Monday, December 19, 2011

Kiongozi wa Korea ya Kaskazini afariki dunia.

Kiongozi wa Korea ya Kaskazini afariki dunia.


Pyongyang, Korea ya Kaskazini - 19/12/2011.  Kiongozi wa Korea ya Kaskazini amefariki dunia siku ya Jumamosi wakati akiwa njiani kutoka katika jiji la Pyongyang.
Kim Jong-Il  69 alifariki kwa kugonjwa wa moyo kwa mujibu wa habari kutoka serikali ya nchi hiyo.
Mtangazaji wa luninga ya taifa ya Korea ya Kaskazini alisema " tumepoteza kiongozi mpendwa wa chama na nchi  na ni uchungu kwa taifa ziama."
Kwa mujibu wa habari kutoka Korea ya Kaskazini zinasema, mtoto wake wa kiume Kim Jong-Un 28 ndiye aliyechaguliwa kushika nafasi ya baba yake.
Kim Jong Il alichukua uongozi wa Korea ya Kaskazini  mwaka 1994 baada ya baba yake Kim Il Sung
kufariki dunina.
Kufuatia  kifo cha kiongozi huyo, nchi za Magharibi zimetoa matazamo tofauti na kutaka uongozi mpya kujitaidi kushirikiana na jumuiya ya kimataifa.
Syria yakubali kusaini mkataba wa makubaliano na jumuiya Kiarabu.



Kairo, Misri - 19/12/2011. Serikali ya Syria imekubali kutia saini mkataba wa makubaliano jumuiya ya nchi za Kiarabu ambao utaruhusu waangalizi wa jumuia hiyo kuingia nchi Syria ili kuangalia hali halisi ya kisiasa nchini humo.
Makubaliano hayo ambayo yalitiwa saini na waziri msaidizi wa mambo ya nje wa  Faisal al Maqgad na latubu msaidizi wa jumuiya ya nchi za Kiarabu Ahmed Ben Helli jijini Kairo nchi Misri.
Waziri wa mabo ya nje wa Syiria Walid Muallem alisema " Syria imesaini makubaliano hay baada ya kuona yana manufaa kwa nchi na hayaingilii mambo ya ndani ya nchi."
Makataba wa makubaliano hayo umekuja siku chache kabla ya jumuiya nchi za Kiarabu kuamua kupeleka swaka la Syria katika balaza la usakama la Umoja wa Mataifa.

No comments: