Sunday, January 1, 2012

Duniani kote washangilia mwaka mpya.

Duniani kote washangilia mwaka mpya.


Muhariri. Launite.blogspot.com - 01/01/2012. Nifuraha iliyoje kila ifikapo wakati wa mwaka kumalizika, kila mtu anakuwa na shahuku kubwa kutaka kufika mwaka unaofuata.
Hii ndivyo ilivyo kuwa duniani kote. Japo  watu wengine walishangilia kabla ya wengine, kutokana na utofauti wa kijiografia, lakini haikusababisha kupunguza furaha.
2012 ni mwaka ambao wengi wetu tusingependa uwe kama mwaka 2011.
Kwani mwaka 2011 umekuja kwa vishindo.
Hata hivyo naomba tukumbushane kale  kajiografia ya kuwa  mwaka 2012 ni mwaka mrefu.
Kama unakumbuka wakati ulipo kuwa darasani,  mwalimu wa jiografia  alifundisha mwaka mrefu na mfupi, na kusema mwaka mrefu huwa unagawanyika kwa 4.
Bila shaka 2012 una kiwango hicho.
Kwaniaba ya launite.blogspot, nawatakia heri na mafanikio ya mwaka mpya wa 2012 na kila kitu kizuri tukipangacho kiwe chenye urefu wa mafanikio kama mwaka 2012.
Mungu atubariki wote 
                      Muhariri mkuu.


Watano wapoteza maisha baada ya mashabulizi nchini Kenya.


Garissa, Kenya - 01/01/2011.  Watu watano wameuwawa na wengine 20 wamejeruhiwa vibaya baada ya klabu ya starehe kushambuliwa Kaskazini Mashariki mwa Kenya kwenye mji wa Garissa.
Mashambulizi hayo ya mabomu ya kutupwa kwa mkono yalifanywa wakati watu wakiwa wanajiandaa kusherekea mkesha wa mwaka mpya 2012.
Kwa mujibu wa shahidi aliyekuwepo kwenye tukio hilo alisema " baada ya mlipuko huo kulikuwepo miripuko ya risasi kuelekea walipo watu na kusababisha watu kukimbia kujificha."
Mkuu wa polisi wa Leo Nyongesa  alithibitisha kwa kusema " watu watano wamefariki dunia na wengine kujeruhiwa na polisi imeanza uchunguzi mara moja na itahakikisha inawakamata wale wote walio husika katika kufanya kitendo hicho."
Mji wa Garissa upo kilomita 100 kutoka mpaka na nchi ya Somalia, ambapo jeshi la nchi ya Kenya linapambana na kundi la Al-Shabab kwa miezi mitatu sasa.
Naye rais wa Kenya  Mwai Kibaki alisema " usalama wa Kenya hautachezewa na tuta hakikisha yoyote ambaye anataka leta vurugu anasimamisha na Kenya  itamaliza kazi iliyo anza ya kupambana wale wanao leta vurugu ili amani isiwepo nchini Somalia, kwani wananchi wa Somalia ni ndugu zetu na tutawasaidia kwa hali na mali mpaka amani ipatikane."
"Amani ya Somalia ni msingi muhimu katika kuimarisha na kustawisha demokrasia kwenye nchi za Pembe ya Afrika Mashariki." aliongezea rais Kibaki.
Tangu jeshi la Kenya kuanza mashambulizi zidi ya kundi la Al-Shabab  Kenya imekuwa ikikumbwa na mashambulizi ya mabomu katika kumbi za starere, jambo ambalo limefanya serikali ya Kenya kuongeza ulinzi na usalama kwa wananchi wake.

Rais Baraka Obama atia sahii vikwazo vya kibenki zidi ya Iran.


