Saturday, December 31, 2011

Kwaheri 2011 kwa mafundisho, karibu 2012 kwa wema barani Afrika.

 Kwaheri 2011 kwa mafundisho, karibu 2012 kwa wema barani Afrika.


 
Mwaka 2011 utakumbukwa na Waafrika kama mwaka ambao ulikuja na majonzi na furaha ya  kihistoria, hasa kwa kizazi cha tatu cha bara la Afrika.
Kizazi cha tatu cha Afrika, ni wale wote waliozaliwa miaka ya 70 hadi miaka ya 90 tangu Afrika ipate uhuru kutoka kwa wakoloni na mwaka 2011 na chini ya uongozi wa demokrasi wameongozwa na kubadika kuliko walivyo tarajia.
 Kizazi hiki cha tatu cha Waafrika  waliozaliwa miaka ya 70 na hadi 90  wameweza kuona mabadiliko ya kijamii, kisayansi, kiuchumi na siasa ambayo wengi hawakutarajia kuyaona kwa muda mfupi wa maisha walioishi kulinganisha na baba mama, mababu na mabibi waliopigania uhuru.
Mwaka 2011 mengi yametokea, hasa kubwa katika swala la kisiasa chini ya kiongozi demokrasi na kuleta mauaji na machafuko katika bara la Afrika tangu uhuru.
 Kizazi hiki cha tatu ambacho wengi wana miaka kati 45 na 20 chini ya kiongozi demokrasi ambaye amewafanya kujitambua yakuwa wanahitaji mabadiliko na kuanza kuyatekeleza kwa njia tofauti.
Yaliyofanyika kimabadiliko chini ya kiongozi demokrasi  yameonekana na sehemu ya matokeo yake yameaanza onekana na mengi matokeo yapo njiani yanakuja.
Jambo ambalo lapaswa kukumbukwa na kizazi cha tatu cha Afrika tangu uhuru ni kwamba swala la uangalifu na umakini utazamwe kwa undani ni kwa jinsi gani kiongozi demokrasi anavyo ongoza katika kuleta mageuzi.
Na vile vile ieleweke ya kuwa  binadamu ameumbwa kuwa na tofauti, na kama hizo tofatuti zikifanyiwa kazi kwa lengo moja mazuri yatafanyika na kuleta haki na amani.
Kwani naimani yakuwa kizazi cha tatu cha bara la Afrika tangu uhuru kina lengo la kuleta maendeleo katika bara la Afrika.
Na kwa viongozi waliopo ningependa kuwakumbusha yakuwa kuongoza ni mthiani mkubwa ambao ipo siku watapata majibu yao kama walifauru au walishindwa.
Ikumbukwe kuwa  wazazi wetu, mababu na mabibi walipo kuwa wanapigania uhuru walikuwa wanajua wafanyalo, hivyo basi kizazi cha tatu cha Afrika chini ya kiongozi demokrasi umakini unatakiwa ili kufikia malengo yaliyo kusudiwa.
Yaliyo tokea mwaka 2011 chini ya kiongozi demokrasi yameleta matokeo ambayo lazima kuyatafakari kwani mtutu wa bunduki na nchi ya mkuki siyo chanzo cha haki sawa kwa wote.
Hivyo basi  mabaya yaliyo tokea mwaka 2011 yawe ni fundisho na yasirudiwe  na tuanze  mwaka 2012 kwa malengo mazuri.
Kwaheri 2011 kwa mafundisho na karibu 2012 kwa wema barani Afrika.
Mungu Ibariki Afrika.
Mungu wabari wale wote wapendao Haki na Amani duniani.
Kwaniaba ya launite.blogspot.com tunawatakia heri ya mwaka mpya 2012 na Mungu atubariki wote. Amina
Mhariri.






No comments: