Sunday, January 22, 2012

Wakenya waombwa kutulia kufuatia uamuzi wowote utakao tolewa na ICC

Wakenya waombwa kutulia kufuatia uamuzi wowote utakao tolewa na ICC.


Nairobi, Kenya - 22/01/2012. Serikali ya Kenya imewataka wanchi wake wawe na hali ya kuwa watulivi kabla na wakati wamatokea ya uamuzi wa mahakama ya kimataifa inayo shughurikia kesi zidi ya ukiukwaji wa haki za binadamu kutoa uamuzi wake kama baadi ya viongozi wa nchi hiyo watashitakiwa.
Katibu mkuu wa maswala ya usalama wa Kenya Francis Kimemia alisema " nimuhimu kwa rais kuwa na amani hasa katika kipindi hiki.
"Kwani pia ikiwa viongozi hao watashitakiwa watakuwa na fursa ya kukata rufaa." Alimalizia Kimemia.
Mahakama ya kimataifa ianayo shughulikia kesi zidi ya ukiukwaji wa haki za binadamau iliyopo nchini Uholanzi chini ya mwana sheria mkuu wa mahakama hiyo Luis Moreno - Ocamp, ilifanya uchunguzi zidi ya mauaji na machafuko yaliyo tokea nchi Kenya kabla na baada ya uchaguzi wa mkwa 2007, na kuwataka baadhi ya viongozi wa vyama vya kisiasa vilivyo shiriki uchaguzi huo wahojiwe kwa uchunguzi zaidi.
Kufuatia uamuzi huo Uhuru Kenyatta Williamu Ruto na viongozi wengine waliwasili nchi Uholanzi na kufanyiwa mahojiwano na mahakama hiyo ambayo inatarajia kutoa uamuzi wake kama kuna kesi zidi ya watu viongozi hao.

Mmoja  wa viongozi wa serikali ya mpito ya Libya  ajiudhulu. 

Bengazi, Libya - 22/01/2012. Mji wa Bengazi umekumbwa na maandamano baada ya wanachi ambao kudai  ya kuwa serikali ya mpito haiwasikilizi hoja jambo ambalo limelazimisha kijiudhulu kwa makamu wa serikali ya mpito.
Abdul Hafez Ghoga alisema " nimeamua kujiudhulu kwa manufaa ya taifa na naamini  nisinge penda kuwa kikwazo na sababu ya kuleta hali yakuto elewana katika kujenga taifa letu."
Abdul Hafez Ghoza ambaye alishambuliwa wakati alipo tembelea chuo kikuuu cha Bengazi, anasadikiwa ya kuwa alikuwa mmmoja ya watu wa karibu wa Muammar Gaddafi.

Rais Ali Abdullah Sareh ajiudhuru urais na kuondoka nchini.

Sanaa, Yemen  - 22/02/2012. Rais wa Yemen amelihutubia taifa la Wayemen kwa mara mwisho akiwa kama rais wa nchi hiyo kabla ya kujiudhuru kiti hicho cha urais na kuondoka kuelekea Oman.
Rais Ali  Abdullah Sareh katika hotuba yake alisema "nomba msamaha kwa yale yoye yaliyo tokea wakati wa utawala wangu wa miaka 33.
"Na kwa  uwezo wa Mungu nitaenda  Marekani kwa matibabu na baadaye nitarudi Sanaa kuongoza chama changu."
Rais Ali Abdullah Sareh ameamua kujiudhuru baada ya bunge la Yemen kupitisha mswaada wa kumlinda ashitakiwe kutokana na makosa yaliyo tokea wakati wa utawala wake, jambo ambalo baadi ya watu wa Yemen wanalipinga na kutaka wale wote waliofanya makosa lazima wafikishwe kwenye vyombo vya sheria.
Rais Ali Abdullah Sareh na serikali yake imekumbwa na vurugu kufuatia vuguvugu la mageuzi ambalo limevumisha upepo katika nchi zote za Kiarabu na kuyumbisha serikali yake.

Saud Arabia yatangaza kuwatoa wajumbe wake katika kamati inayo kagua  nchi Syria.

Riyadh, Saud Arabia - 22/01/2012. Serikali ya Saud Arabia imeamua kuwatoa wajumbe wake ambao wanashiriki katika kuangalia hali halisi ya amani na mvurugo unao tokea nchini Syria.
Waziri wa mambo ya nje ya nchi  wa Saud Arabia mwana wa Kifalme Saud al Faisal alitangaz na kusema " tunatoa wajumbe wetu kwani tunaona serikali ya Syria haitilii mkazo kupunguzwa kwa mauaji na vurugu ambazo zimekuwa zikiendelea kwa muda mrefu na tunaomba jumuiya ya kimtaifa izidi kuisisiza  serikali ya Syria kuleta amani na kukubalia mabadiriko."
Uamuzi wa serikali ya Saud Arabia kuwatoa wajumbe wake katika kamati inayo simamia uangalizi nchi Syria iumekuja  wakati shirikisho la muungano wa nchi za Kiarabu zikiwa zimekubaliana mpango mwingine wa kuongeza muda wakukaa kwa mwezi mmoja zaidi ili kuendele kuangalia na kukagua  hali halisi ya Syria kisiasa Syria na kutoa masharti kwa serikali ya Syria iwaachie watu wote walio jela, kuandaa uchaguzi kwa katika muda wa miezi na kuondoa wanajeshi wake wote waliopo mitaani, kuruhusu maandamano yasiyo leta vurugu, kuhakikisha mauji yanasimamishwa na rais Bashir al Asad kuachia madaraka kwa makamu wake ili kuandaa uchaguzi.

No comments: