Sunday, January 8, 2012

Hali ya amani nchini Nigeria ya tikishwa na kundi la Boko Haram.

Chama kilicho ongoza kupinga ubaguzi wa rangi cha Afrika ya Kusini chatimiza miaka 100.


Bleomfontein, Afrika ya Kusini - 08/01/2012. Chama tawala nchini Afrika ya Kusini  African National Congress (ANC) na kilicho ongoza katika kupambana serikali ya ubaguzi wa rangi kimetimiza miaka 100 tangu kuanzishwa.
Rais wa Afrika ya Kusini Jacob Zuma aliwaongoza viongozi wa serikali na waliotoka nyanja mbali  katika
sherehe hizo, ambazo pia maelfu ya raia wa Afrika ya Kusini wakishangili kwa kudai mabadiriko zaidi yanatakiwa ili kuinua maisha ya kila raia wa Afrika ya Kusini.
Akiongea katika sherehe hiyo rais Jacob Zuma alisema "Ninavyo jisikia nivigumu kusema naomba sherehe hii iwe ya wananchi wa Afrika ya Kusini na wale wote walio wezesha kuwepo na kudumu kwa chama hiki tangu kianzishwe na matunda yake tumeyaona."
Katika sherehe hizo aliyekuwa rais wa kwanza wa Afrika ya Kusini Nelson Mandela  hakuweza kuhudhuria kutokana na hali yake, hata hivyo jina lake lilipo tajwa na rais Zuma, watu walishangilia kwa nguvu na vigelegele.
Nelson Mandela alikuwa rais wa kwanza tangu nchi hiyo kufanya uchaguzi huru baada ya kuutokomeza ubaguzi wa rangi.


Hali ya amani nchini Nigeria ya tikishwa na kundi la Boko Haram.

Lagos, Nigeria - 08/01/2012. Rais wa Nigeria amelaumu kundi la Boko Haram ya kuwa linaleta mashaka na kuvuruga amani nchini Nigeria.
Rais Gooluck Jonathan alisema " hali iliyo sababishwa na  kundi hili kwa wananchi kwa kuvuruga amani ni mbaya kwa kulinganisha na  vita vilivyo tokea miaka ya 1967-70 na ipo haja ya kupambana kwa hali na mali.
"Wakati wa vita vya miaka ya siti tuliwezwa kujua mbinu za maadui kulikoni hali ilivyo sasa kwani kwa ugumu ulioyopo ni kwamba baadhi yao wapo ndani ya jeshi, serikali na kwenye bunge la nchii, maafisa usalama na polisi hivyo kuna ugumu mkubwa sana."
Hotuba hiyo ya rais, Gooluck Jonathan imekuja baada yakiongozi mmoja wa kundi la Wakristu kudai yakuwa  "waondoke katika maeneo yaliyo na waislaam wengi kwani wanaweza kuuwawa." Nakusisitiza ya kuwa wa Kristu lazima wajilinde.
Kundi la Boko Haram limekuwa likidai kuhusika na milipuko ya mabomu nchini Nigeria hasa kwenye makanisa.


Rais wa zamani wa Pakistan atangaza kurudi nyumbani.


London, Uingereza - 08/01/2012. Aliyekuwa rais wa Pakistan ambaye kwa sasa anaishi nchini Uingereza ametangaza kurusi nchini Pakistani ingawa kunahabari ya kuwa huenda akakamtwa atakapo rudi nchini mwake.
Rais huyo wa zamani Pervez Musharraf akiwahutubia watu ambao wanamuunga mkono kwa njia ya mtandao  alisema " Narudi Pakistani na siogopi kitu chochote na nafahamu kuna mbinu nyingi zimekuwa zikisemwa kunitisha na natarajia kuwa nchini mwangu kati ya 27 na 30 mwezi huu wa kwanza na hata kama maisha yangu yapo hatarini."
Pervez Musharraf  anashutumiwa katika kuhusika na mauaji ya aliyekuwa waziri mkuu wa Pakistani Bi Benazir Bhuto mwaka 2007, jambo ambalo alikana.
Hata hivyo mwanasheria wa serikali Chaudhry Ali anayeshughulikia kesi ya mauaji ya Bi Benazir Bhuto
amesema "kesi zidi ya Pervez Musharraf imesha fungiliwa na amri ya kukamatwa kwake ipo na sheria itachukua mkondo wake atakapo wasili nchini."
Naye mwanasheria wa Chaudry Faisal ambaye ni mwanasheria wa Pervez Musharraf alisema "kesi hii zidi ya Pervez Musharraf imefunguliwa kwa kisiasa na haina misingi ya kisheria na swala la kutaka Musharraf akamatwe ni la ajabu."
Rais Pervez Musharraf alijiudhuru uongozi mwaka 2008 na anatarajiwa kuwasili nchini Pakistani kwa kutumia shirika la ndege la Arab Emarates na kusindikizwa na wadau wake 500 tayari kwa maandalizi ya uchaguzi utakao fanyika mwakani.


Iran kuandaa mikakati ya kushirikiana na nchi za Amerika ya Kusini.


Karakas, Venezuela -08/01/2012. Rais wa Iran ameanza ziara ya kiserikali katika nchi za Amerika ya Kusini kwa ajili ya kuimarisha uhusiano zaidi na nchi hizo.
Rais Mahmoud Ahmadinejad ameanza ziara yake kwa kutembelea nchini Venezuela na kukutana na rais wa nchi hiyo Hugo Chavez, ikiwa ni mara ya nne kutembelea Venezuela kama rais wa Iran.
Rais Mahmoud Ahmadinejadi atatembelea pia Kuba, Nikaragua na Ekwado ili .kudumisha mahusiano zaidi na kutia sahii mikataba ya kibishara na kiuchumi na nchi hizo.
Wakati huo huo Iran imetoa shukurani kwa jeshi la maji la Marekani kwa kuwaokoa Wairan ambao walikuwa wametekwa na maharamia wa Kisomali na kusema " hili jambo ni la kiutu."
Ziara hiyo ya rais wa Iran katika nchi za Amerika ya Kusini imekuja  huku hali tete ikiwa inaendelea kati ya Iran na serikali za nchi za Magharibi zikiongozwa na Marekani kwa madai yakuwa Iran inampango wa kutengeneza siraha za kinyuklia na huku inaonyesha hivyo kutokana na mazoezi ya kijeshi inayo yafanya katika ghuba ya Persia.


Vifaa muhimu vya kijeshi vya potea katika kambi ya kijeshi nchini Marekani.


Washington, Marekani - 08/01/2012. Jeshi la Marekani limeanza uchunguzi wa hali ya juu ili kujua ni kwa njia gani baadhi ya mitambo muhimu ya kijeshi inayo tumika katika maswala ya anga kupotea.
Kwa mujibu wa habari zilizo patikana zinasema " wafanyakazi wa kambi ya jeshi ya Lewis McChord wanafanyiwa mahaojiano na kundi la wataalamu wa mambo ya uchunguzi wa Marekani.
Meja Chris Ophardt alisema "vifaa viliovyo potea ni vile vinavyo tumika katika maswala ya ulinzi na siraha zikiwemo nyenzo za mionzi.
Uchunguzi huu utaendelea hadi hapo jibu kamili litakapo patikana."
Kufuatia kupotea huko, zawadi ya dolla za Kimarekani 10,000 itatolewa kwa yoyote atakaye wezesha kupatikana kwa vifaa hivyo au habari zitazo saidi upatikanaji wa vifaa hivyo.

No comments: