Wednesday, January 11, 2012

Ukweli wa serikali ya Rwanda wathibitishwa.

Mwanasayansi mwingine wa Iran auwawa na bomu.


Tehran, Iran - 11/01/2012. Bomu lililokuwa limetegwa kwenye gari  limelipuka na kumuua mwanasayansi wa maswala ya kinyuklia nchini Iran.
Mostafa Ahmad-Roshan ambaye alikuwa mwalimu na mmoja wa wanasayansi anayeshughulikia uboreshaji wa madini ya kinyuklia alifariki dunia baada ya gari alilo kuwa akitumia kulipuliwa na bomu lililo kuwa limetegwa katika gari yake aina ya Peugeot 405.
Kwa mujibu wa habari zilizo tolewa na shirika la habari la Iran FARS limesema " bomu hili huenda bomu hilo limepachikwa  na kulipiliwa kwa kutumia kiwasha (kistua) mbali."
Serikali ya Iran imesema " mauaji ya wanasayansi wetu yahatasimamisha jitihada za kuendelea na mradi wa sayanyi wa kinyuklia na mauaji haya kwa 100% yamefanywa na Mossad shirka la ujasusi la Izrael kwa nia ya kusimamisha juhudi zetu za kisayansi."
Iran imekuwa ikikumbwa na matukio ya wanasayansi wake wanao shughulikia maswala ya kinyuklia kuuwa kwa milipuko ya mabomu kwa kipindi cha miaka miwili sasa.


China na Marekani zashidwa kuafikiana juu ya Iran. 


Beijing, China - 11/01/2012. Serikali ya Marekani imeshindwa kuafikiana na serikali ya chini katika jitihada za kuiwekea vikwazo Iran baada ya kufanyika mazungumzo kati ya waziri wa fedha na mipango ya uchumi wa Marekani Timoth Geithner na viongozi wa China.
Waziri wa mambo ya nchi za nje wa China Zhai Jun alisema "hatukubaliani na muswada wa kutumia nguvu kwa kuwekewa vikwazo nchi ya Iran, kwani havisaidii na tunatarajia vikwazo vilivyo wekwa havita hathiri uchumi wa China."
China ni nchi ambayo nimnunuzi mkubwa wa mafuta kutoka Iran, na imekuwa ikipinga kuwekewa vikwazo kwa Iran kwa madai havisaidi, la muhimu ni kufanya mazungumzo, jambo ambalo limekuwa ligumu kufanyika kati ya serikali ya Iran na nchi za Magahribi zinazo dai kwanza Iran isimamishe uzalishaji wake wa madini ya kinyuklia.


Ukweli wa  serikali ya Rwanda wathibitishwa.


Paris, Ufaransa - 11/01/2012. Wachunguzi walio kuwa wanachunguza uangukaji wa ndege iliyo muua rais wa Rwanda 1994 Juvenal Habyarimana, wamethibitisha ya kuwa watu waliokuwa karibu na  rais wa sasa wa Rwanda hawakuhusika katika uangushwaji wa ndege hiyo.
Shutuma hizo ambazo hapo awali zilidai ya kuwa watu  saba walio kuwa karibu ya rais Paul Kagame ndiyo waliohusika katika kuangusha ndege hiyo na kupelekea kufunguliwa kwa kesi hiyo kwani katika ajali hiyo walikuwepo raia wa Kifaransa.
Wachunguzi watoa repoti kwa kusema " uangushwaji wa ndege iliyokuwa imebeba rais Juvenal Habyarimana iliangushwa na wanajeshi wa waliokuwa ndani ya serikali."
Waziri wa mambo nchi za nje wa Rwanda Louise Mushikiwabo alisema " ukweli uliopatikana umethibitisha ya kuwa watu walioshutumiwa hawakuhusika katika kufanya kitendo hicho na serikali ya  Rwanda ilisha kanusha madai hayo ya kuhusika katika kuangusha ndege hiyo."
Hapo awali mwaka 2006 serikali ya Ufaransa ilitoa kibali cha kukamatwa watu hao saba wakamatwe wakiingia ndani ya Ufaransa, jambo ambalo lilipelekea uhusiano kati ya Rwanda na Ufaransa kuzorota hadi mwaka 2009 ulipo anza kuimarika.

Libya yatakiwa kueleza ni kwa namna gani kesi ya Seif al Islam  Gaddafiitaendeshwa.


Tripol, Libya - 11/01/2012. Serikali ya mpito ya Libya imeagiziwa na mahakama ya kimataifa inayo shughulikia makosa ya ukiukwaji wa haki za binadamu kutoa majibu sahihi kuhusu kesi ya Seif al Islam Gaddafi itakavyo endeshwa ifikapo Jumanne wiki ijayo.
Uamuzi wa mahakama ya kimataifa kuuliza umekuja baada ya muda wa makubaliano uliyo wekwa kati ya  serikali ya mpito na mahakam ya kimataifa kuhusu uendeshaji wa kesi zidi ya Seif al Islam Gaddafi  kupita tangu akamatwe akiwa njiani kutoroka kutoka nje ya Libya.
Seif al Islam Gaddafi ambaye ni mtoto wa aliye kuwa rais wa Libya Muammar Gaddafi aliye tolewa madarakani na muungano wa makundi yaliyo ongozwa na serikali ya mpito kwa msaada wa NATO na baadaye kuuwawa.

Rais wa Syria ashutumu nchi za jumuiya ya Kiarabu.


Damascus, Syria - 11/01/2012. Rais wa Syria amelihutubia taifa na kuitupia lawama jumuiya ya nchi za Kiarabu kwa kujaribu kuiyumbisha Syria.
Rais Bashar al Assad alisema " Hii jumuiya ya nchi za Kiarabu na ufalme wao wana in haki gani ya kutufundisha sisi wa Syria. Bunge la kwanza la Syria lilikuwa mwaka 1917, je hizi nchi za kifalme zilikuwa wapi? na  vurugu na mashambulizi yanayo tokea nchini Syria ni ya makundi ya kigaidi ambayo yanapata misaada toka nchi za nje.
"Hali hii ni sawa na mganga kumkataza mgonjwa asivute sigara, wakati mganga anasigara mdomoni."
"Sijawahi kutoa ruhusa ya kuwa watu wapigwe risasi, na kutoka kwangu madarakani kutakuwa ni maamuzi ya wanachi."  Alisema rais Assad.
Rais Bashar al-Assad alitoa hotuba hiyo kwenye chuo kikuu  Damascus, mwezi mmoja sasa tangu kuwepo na waangalizi 165 wa jumuiya ya nchi za Kiarabu waingie nchini Syria ili kukagua hali halisi ya vurugu zinazo endelea.

No comments: