Saturday, January 14, 2012

Uchaguzi wa mkuu wa Kenya 2012 mikononi mwa Mwai Kibaki na Raila Odinga.



Uchaguzi wa mkuu wa Kenya  2012 mikononi mwa Mwai Kibaki na Raila Odinga.


Nairobi, Kenya - 14/01/2012. Mahakama Kuu nchini Kenya imetoa uamuzi ya kuwa uchaguzi mkuu wa nchi hiyo  ufanyika mwaka 2013 au kama ukitakiwa kufanyika mwaka huu itategemea makubaliano ya serikali ya muungano.
Jaji Mumbi Ngugi akiwa na majaji wenzake David Majanja na Isaac Lenaola alisema " Jopo hili la majaji limekubaliana kwa pamoja ya kuwa uchaguzi mkuu ufanyike mwaka 2013 Machi, na kama serikali itakubali baraza la mawaziri livunjwe mapema basi uchaguzi unaweza fanyika mwaka huu."
Na inabidi makubaliano hayo yawe kimaandishi


Angola yawapiga jeki Wareno kibiashara.


Luanda Angola - 14/01/2012 - Wafanya biashara wanaotoka nchini Angola wamekuwa na wakati mzuri wa kunua hisa na kufanya bishara zao nchini Ureno kutokana na nchi hiyo kuyumba kiuchumi.
Ureno ambayo ilitawala Angola miaka ya nyuma kabla ya Angola kupata uhuru 1975, imejikuta ikipigwa jeki na Angola katika sekta tofauti za kibiasha baada ya wafanya bishara kutoka nchi hiyo kuanza kufanya biashara na kuwekeza nchini humu katika baadhi ya mabenki.
Kwa mujibu wa wachunguzi wa maswala ya kiuchumi wanasema " Wareno wengi sasa wanaamia Angola katika harakati za kutafuta kazi na wakati huo huo kuuza na kununu bidhaa nchini Angola."
Angola na Ureno zimekuwa na historia ya karibu kwa kuzingatia nchi hizo zina watu ambao kwa njia moja au nyingine wanauhusiano wakaribu sana kijamii,


100% - Namuunga mkono   Baraka Obama hadi mwisho




Johannesburg, Afriak ya Kusini 4/01/2011. Mwana mama maharufu duniani kwa vipindi vyake maili alivyokuwa akivitangaza wakati wa kipendi chake cha TV nchini Marekani ameudhihirishia umma ya kuwa yupo pamoja na rais Baraka Obama kwa hali na mali.
Oprah Winfrey alisema " nina muunga mkono Baraka Obama kwa hali na mali na kwa kluzingatia kazi ngumu aliyonayo na jitihada zote ambazo ameonyesha katika kuinua maisha ya watu wote nchini Marekani kwakuzingatia wakati mgumu iliyopo na nikiongozi mwenye uewezo."
Na kama akiitaji huduma zangu nipi tayari kutoa huduma hizo wakati wowote, kwani niliyo hakuna asiye fahamu sifa za Baraka Obama hasa kwa wananchi wa Marekani kwani ameleta mabadiliko makubwa sana.
Oprah Winfley aliyasema hayo baada ya kumaliza kutoa zawadi ya vyeti kwa wanafunzi wa kwanza  walio maliza shule ambayo aliijenga nchini Afrika ya Kusini kwa ajili ya kuinua na kusaidia wasichana wasio na uwezo.

1 comment:

muhaiminabdullah said...

Althought I don't know what this post talk about but I know there are Oprah Winfrey and Barrack Obama in it's picture... I'm Indonesian... Nice blog brother...