Tuesday, January 17, 2012

Watanzania ni wachangamfu na wanamatumainai ya maisha.

Watanzania  ni wachangamfu na wanamatumaini ya maisha.

Dar er Salaam, Tanzania - 17/01/2012.Shirika linalo chunguza tabia na maisha ya binadamu wanavyo ishi  katika mazingira tofauti limeripoti ya kuwa wanchi wa Tanzania watu wachangamfu, wacheshi na furaha kwa ujumla na kuwa na matumaini makubwa kimaisha.
Shirika hilo The Legatum Prospertity Index limeasema " Tanzania ni nchi ya kwanza katika nchi za Afrika Mashariki na Kati na watu  waishio nchi Tanzania  wanauwezo wa kukabiliana na hali iliyopo, jambo ambalo linawapa matumaini ya kimaisha kwa kila siku na kuwa na furaha ya kimaisha."
"Tanzania pia ni nchi yenye amani na watu wake wanaweza kujitafutia, wanashirikiana kwa hali na mali kiti ambacho kinaleta furaha kwa jamii nzima." lilisema shirika hilo lenye makao makuu nchi Uingeraza Londo.

Somalia Puntland kuanza kuchimba mafuta.


Puntland, Somalia - 17/01/2012. Shirka moja la kutoka Kanada limeaanza kuchimba ili kutafuta vyanzo vya mafuta katika eneo lili Kaskazini mwa Somalia kenye  jimbo la Punland.
Shirika hilo lijulikanalo kama Canadian Africa Oil,  limeaanza uchimabaji huo kwa makubaliano na serikali ya Punland jimbo la Somalia lililo jitenga na Serikali ya Kuu Somalia.
Issa Farah mkurugenzi mkuu wa madini na nishati alisema " huu ni mwanzo wa mabadiliko kwa Wasomalia wote kwa kuzingatia Somalia imekuwa na matatizo tangu mwaka 1991 na fikili baada ya miaka 10 Somalia itakuwa imebadilika kiuchumi kwa kiasi fula."
Uchimbaji wa kutafuta vyanzo vya mafuta hayo utaanza kwa kuchimbwa mita 38000 ambapo inatarajiwa kufikia mafuta amboyo yanakadiliwa kuna mapipa zaidi ya bilion 4.

Uingereza yakataliwa kumridisha kwa nguvu Abu Qatada nchini Jordani.


London, Uingereza - 17/01/2012. Mahakama ya kutetea haki za binadamu ya nchi za jumuiya ya Ulaya imepinga ombi la serikali ya Uingereza la kutaka mmoja wa dau wa Osama bin Laden arudishwe nchi Jordani.
Mahakama hiyo ilikataa abu Qatada kuridishwa kwa nguvu nchini Jordani ambapo anakabiliwa na kesi za uhaini, kwa kuwa kuna uwezekano haki zake za kibinadamu zikavunjwa na serikali ya Jordani.
Mahakama ilisema " tumeona ya kuwa Abu Qatada akirudisha nchini Jordani huenda akateswa na kupewa adhabu ambazo zinakwenda na kinyume na haki za bibanadamu."
Abu Qatada, anayejulikana kwa jina la Omar Mohammed  Othman alipata ruhusa ya kuishi nchi Uingereza  1993 baada ya kukumbia to  Jordani kwa kuwa serikali ya nchi hiyo ilikuwa inamuhusisha na tukio la kulipuliwa kwa shule ya Waamerika iliyopo nchini Jordan na Jerusalem Hotel.

No comments: