoa tahadhali uwezekano wa Kenya kushambuliwa na magaidi.

Nelson Mandela kutokuwepo kwenye sherehe ya miaka 100 ya ANC chama tawala.


Johannesburg, Afrika ya Kusini - 07/01/2011. Chama tawala nchini Afrika ya Kusini African National Congress- ANC na ambacho kilikuwa mstari wa mbele katika kupinga ubaguzi wa rangi nchini Afrika ya Kusini kimeandaa sherehe yakutimiza miaka mia tangu kuanzishwa.
Habari kutoka kwa ofisi cha chama hicho ambacho kilianzishwa 08/01/1912, zimesema "katika kuadhimisha sherehe hiyo viongozi wastaafu wa chama hicho watakuwepo ispokuwa rais wa kwanza wa Afrika ya Kusini baada ya kuangushwa kwa serikali ya ubaguzi wa rangi Nelson Mandela 93 hatakuwepo."
Mahazimisho ya sherehe miaka mia ta chama cha ANC yatatanguliwa na hotuba na shughuri mbalimbali za kujenga taifa.

Rais wa Sudani afanya ziara ya kiserikali nchini Libya.


Tripol, Libya -  Serikali ya mpito ya Libya imemkaribisha rais Sudan ambaye anatafutwa na mahakama ya kimataifa inayo shughulikia makosa ya ukiukwaji wa haki za binadamu ili kujibu mashitaka katika kesi aliyofunguliwa ya kuwa anahusika katika kukiuka haki za binadamu.
Omar Hassan al Bashir aliwasili nchi Libya na kufanya mazungumzo na viongozi wa serikali ya mpito baada ya serikali ya Muammar Gaddafi kutokuwa na uhusiano mzuri na Khartoum kwa madai serikali ya Gaddafi ilikuwa ikiwasaidia wapinzani wa serikali ya Sudan.
Serikali ya Sudan imekumbwa na wakati mgumu kufuatia kugawika kwa nchi ya Sudan, ambapo eneo kubwa lenye mafuta limekuwa mikononi mwa serikali ya nchi mpya Sudani ya Kusini.

 Wanajeshi wazidi kulisaliti jeshi la serikali nchini Syria.


Hama, Syria - 07/01/2012. Mmoja wa wakuu wa jeshi la Syria na wanajeshi wengine 50 wamekimbia na kusaliti jeshi la serikali  kwa madai ya kuwa serikali hifanyi haki kwa wananchi wake wanao andamana.
Kanali Affet Mahmoud Suleiman ambaye ana toka katika kambi inayo shughulikia maswala ya anga alitangaza kusaliti jeshi kwa kusema "tumeamua kujitoa kwenye jeshi la serikali kutokana na vitendo vya jeshi na maafisa usalama wa serikali kushiriki katika mauaji. Na tunaomba kama kuna mtu atusaidie kutafuta kaburi lililo wekwa wanajeshi walio uwawa."
Serikali ya Syiria imekuwa na wakati mgumu tangu kuanza maandamano ya kupinga serikali na mauaji yamekuwa yakitokea mara kwa mara na kukadiliwa kuna watu zaidi ya 3000 wamesha uwawa na wengine kujeruhiwa.

No comments: