Zawadi ya Nobel ya amani ya mwaka 2011 yatolewa rasmi kwa watunukiwa.

Oslo, Norway - 10/12/201. Rais wa Liberia na wenzake wawili ambao walichaguliwa kutunukiwa zawadi ya amani ya Nobel wamekabidhiwa rasmi katika jiji la Oslo nchini Norway.
Ellen Johnson Sirrleaf Leymah Gbowee na Tawakul Karman walitunukiwa rasmi zawadi mbele ya wageni rasmi na wageni waalikwa ili kuja kushuhudia kutolewa kwa zawadi hiyo.
Mwenyekiti wa kamati inayo simamia utoaji wa zawadi hiyo Thorbjoern Jaglang alisema " wana mama hawa watatu wameonyesha mfano mzuri kwa jamii ya kuwa wakina mama wakipewa nafasi wanaweza kufanikisha kuleta amani duniani."
Wakina mama hao waliteuliwa mapema mwaka huu kutokana na mchango wao katika harakati za kupigania amani na utulivu kwenye nchi zao.
Kroatia yakubaliwa kujiunga na nchi wanachama wa jumuiya ya Ulaya.

Zagreb, Kroatia - 10/12/2011. Serikali ya Kroatia imetia sahii mkataba wa kuwa nchi ya 28 kujiunga na jumuiya ya nchi za Ulaya.
Sahii hiyo iliwekwa 09/12/2011, masaa machache baada kumalizika mkutano wa viongozi wa nchi hiyo walipo kutana kujadili mbinu za kudhibiti matumizi ya nchi wanachama wa jumuiya hiyo ya Ulaya.
Rais wa jumuia ya Ulaya Herman Van Rompuy alisema "Kroatia imeonyesha unadni wake na kutaka nchi hiyo iwe mwanachama wa kweli wa nchi za jumuiya ya Ulaya na tunaikaribisha."
Rais wa Kroatia Ivo Josipovic alisema " leo Kroatia imeingia ndani ya jumuiya ya Ulaya ili cha muhimu ni kwamba jumuiya ya Ulaya imefunguliwa milango na Wakroatia."
Uanachama huo wa Kroatia utaanza kamili ifikapo mwakani meizi ya kati ya mwaka.
Papa Benedikt XVI kufanya ziara nchini Kuba.

Vatican, Vatican City - 10/12/2011. Papa Benedikt XVI atatembela nchi ya Kuba hapo mwani kwa mujibu wa ofisi inayo shughulikia safari za Papa.
Kwa mujibu wa habari hizo zinasema "ziara ya Papa nchi Kuba itambatana na kuazimishwa kwa miaka 400 ya Mtakatifu Virgin wa Caridad del Cobre na itazidi kuongeza na kukuza imani ya Wakuba ambo wengi ni watu wa imani."
Hata hivyo tarehe ya Papa kuanza ziara nchini Kuba itatangazwa siku chache kabla ya kuanza ziara hiyo.
Ziara hiyo ya Papa Benedikt XVI inafuatia ziara ya marehemu Papa Benedikt aliyo ifanya nchini Kuba mwaka 1998.
Hali si shwali nchi JKD na Joseph Kabila atangazwa kushinda uchaguzi wa urais.


Akiongea kupitia TV na kuelezea matokeo ya uchaguzi huo, waziri wa mawasiliano Ngoy Mulunda alisema, " mpaka sasa rais Joseph Kabila amesha pata 48% ya matokeo ya uchaguzi, ila bado tunasubiri uamuzi wa mwisho wa mahakama kuu kutoa uamuzi wake."
Mgombe mpinzani wa kiti hicho cha urais, Etienne Tsheked alisema "sisi wapinzani hatuta kubaliana na matokeo yoyote kwani shughuli zote za upigaji kura haukuwa wa kihalari."
Uchaguzi wa JKD Kongo ulifanyika 28-28/12/2011 ili kumchagua rais atakaye ongoza nchi hiyo kwa kipindi kingine cha miaka mitano.
No comments:
Post a Comment