Monday, December 26, 2011

Papa Benedikt aongoza misa ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo.

Papa Benedikt VXI aongoza misa ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo. 




Vatican, Vatican City - 26/12/2011. Papa Benedikt wa XVI ameongoza misa ya Kristmas katika kanisa la Mtakatifu Peter Basilika wakati wa  kusherekea siku ya kumbukumbu ya  kuzaliwa kwa Jesu Kristo mjini .
Papa Benedikt alisema " waumini lazima tufanye mabadilko makubwa ya kiimani na kujua umuhimu wa siku kuu ya Krismas, kwan siku hizi sikukuu ya Krismas imekuwa siku ya biashara na kusahahu ya kuwa sisi binadamu tunatakiwa tukumbuke ya kuwa ni siku ambayo tuliletewa mkombozi ili aje kutukomboa kutonaka na dhambi zetu, na inapaswa kutafakari ukarimu huo."
"Tumwombe Mungu atuzidishie mapenzi na tupendane kusaidiana, kwani machafuko ugomvi na mvurugo wa amani katika jamii vina sababishwa na kutokuwa karibu na Mungu na wale wote waletao hayo wajue ya kuwa jesu Kristo atawashinda tu. Aliongeza Papa Benedikt.
Misa hiyo iliyo ongozwa na Papa Benedikt wa VXI ilikuwa moja ya misa na sara zilizo fanyika duniani kote ili kusherekea kuzaliwa Jesu Kristo. 

Urusi ya mteua mkuu mpya wa maswala ya sayansi ulinzi jeshi
na upelelezi.


Moscow, Urusi - 26/12/2011. Serikali ya Urusi imemteua mkuu mpya wa maswala ya upelelezi wa kiulinzi jeshi  ili kuchua nafasi iliyo achwa wazi na aliyekuwa kiongozi wa sekta hiyo.
Habari kutoka ofisi ya wizara ya ulinzi zilisema "Maja Jenerali Igor Sergu 64 alichaguliwa  kuchukua nafasi hiyo baada ya Kanali Generali Alexander Shlyakhtuvo kujiudhuru kutokana na sababu kibafsi ikiwa ni moja ya maandalizi ya kulitaya kazi kutokana na umri."
Meja Generali Igor Sergun atashughulikia  maswala ya ulinzi wa kisayansi jeshi na kusimamia mambo yote yanayo husu sekta ya  ukachelo wa kiulinzi jeshi.

Waziri wa mambo ya nje wa Izrael adai rais wa Wapelestina siyo mtu wa kuleta amani.


Jerusalem, Izrael - 26/12/2011. Waziri wa mambo ya nje wa Izrael awahutubia watu waliohudhuria mkutano mjini Jerusalem na kudai  ya kuwa mapatano na Wapalestina ni kitendawili.
Waziri Avigdor Liebrman alisema " rais wa Wapalestina siyo mtu wa kukaanaye ukaongea maswala ya amani na hihi imetokea mara kwa mara na yoyote anayesema ya kuwa matatizo kati ya Waizrael na Wapalestina yatakwisha hivi karibuni anawaongoza wengine vibaya na visivyo kwani hali hii inaonekana itachukua miaka na lazima tujiandae ili kuweza kutafuta ufumbuzi wake kiuchumi, kijamii, kiushirikianao na bila kusahahu swala la ulinzi na usalama."
 "Na haiwezekani kuanza kuweka msingi wa nyumba wakati bado tetemeko la ardhi lina tikisa ardhi?"Aliukiza waziri Lieberman.
Jambo muhimu kati Waizrael na Wapalestina ni kutafuta njia ya kutatua ugomvi uliopo na siyo kusimamisha ugomvi." aliongezea Lierbman. 
Mgogoro wa Wapalestina na Waizrael na Wapalestina  imekuwa kitendawili kwa jumuia ya kimataifa kwa miaka mingi na hadi sasa bado utatafutiwa ufumbuzi.

Kiongozi wa kundi la JEM nchini Sudani auwawa na jeshi la Sudani.



Kordofan, Sudan - 26/12/2011. Jeshi la Sudani limetangaza ya kuwa limefanikiwa kumuua aliyekuwa kiongozi wa kundi la upianzani la  Justice Equality Movement JEM na baadhi ya wapiganaji wake 30.
Kwa mujibu wa habari kutoka jeshi la Sudani zinasema " mashambulizi hayo yalifanyika mapema alfajiri wakati ndege za kijeshi zilipo fanya mashambulizi kwenye aneo ambalo alikuwepo Khalil Ibrahim na badhi wa piganaji wake."
 Waziri wa habari wa Sudani allisema "tungependa kundi hilo lijiunge kwenye meza ya makubaliano ya amani kwani milango bado ipo wazi na itakuwa jambo la busara kama kundi hilo litaamua hivyo."
Mashambulizi hayo yamekuja baada ya kundi la JEM kudai yakuwa lilikuwa linakaribia kuingia jijini Khartoum tayari kujianda kuuangusha utawala wa  rais Omar al Bashir wa Sudan.
Kundi la JEM limekuwa likilaumiwa kwa kufanya au kuhusika na mashambulizi mara kwa mara nchini Sudan

Mchezajiwa Kriket nchini Pakistan aanza kampeni za uchaguzi.


Karachi, Pakistani - 26/12/2011. Mamia ya waru walikusanyika kusikia hotuba ya aliyekuwa mchezaji maarufu wa mchezo wa kriketi na ambaye kwa sasa ni mwanasiasa maarufu nchini Pakistani.
Imran Khan, ambaye amefanya mkutano huo zikiwa zimebakia siku chache za kuanza uchaguzi wa wabunge alisema "Pakistani inatakiwa kufuata maadili ya Uislaam, ambapo kila mwanachi apate haki sawa kielimu, afyaa na huduma nyingine zote za jamii na bila kusahau haki itendeke kwenye vyomb vya sheria."
"Nafahamu yote hayo yapo, lakini kwa sasa hayo yote ayatekelezwi ipoasavyo, na kama nchi za Ulaya UK zingekubali kutekeleza Uislaam zingekuwa nchi bora kuliko sisi. Aliongezea Khan.
Katika hotuba yake hiyo, Imran Khan  alihaidi kupambana na rushwa na kuongeza ya kuwa matatizo yaliyopo nchini Pakistani yanaweza tatuliwa ikiwa



No comments: