Monday, December 26, 2011

Miaka 20 yatimia tangu kuvunjika kwa USSR.

Wapiganaji walio saidia kumng'oa Gaddafi wadai wapo tayari kwenda Syria kwa mapigano.

Tripol, Libya - 26/12/2011. Kiongozi wa kundi lililoshiriki kumtoa madarakani Muammar Gaddafi amewahimiza wananchi wa Syria kufanya mapinduzi.
Mohamed Alhuraizi alisema " tupo tiyari kuwasaidia ndugu zetu wa Syria, vijana wapo tayari  kupigana kuikomboa Syria, kwani kwa uwezo wa Mola tutashinda kwa kufuata nia ya Che Guevara ya kupigania haki  amani na uhuru tnataka kuwasaidia ndugu zetu na nafikiri ni wajibu wetu."

Pakistani na China kushirikiana kiukaribu zaidi.


Isamabad, Pakistan - 26/12/2011.  Serikali ya Pakistan na China zimehaidi kushirikaiana kikamilifu ilikudumisha uhusiano uliopo.
Hayo yaliongelewa na rasi wa Pakistani  Asif Ali Zardari na mgeni wake mwakilishi wa serikali ya China kamishna Dai Bingguo.
Kukutana huko kumekuja katika kuadhimisha miaka 60 ya ushirikiano wa China na Pakistani.
Beijing na Islamabad zilitiliana sahii mkataba wa kibiashara wa $1.6 billion ambapo nchini hizi mbili zitaweza kubadilishana kibisahara na kupunguza kutegemea mzunguko wa pesa.
Uhusiano wa China na Pakistan umekuwa wa karibu saana na hata kufikia kufanya mazoezi ya pamoja ya kijeshi katika mji wa Jhelum uliopo Pakistan.

Brazil yakuwa kiuchumi na kuipita Uingereza.


Rio de Janairo Brazil - 26/12/201. Kitengo kinacho shughulikia maswala ya uchunguzi wa uchumi duniani Centre Economics and Business Research CEBR kimetangaza matokeo ya maendeleo ya kiuchumi duniani.
CEBR imeripoti " Brazil imekuwa nchi ya sita kiuchumi na kuipita nchi ya Uingereza kutonaka kukua uchumi kwa 7.5% sambamba na mipango mbinu ya uzalishaji wa bidhaa zinazo tumika na kuuza vitu vyake hasa nchini China na kuagizia vitu vichache kutoka nje ya nchi (Brazil)."
Kitengo hicho kimetabiri ya kuwa huenda Urusi ikakuwa kiuchumi ifikapo mwaka 2020 kwani kwa sasa  ni ya tisa na nchi za Ulaya huenda zikadondoka kiuchumi ifikapo 2020.

Syria yahaidi kushirikiana na wajumbe wa jumuiaya ya nchi za Kiarabu waliopo nchini humo.


Damascus, Syria - 26/12/2012. Wajumbe wa umoja wa nchi za Kiarabu wamehakikishiwa kupata ushirikiano wa kila aina kutaka serikali ya Syria.
Habari kutoka serikali ya Syria zinasema " serikali itashirikiana kikamilifu katika kuahakikisha ya kuwa mipango yote iliyo pendekezwa na umoja huo zinafuatwa."
Mkurugenzi wa maswala ya unangalizi wa Mashariki ya Kati Haisham Jaber alisema "habari zinazo tolewa na vyombo vya habari zinaelezea vifo vya watu , lakini havielezei ya kuwa pia makundi ya upinzani ya wanajeshi ambao wanapigana na serikali, na nibora kutenganisha kati wa wanajeshi wapinzani na raia na hii ndiyo inaweza kuwa chanzo cha ugumu wa kazi kwa wajumbe wa jumuiya  ya Kiarabu waliopo nchini Syria."
Wajumbe hao ambao waliwasili nchini Syria, wamekuwa na wakati ngumu, kutokana na hali ya mvutano wa kisiasa na misimamo na malengo ya vyama vya upinzani vinavyo pinga serikali ya Syria iliyopo chini ya rais Bashar al Assad.

Miaka 20 yatimia tangu kuvunjika kwa USSR.


Moscow, Urusi - 26/12/2011.  Wanchi waliokuwa katika shirikisho la nchi za  United Soviet Socialist Repiblic USSR wanaadhimisha miaka 20 tangu kuvunjika kwa shirikisho hilo.
Shirikisho hilo ambalo liliundwa 1922 lilivunjika  chini ya uongozi rais Mikhail Gorbachev na nchi zote ambazo zilikuwa katika shirika hilo kuwa nchi huru na kuanza kujijenga ka nchi.
Hata hivyo waziri mkuu wa sasa wa Urusi Vladmir Putin alisema "kuvunjika kwa shirikisho hilo ni moja ya makosa ya kihistoria ya karne ishirini na ishirini na moja." Waziri mkuu Putini aliyasema haya wakati alipo kuwa rais wa Urusi.
Hata hivyo wachunguzi wa mambo ya kisiasa wanadai kuvunjika kwa USSR, hakukuwa kama mapinduzi, bali ilikuwa ni utengano wa amani ambao matokeo yake yanaonekana mpaka sasa.



No comments: