Monday, January 23, 2012

Kenyatta Ruto na wengine wawili wahitajika kujibu kesi zidi yao na mahakama ya Hague Uhollanzi.

Kenyatta Ruto na wengine wawili wahitajika kujibu kesi zidi yao na mahakama ya Hague Uhollanzi.

Hague, Uhollanzi - 23/01/2012. Mahakama inayo shugurikia kesi zinazo kiuka haki za binadamu iliyopo nchini Uhollanzi imewafungulia kesi viongozi wanne kutoka Kenya ili kujibu tuhuma zinazo wakabili katika kuhusika na vurugu na mauji yaliyo fanyika mkwa 2007 kabla na baada ya uchaguzi.
Kwa mijibu wa habari kutoka mahakama hiyo zinasema wailio funguliwa kesi ni " Makamu wa Waziri Mkuu na Waziri wa Fedha Uhuru Kenyatta 50, aliyekuwa waziri wa Elimu William Ruto 45, Joshua Arap Sang 36 ambaye alikuwa mtangazaji wa redio na katibu wa mawaziri Francis Muthaura."
Hata hivyo washitakiwa wote wamekanusha madai hayo na kudai ya kuwa wwatashirikiana na mahakama hiyo na ukweli utajieleza.
Naye William Ruto amedai yakuwa kesi hiyo haita mzuia kugombani kiti cha urais na kusema " kesi hii ni kishangazo kwangu na naamini ukweli utaonekana na naomba wapinzani tukutane kwenye uchaguzi na wananchi waamue."
Kufunguliwa kesi zidi ya Wakenya hao kumekuja baada ya mwanasheria mkuu wa mahakama ya kimataifa  Luis Moreno Ocampo kumaliza kufanya uchunguzi wake.

Syria yapinga miswada ya jumuiya yaa nchi za Kiarabu.


Damascus, Syria 23/01/2012. Serikali ya Syria imezilaumu nchi za jumuiya za Kiarabu na kupinga miswada yote ambayo imetakiwa itimize.
Serikali ya Syria imesema " kitendo cha nchi za jumjuiya za Kiarabu kupitisha miswada hiyo ni kuingilia mambo ya ndani ya Syria  na haitokubaliana na ma miswada hiyo."
Miswada iliyo pitishwa ni kwamba rais Bashar al Assad achie madaraka na kukumkabidhi makamu wake ili aandae mpango wa uchaguzi na kupanga serikali ya mpito na lazima Syria ihakikishe yakuwa mauaji yanasimamishwa na maandamano yaruhusiwe.
Kwa mujibu wa muswada wa nchi za jumjuiya ya kiarabu, zililikuwa zimepanga yakuwa mabadiriko ya siasa nchi Syria yangekuwa kama yale ya Yemen.


Nchi za jumuiya  ya Ulaya zaiwekea vikwazo vya mafuta Iran


Brussels Ubeligiji - 23/01/2012. Nchi wanachama wa jumuiya ya Ulaya zimekubaliana kwa pamoja kuiwekea vikwazo Iran kwa kukubaliana kutonunua mafuta yanayo toka Iran.
Makubaliano hayo yemefikiwa nna nchi hizo ili kuilazimisha Iran kuachana na mpango wake wa kuendelea na uzalishaji wa nyuklia jambo ambalo nchi za laya na Marekani zinahisi ya kuwa Iran inampango wa kutengene siraha za kinyukli.
Vikwazo hivyo vya nchi za jumuiya ya Ulaya vimekuja baada ya Marekani kuiwekea vikwazo Iran katika maswala ya fedha na mabadiriko ya kibenki kati ya nchi hizo.
Mwakilishi wa jumuiya ya Ulaya katika maswala ya kigeni Catherine Ashton alisema " nchi zote 27 za jumuiya  ya Ulaya zimekubaliana kuiwekea vikwazo Iran ili kuishinikiza kuachana na mpango wake wa kuzalisha nyuklia."
Msemaji wa mambo ya kigeni wa Iran Ramin Mehmanpaarast alisema " vikwazo zidi ya Iran havitaifanya  nchi hiyo kusitisha mpango wake kuzalisha nyuklia na Iran itaibuka kuwa mshindi na nchi za Ulaya ndizo zitaathirikaa."
Iran ambayo hapo awali ilitangaza kuwa ikiwa vikwazo vitawekwa na kuathiri uuzaji wa mafutaa yake basi watafunga mfereji uliopo katika Ghuba ya Strait Hormuz.



No comments: