Friday, January 13, 2012

Marekani yaomba msamaha kwa Waafghanistani.


Eric Cantona ataka kugombea urais wa Ufaransa.


Paris, Ufaransa - 13/01/2012. Aliyekuwa mchezaji maarufu wa timu ya Manchester United ametangaza wiki hii  nia yake ya kugombea urais wa Ufaransa unao tarajiwa kufanyika hivi karibuni.
Eric Cantona 45 alifanya uamuzi huo na kuandika barua kwa Mameya ili kupata sahii 500 ambazo zitamwezesha kugombea uchaguzi wa rais.
Eric Cantona ambaye atakumbukwa  mmnamo mwaka 1995, arimrukia mmoja ya wapenzi wa mpira wa miguu aliye mtupia maneno machafu wakati Cantona akiwa uwanjani akicheza mechi.
Wanachi wa Ufaransa wanatarajia kufanya uchaguzi wa raia hivi karibu, ambapo rais wa sasa Nicolas Sarkozy atagombea tena kiti hicho kwa mara ya pili.

Kundi la al Shabab lafanya mauaji nchini Kenya.


Gerille, Kenya - 13/01/2012. Kundi la al Shabab limefanya mashambulizi na kuwauwa watu sita na kuteka nyara watu watatu.
Watu walio uwawa ni polisi wanne, mfanyakazi mmoja wa serikali na raia mmoja baada ya kushambuliwa kwa sisasi katika mji wa Gerille uliopo karibu na mpaka wa Kenya
Mkuu wa polisi wa Gerille Leo Nyangosa alithibitisha habari za mashabulizi hao na kuuwawa kwa watu sita na wengine kutekwa nyara na kundi la al Shabab.
Kundi la al Shabab limedai ya kuwa mashambulizi hayo ni kisasi kutokana na kitendo cha serikali ya Kenya kuvamia nchini Somalia.
Jeshi la Kenya liliingia nchini Somalia miezi mitatu iliyopita ili kupambana na kundi la al Shabab ambalo linapingana na serikali ya Somalia na kuhusika na kuteka nyara baadhi ya watalii waliokuwa wamefanya utalii nchini Kenya.


Marekani yaomba msamaha kwa Waafghanistani.


Washingtone, Marekani - 13/01/2012.  Waziri wa ulinzi wa Marekani amemtaka radhi rais wa Afghanistani, baada ya picha za video zilizo sambazwa katika mitanado ambazo zinaonyesha baadhi ya wanajeshi wa Marekani wakikojolea miili ya watu walio kufa.
Waziri wa ulinzi Leon Panetta alisema " nimeziona hizo picha na kitendo hicho kinasikitisha na kinakwenda kinyume na maadili ya jeshi la Marekani na wale waliohusika katika kufanya kitendo hicho wamesha fahamika na watachukukiwa hatu kali."
Naye rais wa Afghanistan Hamid Karzai alisema " hiki nikitendo cha kusikitisha na lazima kilaaaniwe."
Wanajeshi hao ambao walionekana wana kojelea miili ya watu ambao hawajulikani kama ni wapiganaji wa Taliban au raia wa kawaida.
Kitendo cha wanajeshi huenda kikazidi kuleta ugumu kwa wanajeshi wa Marekani waliopo nchini Afghanista ili kuimarisha ulinzi na kuwaandaa Waafghanistan kujilinda wenyewe baaada ya jeshi la Marekani kuondoka nchini humo.

No comments: