Friday, January 27, 2012

Pevez Musharraf achelewesha nia yake ya kurudi Pakistan.

Etienne Tshisekedi bado alia na rais Joseph Kabila. 


Kinshasa, Jamuhuri ya Kidemokrasia Kongo - 27/01/2012. Mpinzani wa serikali ya Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo Etien Tshisekedi amewaagiza wadau nawale wote wanao muunga mkono kuendela kuandamana hadi hapo watakapo fanikiwa nia yao.
Etienne Tshisekedi ambaye ni kiongozi  wa chama cha Unino Democracy and Social  Progress (UDPS), na anapinga kwa madai ya kuwa rais wa sasa Joseph Kabila hakushinda uchaguzi,na hastahili kuwa rais wa nchi na kudai yeye ndiye aliyeshinda uchaguzi na anatakiwa aongoze nchi.

Pevez Musharraf achelewesha nia yake ya kurudi Pakistan.



Islamabad, Pakistan - 27/01/2012. Aliyekuwa rais wa Pakistan na ambaye anaishi nchi Uingereza, amechelewesha nia yaa ke ya kurudi nyumba Pakistan, kwa kutishiwa kukamatwa.
Pevez Musharraf ambaye alikuwa rais wa Pakistan na mkuu wa jeshi mwaka , ambaye baada ya kuachia madaraka 2008 aliamia Uingereza na baadaye mapema miaka miwili alitangaza kurudi nyumbani ili kugombania kiti hicho cha urais tena kwa kupitia chama chake All Pakistan Muslim League.
Msemaji wa chama ambacho Pevez Musharraf angegombania kiti cha urais Muhammad Ali Saif alisema " Uamuzi wa kuchelewesha kurudi nyumbani kwa Pevez Musharraf ni uamuzi ambao chama kilimlazimisha kufanya hivyo baada ya kukaa kikao kwa muda wa masaa  mawili, jambo ambalo Pevez Musharraf alikuwa amelipinga.
"Na chama kitaamua lini Pevez Musharraf atarudi nyumbani Pakistan."
Uamuzi wa  kuimzuia Pevez Musharaf asirudi Pakistan, umekuja baada ya bunge kupitisha uamuzi ya kuwa akirudi nyumbani lazima akamatwe.


Viongozi wa dunia waagiziwa kutupia macho swala la wakimbizi duniani.


Davos, Uswis - 27/01/2012. Mkuu wa shirika la umoja wa mataifa linalo shughulikia hali na maswala ya wakimbizi amewaagiza viongozi walioudhuria kwenye mkutano wa kutasmini hali ya uchumi dunia ya kuwa wasifunge milango na kulitupia macho swala la wakimbizi ambalo linaongezeka kila siku.
Antonio Guterres alisema " hali ya kutokuwepo na utulivu na amani na vita vimekuwa vikiwaacha mamilioni wakiwa wanaishi katika maaisha ya kikimbizi na magumu.
Wakati vita na vurugu watu wanashindwa kujenga maisha yao, katika nchi yao na kukumbilia maaeneo yaliyo na amani jmbo ambalo watu wengi wamekuwa naa wakati mgumu, kwa mfano zaidi ya watu 350,000 ambao wameacha makazi hasa katika nchi za Sudan na Somalia."
Viongozi kutoka nchi tofauti duniani wanakutana ili kujadili haali halisi ya uchumi duniani.

No comments: