Wednesday, January 18, 2012

Janga la njaa laanza kunyemelea nchini Sudan.

Janga la njaa laingia nchini Sudan.

Kordofan, Sudan - 18/01/2012. Mwakilishi wa serikali ya Marekani anayeshughulikia maswala ya Sudan ameonya ya kuwa kuna watu zaidi ya milllion moja watakumbwa na janga la njaa nchini Sudani.
Princeton Lyman alisema "ikiwa huduma za kijamii hazitafikishwa  kwa haraka katika maeneo ya Kusini kwa Kordofan na mto Nile Bluu, basi hali itakuwa mbaya kiasi watu kufa na njaa hadi ikifika mwezi Machi."
Nafikili imefikia wakati wa Afrika kusema kwa sauti moja katika swala hili na kutoruhusu swala hili kutokea na ni wajibu wa viongozi wa Afrika kuleta amani na usalama kwa wanchi wao ili misaada iweze kutolewa kirahisi pindipo inapo itajika na dunia nzima lazima ilitizame tatizo hili."
Balozi wa Sudan nchini Afrika ya Kusini Ali Yusuf Alsharif alisema "hali ineweza kuwa mbaya kuliko Somalia, na hasa nguvu zisizo na busara zinapo tumika kwani zinafanya hali inakuwa tete na kuweka wakati mgumu kwa kila pande."
Princetone Lyman aliyasema hayo nchini Afrika ya Kusini, na kusisi tiza mashirika ya kimataifa yaruhusiwe kufanya kazi zake za kutoa misaada, jambo ambalo serikali ya Sudan imekuwa ikidai yakuwa maeneo hayo ni ya hatari kwa mashirika ya kimataifa.

Vyama vya wafanyakazi vyasimamisha mgomo nchini Nigeria.


Lagos, Nigeria - 18/01/2012. Jiji la Lagos na majimbo mengine nchini Nigeria yamekuwa na utulivu baada ya vyama viwili vya wafanyakazi kukubaliana kusimamisha mgoma ambao ulikuwa umepangwa kutokana serikali kukubali kupunguza bei ya mafuta.
Vyama hivyo Nigeria Labor Congress na Trade Union Congress vilikuwa vimeitisha mgomo kwa wanachama wake kutokana na kitendo cha serikali kutaka kusimamisha rudhuku katika mafuta jambo ambalo lilileta vurugu karibu nchini nzima ya Nigeria.
Uamuzi huo ulifikiwa baada ya rais wa Nigeria Goodluck Jonathan kutangaza ya kuwa serikali itapunguza bei ya mafuta.
Ningeri nchi mojawapo inayo zalisha mafuta kwa wingi duniani, lakini imekuwa namatatizo ya zao hilo jambo ambalo limefikia hata kusababisha hali ya kiusalama katika maeneo yanayi chimbwa zao hilo kuwa tete.


Izrael haina mpango wa kufanya mashambulizi nchini Iran kwa sasa.




Tel-Aviv, Israel - 18/01/2012. Waziri wa ulinzi wa Izrael  ametamka ya kuwa mashambulizi zidi ya mitambo ya kinyuklia ya Iran hayapo kwenye meza yake na serikali haina mpango huo.
Waziri wa ulinza Ehud Barak alisema " uamuzi wa kuyashambulia maeneo yaliyo na mitambo ya kinyuklia nchini Iran ni kitu ambacho si cha ukaribu na cha kuzaniwa kwa sasa, hivyo na nisingependa kuwapa muda maalumu."
Hata hivyo Ehud Barak alishindwa kuelezea kama Iran inauwezo wa kutengeneza bomu la kinyuklia kwa kusema "sijui na siwezi kuthibitisha hilo."
Waziri wa ulinzi Ehud Baraka aliyasema hayo wakati alipokuwa akihojiwa na radio ya kijeshi ya jeshi la Izrael.

Benki ya dunia yaonya kuibuka kwa myumbo wa uchumi duniani.




New York, Marekani 18/01/2012. Benki ya dunia imetahadharisha ya kuwa huenda dunia ikakumbwa tena na myumbo wa kiuchumi ambao utaleta madhara kuli ilvyo tarajiwa.
Onyo hili limekuja baada ya habari kutoka benki hiyo kusema " madeni yanayo zikumba nchi za Ulaya, msukosuko wa usambazaji wa mafuta na soko la kifedha kutokuwa na muhimiri imara ndizo zitakuwa sababu ya kuyumba kwa uchumi wa dunia."
Myumbo wa uchumi duniani umekuwa ikileta vichwa kuuma kwa wakuu wa nchi na viongozi wa sekta mbalimbali kwa muda sasa na bado wapo mbioni kutafuta ufumbuzi wa swala hilo.

No comments: