Jiji la Dar-es- Salaam nchini Tanzania la kumbwa na mafuriko.
Dar-es- Saalam, Tanzania - 22/12/2011. Jiji la Dar -es- Salaam nchini Tanzania limekubwa na mafuriko makubwa baada ya mvua kubwa kunyesha na kusababisha maafa makubwa ya kijamiii na kimazingiia
Kwa mujibu wa habari kutoka serikalini zilisema "watu wapatao kumi na mbili wamefariki dunia na watu walio wengi wamepoteza makazi yao."
Mkuu wa polisi wa jiji la Dar -es- Salaam Suleiman Kova alisema " maeneo yaliyo kumbwa na mafuriko ni Tabata, Buguruni, Kinondoni Mkwajuni, Jangwani, Kigogo na maeneo ya Mikocheni.
pia mafuriko hayo yalibomoa barabara na kuvunja madaraja."
Kitengo kinacho shughulikia hali ya hewa kimetoa maelezo yakuwa mvua hizi hazijawahi kunyesha kiasi hiki tangu 1956 ambapo zilifikia kina cha 216 cha ujazo wa maji ardhini na pia kusababishwa na upepo unao enendelea.
Sweden yata waandishi wa habari kutoka Sweden waliopo Ethiopia waachiwe
Adis Abeba, Ethiopia - 22/12/2011. Mahakama jijini Adis Ababe imewakuta na hatia waandishi wa habari kutoka Sweeden na kosa la uhaini kwa kuwakamata katika kundi la wapiganaji wanao pinga serikali la Ogaden.
Johan Persso na Martin Schibbye walikamatwa mwezi wa Julai wakati jeshi la serikali ya Ethiopia lilipo kuwa likipambana ba kundi la Ogaden na baadaye kushitakiwa kwa kukutwa makosa ya kuingia nchini Ethiopia kiyume na sheria na kutoa msaada wa kundi la kigaidi.
Waaandishi wa habari hao wanatarajiwa kuhukumiwa vihi karibuni kabla mwisho wa mwaka na wanaweza kukaa jela miaka 18.
Hata hivyo serikali ya Sweden imeitaka serikali ya Ethiopia kuawachia waandishi wa habari hao, kwani walikuwa wanafanya kazi zao bila makosa.
Rais wa Urusi atangaza mpango mpya wa mfumo wa siasa nchini Urussi.
Rais Dmitry Medvedv alisema " serikali ya Urussi haitakubali machafuko yanayo letwa na watu wenye itikadi kali kwa kutumia mlango wa neno demokrasia na hatuta ruhusu watu wanamna hiyo kuwa na nafasi."
"Nchi inataka mabadiliko ya kisiasa yenye demokrasi bora na siyo vurugu, hii inahitajika ili kufungua ukurasa mpya ambapo kila raia wa Urussi atakuwa na haki sawa na kila chama kitapata nafasi katika demokrasi itakayo wafaa raia wa Urussi."Alimalizia rais Medvedev.
Hotuba hiyo ya rais Dimitry Medvedev, imekuja siku chache baada ya uchaguzi wa wabunge uliyo fanyika nchini humo na kuleta wasiwasi mkubwa kufuatia matokeo ya uchaguzi huo na watu kuandamana.
Jiji la Baghda nchini Irak lashutushwa milipuko ya mabomu iliyo leta maafa.
Baghdad, Irak - 22/12/2011. Jiji la Baghdad limekumbwa na milipuko ya mabomu ambayo yamesababisha maafa makubwa na kuleta hali ya wasiwasi kwa wakazi wa jiji hilo.
Kwa mujibu wa mashahidi walisema " kunametokea milipuko zaidi ya kumi na mbili tofauti katika jiji hilo."
Habari kutoka wizara ya ndani ya Irak zinasema " watu wapatao 63 wamefariki dunia na wengine 176 kujeruhiwa vibaya kutoka na milipuko hiyo iliyo tokea sehemu tofauti ndini ya jiji la Baghdad."
Milipuko hiyo imetokea siku chache baada ya jeshi la Marekani kuaanza kuondoka nchini Irak na wakati huo huo kukiwa na mvutano wa siasa katia ya waziri mkuu Nour al Marik Shia na makamu wa rais Tarik al Hashim Sunni ambaye yupo ukimbizini katika eneo linalo ongozwa na Kurdish.
No comments:
Post a Comment