Friday, December 9, 2011

Vladmir Putin aionya Marekani kuingilia maswala ya kisiasa ya Urussi

Wagombea wa Republican nchini Marekani wahaidi kuleta mabadiliko Mashariki ya Kati.
Washongton, Marekani - 08/12/2011. Viongozi wanaogombea kiti cha urais kupitia chama cha Republican nchi Marekani wamehaidi kupambana na serikali zilizopo za Syria na Iran kama wakichaguliwa.
Wakiongea kwa nyakayi tofauti wagombea Newt Gingrich , Mitt Romney na Rick Santorum walisema inabidi serikali za Iran na Syria zibadilishwe kwani zinahatarisha maeneo ya Mashariki ya Kati."
Viongozi hao walidai pindipo watakapo kuwa madarani watafanya kila liwezekanalo ili kuzing'oa serikali za Syria na Iran.
Kwa kuongezea Newt Gingrich alisema " rais Obama amekuwa hafanyi lolote katika kupambana na vitisho vya Iran na hata kufikia kumtuka waziri mkuu wa Izrael Benyamin Netanyahu."
Hata hivyo, mmoja wa viongozi wa chama cha Democrat cha Marekani Nita Lowey alisema " usemi huu wa viongozi hao wa Republican unaharibu mahusiano ya kidiplomasia na inatia aibu kuona wanavyo mlaumu rais Baraka Obama."
Wagombea wa chama cha Republican wapo mbioni katika kampeni ya kutaka kuchaguliwa ili kuweza kupambana na rais Baraka Obama katika uchaguzi mkuu wa urais hapo mwakani.
Iran yaonyesha video ya ndege ya Kimarekani aina ya drone iliyo ikamata.
Tehran, Iran - 08/12/2011. Serikali ya Iran imeonyesha picha za video ya ndege ya Marekani aina ya drone ambayo ilidai kuingusha hivi karibuni.
Habari kutoka ndani ya jeshi la Iran zinasema, "ndege hiyo aina ya drone imetengenezwa kwa mitambo ya kisasa na ya hali ya juu ili kuweza kuchunguza popote inapo tumwa na ilikuwa inatumika katik kuchunguza Iran japo kuwa ilikuwa kwenye mipaka ya Aghanistan."
Kufuatia kukamtwa huko kwa ndege ya aina ya drone, serikali ya Iran imemwkita balozo wa Uswisi nchi Iran, ili kutoka malalamiko yake kutokana na kitendo cha Marekani kuingia anga la Iran bila ruhusa.
Vladmir Putin aionya Marekani kuingilia maswala ya kisiasa ya Urussi
Moscow, Urussi - 08/12/2011. Waziri mkuu wa Urussi ameilaumu serikali ya Marekani kwa kuingilia maswala ya ndani na ya kisiasa ya Urussi.
Vladmir Putin, alisema " maandamano na vurugu ambazo zinatokea kwa sasa zinatokana misaada inayo tolewa na serikali ya Marekani na hilo siyo jambo la busara kuendelea kufanya hivyo."
Waziri mkuu Putin alisema hayo kufuatia kauli iliyo tolewa na waziri wa mabo ya nchi za nje wa Marakani Bi Hillary Clinton ya kuwa "uchaguzi uliyofanyika nchini Urussi haukufuata uhalali wa misingi ya uchaguzi."
Kufuatia kauli hiyo, waziri mkuu Putin aliagiza kuwepo na mazungumzo na vyama upinzani ili kujua ukweli na kutatua tatizo hilo.
Rais Robert Mugabe ataka uchaguzi mkuu wa Zimbabwe ufanyike mwaka 2012.
Harare
, Zimbabwe - 08/12/2011. Rasi wa Zimbabwe ameitisha uchaguzi mkuu ufanyike nchini humo ifikapo mwakani 2012.
Rais Robert Mugabe aliyasema hayo alopokuwa akiwahutubia wanachama wa chama tawala cha ZANU-PF uliyo fanyika mjini Bulawayo
Rais Mugabe alisema "namatumaini makubwa chama chetu cha ZANU-PF kitashinda na umefikia wakati muafaka wa kujiandaa na uchaguzi na jambo hilo tunawapa wananchi wa Zimbabwe na hili swala la kuwepo na serikali ya muungano hailisaidii wananchi wa Zimbabwe."
Kuitishwa kwa uchaguzi huo, kunakuja wakatia serikali ya muungano inayo ongoza nchini Zimbabwe inaonekana kuyumba zaidi tangu kuundwa.
Rais Robert Mugabe amekuwa katika kiti hicho tangu Zimbabwe ilipo pata uhuru mwaka 1980 kutoka serikali ya Uingereza.

No comments: