Mkutano wa mazingira bado kitendawili.
Durban, Afrika ya Kusini - 05/12/2011. Mamia ya wananchi wamendamana katika jiji la Durban nchini Afrika ya Kusini ikiwa ni kupinga kitendo cha kucheleweshwa kwa uamuzi wa kupambana na uchafuzi wa mazingira.
Waandamanaji hao walionekana wakiwa wamebeba mabango yanayo onyeshwa kutorizika kwao na nchi tajiri duniani kama Marekani na Kanada kutochukua uamuzi wa busara katika kupambana na uchafuzi wa mazingira.
Mkutano huo unafanyika ili kupata jibu ni kwa jinsi gani mazingira yanaweza kulindwa, kufuatia habari kutoka kwa wataalaamu wa mazingira ya kuwa kuna "dalili kubwa ya kuwa kwa sasa uharibifu wa mazingira umefikia kiwango cha kutisha kiasi cha kuhatarisha mazingira ya kizazi kijacho"
Hadi sasa uamuzi wa kupambana na uharibifu wa mazingira umekuwa ukikumbwa na wakati mgumu kutokana na nchi tajiri kusita kukubaliana na masharti ya uamuzi wa kupambana na uharibifu wa mazingira.
Irani ya dai kuangusha ndege aina ya drone ya Kimarekani.


Tehran, Iran - 05/12/2011. Jeshi la Iran limedai kuangusha moja ya ndege aina ya Drone ambayo iliingia katika anga la Iran.
Habari zilizo patikana kutoka Iran na kutangazwa na idhaa tofauti za kiarabu za zinazo milikiwa na Irani zimesema " jeshi la Iran limefanikiwa kuiangusha ndege ya aina ya Drone RQ-170 iliyo ingia mashariki mwa Iran hivi karibuni baada ya ndege hiyo kuingia katika anga la Iran kinyume cha sheria."
Hata hivyo serikali ya Marakani haikuthibitisha tukio hilo, japo kituo kinacho shughulikia kurusha ndege hizo kimesema "moja ya ndege yake ilipotea kwenye radar zake na hadi sasa haijulikani ilipo."
Iran imekuwa na mvutano na nchi za Ulaya na Marakani kwa kushukiwa kutengeneza mambomu ya nyuklia.
Chama cha waziri mkuu Vladmir Putin cha shinda uchaguzi tena.

Moscow, Urusi - 05/12/2011. Matokeo ya uchaguzi wa wabunge nchini Urussi yamekipa chama tawala cha United Russi Party viti ambavyo havikutarajiwa.
Chama hicho ambacho waziri mkuu Vladmir Putin anatarajiwa kugombea urais kupitia chama hicho kilipata viti 238 kati ya viti 450 ambayo vipo katika bunge hilo la DUMA la Urussi.
Vladmir Putin alisema " ingawa tuna wakati mgumu wanachi wameonyesha kuamini uongozi wetu na tutaendelea kuijenga nchi yetu kwa hali na mali na hii ndo demokrasi ya kweli kwani wanachi wameongea kutumia kura zao."
Asilimia 60 ya watu wa Urusi ambao wapo 110 millioni ndiyo waliojiandikisha kupiga kura ya kuchaguwa wabunge wa baraza la DUMA.
Baraka Obama na Asif Ali Zardari waongea juu ya shambulizi nchini Pakistani.


Washington, Marekani - 05/12/2011. Rais wa Marekani ametuma salamu za rambi rambi kwa rais wa Pakistani na kusisitiza yaa kuwa shambulizi lilifanyika hivi karibuni na kuua wanajeshi wa Pakistani lilitokea kwa bahati mbaya.
Baraka OBama alisema "nasikitika kuona maisha ya watu yamepotea,"alimweleza rais wa Pakistani Asif Ali Zardari.
Rais Oboma aliongeza kwa kusema " serikali ya Marekani itajitahidi kwa kila njia kuchunguza ni kwanini mashambulizi hayo yametokea."
Shambulio hilo limeleta hali ya kupingwa kwa Marekani na wanachi wa Pakistani kwa kufanya maandamano jambo ambalo limepelekea kwa serikali ya Pakistani kuamrisha baadhi ya wafanyakazi wa Marekani waondoke nchini humo na kugomea mkutano wa kuimarisha ulinzi nchini Afghanistani unaofanyika nchini Ujerumani Bonni
Katika mazungumzo hayo rais Obama na Ali Zardari walihaidi kushirikiana na kuzidi wasiliana.
No comments:
Post a Comment