Washington, Marekani - 01/01/2011. Rais wa Marekani ametia sahii sheria ya kutaka vikwazo zaidi zidi ya serikali ya Iran.
Rais Baraka Obama alitia sahii mkataba ambao utazuia mabenki ya Marekani kufanya biashara na benki za Iran zikiwemo biashara za aina yoyote zinazo husisha maswala ya kifedha.
Kwa mujibu wa sheria hiyo " makampuni yanatakiwa kuchagua kufanya biashara na benki za Iran au benki za Marekani katika kufanya bishara zao."
Sheria hiyo ya vikwazo juu ya Iran katika mabenki, huenda ikaleta mvutano na serikali za Uchina na Urussi nchi ambazo zimekuwa zikifaya biashara na Iran mara kwa mara.
Vikwazo hivyo vimekuja wakati nchi za umoja wa Ulaya zinajiandaa kufanya mazungumzo na serikali ya Iran ikiwa hakuna vipingamizi vitakavyo wekwa.

Iran yadai yakuwa imefanikiwa kutengeneza chembe nyuklia.


Tehran, Iran-01/01/2012. Serikali ya Iran imetangaza ya kuwa imefanikiwa kutengeneza madini ya chembe nyuklia ambayo yamesimamiwa na wanasayansi wa Kiiran bila msaada kutoka nje ya nchi.

Gazet la Tehran Times limeripoti ya kuwa " kufanikiwa huko kwa Iran kuwa nauwezo wa kutengene na kuzalisha madini ya kinyuklia  kumekuja kinyume na nchi za Magharibi ambapo zilizani Iran haitafanikiwa  kutengeza madini hayo."
Ugunduzi wa  chembe nyuklia  hizo ambazo zitatumika katika kuimarisha mitambo ya kinyuklia nchini Iran kumekuja wakati jeshi la Iran likiwa linafanya mazoezi ya kijeshi na kujaribu siraha ambazo zimetengenezwa nchi Iran na wanasayansi wa Iran.
Hata hivyo serikali ya Iran imekuwa ikishikilia msimamo wake ya kuwa mradi wa kutengeneza mitambo ya kinyuklia ni kwa ajili ya kuinua sayansi na kutoa huduma bora za nishati kwa wanachi na siyo kwa ajili ya kutengeneza mabomu ya nyuklia.

Wakaguzi waliopo Syria wakutwa na wakati mgumu kutoka kwa bunge la nchi za Kiarabu.


Dumaskas, Syria - 01/01/2012. Baraza la washuri la  bunge la nchi za Kiarabu limetaka wakaguzi wa mambo ya siasa kutoka umoja wa nchi za Kiarabu waliopo nchini Syria kuondoka mara moja.
Mwenye kiti wa bunge hilo Ali al- Salem al Dekbas zinasema " tangu wakaguzi hao kwenda nchini Syria hali haijabadirika na mashambulizi yenye kuamba tana na vurugu yanendelea na kuzuia ukweli kuhusu hali halisi ya ukandamizwaji na mauaji yanayo tokea yasionekane."
Tunaomba katibu mkuu wa nchi za umoja wa nchi za Kiarabu aitishe mkutano wa kuwataka wajumbe hao watoke nchini Syria. " ziliongezea mwenyekiti huyo wa bunge la nchi za Kiarabu.
Hata hivyo habari kutoka zilizo kuwa zimepatikana ya kuwa vyama viwili vikuu vya upinzani vilivyo nje ya Syria  
Syria National Council SNC na National Co-ordination Commitee NCC ya kuwa viliungana katika mkakati wa kutaka kuuong'oa utawala wa rais Bashr al Asaad, umeleta sura mpya baada ya moja ya chama hicho kukanusha ya kuwa hakukua na makubaliano wala mkataba ambao umefikiwa kati ya vyama hivyo viwili vikuu.
Mkurungenzi wa mambo ya uhusiano wa nje wa chama cha SNC Waleed Al Buni alisema " hakuna  makubaliano kama hayo na ilikuwa ni mawazo yaliyo zungumzwa na hayaja fikishwa katika chama."
Hata hivyo mkuu wa NCC Haytham al Manna alisema makubaliano yalisha fanyika kati ya vyama hivyo viwili."
Syria imekuwa na wakati mgumu kutokana na vurugu zinazo endelea kwa muda mrefu na huku mamia ya watu wakiwa wanajeruhiwa kila siki na wengine kupoteza maisha.

No comments: