Saturday, January 21, 2012

Mashindano ya kugombea kombe la nchi bingwa katika bara la Afrika ya anza.

Mashindano ya kugombea  kombe la  nchi bingwa  katika bara la  Afrika ya anza.


Malabo, Equqtorial Guinea - 21/01/2012. Mashindano ya mpira wa miguu yanayo zikutanisha nchi za Kiafrika zilizo fauru kuingia kwenye fainali za kugombea ubingwa wa Afrika katika mchezo wa mpira wa miguu yameanza rasmi nchini Equatorial Guine katika jiji la Malabo.
Katika ufunguzi wa mashindano hayo wenyeji timu ya taifa ya Equarorial Guinea watafungua mashindano hayo kwa kukwaana na timu ya taifa ya Libya.
Sauti za mavuvuzela zimekuwa zikisikika kila kona ya jiji la Malabo tayari kwa kuwakaribisha watu wote anao shiriki katika mashindano hayo hasa timu za mpira wa miguu za mataifa yanayoshiriki.
Mashindano hayo yametayarishwa na nchi mbili Gabone na Equatorial Guinea.

Chama cha Kiislaamu cha shinda uchaguzi nchini Misri.


Kairo, Misri - 21/01/2012. Matokeao ya uchaguzi uliyofanyika nchini Misri yameipa chama cha Kiislama ushindi mkubwa zidi ya vyama vingine ya siasa.
Chama cha Muslim Brotherhood Freedom kimeshinda uchaguzi huo kwa kupata asilimia 47 ya viti katika bunge lijalo la nchi hiyo.
Uchaguzi huo ni wa kwanza tangu kuangushwa kwa madarakani amliyekuwa rais wa Misri Husni Mubara mwaka jana, kutoka na maandamano makubwa yaliyo fanyika nchini humo.

serikali ya Nigeria yatangaza hali ya hatari katika mji wa Kano.

Kano, Nigeria - 21/01/2012.Serikali ya Nigeria imetangaza hali ya hatari na kuweka vizuizi katika mji wa Kano kufuatia milipuko ya mabomu iliyo sababisha mauaji ya watu 126 na wengine kujeruhiwa vibaya.
Kundi la Boko Haramu limedai ya kuwa limehusika na milipuko hiyo.
Kufuatia milipuko hiyo, serikali ya Nigeria imefunga mipaka inayo pakana na Niger na Kamerooni kwa madai ya kuwa mipaka hiyo imekuwa ikitumika na makundi kama Boko Haram.

Kiongozi wa kundi Hamas Khaled Meshaal la  kutogombani  uongozi tena. 

Ghaza, Palestina - 21/01/2012. Kiongozi wa kundi la Hamas ametangaza ya kuwa hatagombea tena kiti cha uongozi wa kundi hili ambalo amekuwa kiongozi tangu mwaka 2004.
Khaled Meshaal alisema hayo wakati alipo kutana  na jopo la viongozi wa kundi Hamas na kusema " nimeamua kutogombea uoangozi huo kutokana na sababu za kibinafsi na hata hivyo nitazidi kutumikia chama changu cha Hamas na watu wa Palestina."
Khaled Meshaal alichukua uongozi wa kundi la Hamas baada ya kifo cha Abdel Aziz al Rantisi, ambaye aliuwawa na jeshi la Izrael.

Yemeni yapitisha sheria ya kulinda rais asishitakiwe akitoka Madarakani.


Sanaa, Yemen - 21/01/2012. Bunge nchini Yemen limepitisha mswada ambao utamlinda rais asiweze kushitakiwa
Sheria hiyo ambayo ilichelewa baada ya rais wa Yemen kutaka mabadiliko yafanyike ili kumpa nafasi ya yeye na wenzake ambao walikuwa wanaongoza serikali kuwekewa nguzo ya kisheria ambayo itawalinda washishitakiwe baada ya kutoka madarakani.
Waziri wa habari  Ali al Amrani alisema " sheria hii imepita na itasaidia kuleta na kufikia malengo ya amani na mabadiriko ya kisiasa ambayo ndiyo kilio cha wananchi wa Yemen." 
Kufuatia kupitishwa kwa sheria hiyo, rais wa Yemen Ali Abdullah Saleh atajihudhuru na kutoka katika kiti cha urai ambacho amekikalia kwa muda miaka 33.

Madagaska yamkatalia rais wazamni kurudi nchini mwake

Madagaska, Antananarivo - 21/01/2012. Ndege ambayo ilikuwa imembeba aliyekuwa rais wa zamni wa Madagaska  na aliyetolewa madarakani mwaka 2009 na kukimbilia ukimbizini nchini Afrika ya Kusini ilikataliwa kuingia anga la Madagaska.
Rais Marc Ravalomanana ambaye alikuwa akielekea nchini mwake baada ya kukua ukimbizini nchini Afdrika ya Kusini, alijikuta akikataliwa kuingia nchini Madagasca.
Kwa mujibu wa serikali ya Madagaska zinasema "ikiwa Marc Ravalomanana atarudi nchini Madagaska atakamatwa na jambo hili linaweza kuleta vurugu katika nchi, kwani watu ambao wanamuunga mkono wanasubiri kitendo hicho."
Hata hivyo, Marc Ravalomanana alisema " nataka kurudi nyumbani ili kuongoza na kuleta mabadiliko ya kisiasa yenye amani na siyo kuleta vurugu."
Marc Ravalomanana amekuwa akitaka kurudi nchini mwake,lakini serikali ya Madagasca imekuwa ikimkatalia kwa kuhofia ya kuwa kurudi kwake kunaweza kuleta mchafuko wa amani.

No comments: