Sunday, January 29, 2012

Vionngozi na Marais wa Afrika wakutana nchini Ethipia.


Adis Ababa, Ethiopia - 29/01/2012. Viongozi na Marais wa Afrika wanakutana nchini Ethiopia katika mkutano wa kwaza tangu kuuwawa kwa  rais wa Libya Muammar Gaddafi ambaye alikuwa mmoja wa viongozi maarufu katika jumuiya ya mungano wa viongozi wa bra la Afrika.
Rais wa Benin Thomas Boni Yayi  ambaye ndiye mwenyekiti wa kikao hicho cha viongozi wa muungano wa nchi za Afrika alisema " tumekutana hapa ili kujadili na kutafuta ufumbuzi wa matatizo yanayo likumba bara la Afrika hasa nchini Somalia, Sudan, Senegal na Niger, kwani yankuwa yakileta shida na matatizo kwa wanachi wa maaeneo hayo na bara la Afrika kwa Ujumla."
Naye katibu mkuu wa umoja wa Matifa Ban ki -Moon ambaye ameudhuria mkutano huo  alisema  " inapaswa serikali za Afrika ziepukane na ubaguzi wa kijinsia na kuwapa raia wake haki sawa."
Hata hivyo kufuatia hotuba hiyo ya Ban ki- Moon, hakuna maoni yaliyo tolewa na kutoka kwa viongozi wa Afrika ambao hapo mwanzo baadhi ya nchi wanachama wa muungano huo wa Afrika hawakukubaliana na jambo   hili hasa linapo kuja kuhusu swala la ushoga wakati waziri mkuu wa Uingereza alipo lizungumzia kwa mara ya kwanza nchini New Zealand wakati wa mkutanao wa nchi zilizo tawaliwa na Uingereza.

Uzalisha wa mafuta Sudan kuwa na mgogoro kati ya wassudan.

Juba, Sudani ya Kusini - 29/01/2012. Serikali ya Sudani ya Kusini imeamua kussimamisha uzaliashaji wa mafuta hadi hapo itakapo fikia makubaliano na serikali ya Kartoum.
Stephen Dhiue Dau waziri wa madini na nishati wa  udani ya Kusini alisema " kufuatia majadiiliano yaliyo fanyika hivi karibuni kati ya serika ya Juba na Kartoum na kutofikiwaa makubaliano itakuwa vigumuu kuendelea na uzalishaji.
"Katika mkutano huo, serikali ya Kartoum inatakiwa kukubaliana na serikali ya Juba katika maswala ya uzalishaji wa mafuta na kuondoa majeshi yake yaliyopo katika mpaka wa maeneo ya Abyei." Aliongezea waziri Stephen Dhieu Dau.
Mvutano kati aya serikali ya Juba na Kartoum zimekuwa zikivutana tangu Sudani ya Kusini kujitenga na serikali kuu ya Kartoum mwaka jana.


Wakaguzi wa maswala ya kinyuklia wawasili nchini Iran.


Tehran, Iran - 29/01/2012. Wakaguzi wa mswala ya kinyuklia wameawasili nchini Iran kwa ziara ya siku tatu, ili kukagua ni kwa kiasi gani Iran inazalisha zao hilo la kinyuklia kulingana na vipimo vyakimataifa.
Herman Nackaerts ambayye ni kiongozi anaye ongoza msafara wa wajumbe wa shirika linalo simamia maswala ya kinyuklia alisema " tunatumaini serikali ya Iran itashirikiana nasi kwa kila hali ili kupa uhakika wa mpango wao wa kinyuklia."
Katika ziara hiyo wajumbe hao wa shirika ya umoja wa mataifa linalo shughurikia maswala ya kinyuklia watafanya mazungumzo na  waziri wa mambo ya nje ya Iran Ali-Akbar Salehe.
Ziara hiyo ya wajumbe wa shirika la kimataifa linalo shughurikia maswala ya kinyuklia inafanyaka wakati nchi za jumuiya ya Ulaya na Marekani zimeiwekea vikwazo  Iran kwa madai inakiuka viwango vyauzalishaji wa viwango vya nyuklia na kuwa na mpango wa kutengeneza siraha za kinyuklia.

No comments: