Hali ya kisiasa nchini Kongo JK yazidi kuleta utata.
Kinshasa, Kongo JK - 24/12/2011. Maafisa usalama nchini Kongo JK wamepambana na waadau na wale wanao muunga mkono kiongozi wa upinzani wa nchini hiyo Etienne Tshisekedi.
Mapambano hayo yametokea wakati wa maandalizi ya kumwapisha kiongozi huyo, kwa kudai Etienne Tshisekedi ndiye mshindi rasmi na anatakiwa ahapishwe awe rais.
Hata hivyo kwa mujubu wa habari zilizo patikana zinasema "Etienne Tshisekedi aliapishwa katika makazi yake."
Matokeo ya uchaguzi nchini Kongo JK yameteta mvutano kufuatia ripoti za jumuiya za kimataifa ya kuwa uchaguzi huo ulikuwa na matatizo.
Katika uchaguzi huo rais wa sasa wa Joseph Kabila alitamkwa kama mshindi kwa kupata kura 49% za kura na mpinzani wake Etienne Tshesekedi kupata 32%.
Joseph Kabila aliapishwa hivi karibuni kuwa rais wa Kongo JK na ataongoza nchi hiyo kwa kipindi kingine cha miaka mitano.
Uhuusiano wa Uturuki na Ufaransa wazidi kuwa na mvutano.
Ankara, Uturuki - 24/12/2011. Serikali ya Uturuki imeishambulia kwa maneno serikali ya Ufaransa na kudai pia kuwa Ufaransa kuhusika na mauaji ya kimbari nchini Algeria.
Uamuzi huu wa serikali ya Uturuki kufanya hivyo, umekuja baada ya bunge la Ufaransa kupiga kura kutambua ya kuwa mauaji ya Armenia yaliyo fanyika nchini Uturuki ni ya kimbari.
Waziri mkuu wa Uturuki Recep yayyip Erdogan alisema "mauaji yaliyo fanywa na Ufaransa nchini Algeria kuwanzia mwaka 1945 ni ya kimbari na yatambulike hivyo pia."
Ikiwa rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy ahajui kuhusu mauaji hayo ya kimbari, ni bora amuulize
baba yake Paul Sarkozy ambaye alikuwa mwanajeshi aliyepigana nchini Algeria 1940."Aliongezea waziri mkuu Reccep Erdogan.
Mvutano kati ya Ankara na Paris ulizidi kuwa mbaya baada ya kura hiyo na serikali ya Ututuki kutangaza kufunga mahusiano na Ufaransa.
Kuba kuachia wafungwa wa kisiasa.

Havana , Kuba - 24/12/2011. Rais wa Kuba amatangaza msamaha kwa wafungwa wapatao 3000 wakiwemo wafungwa 86 kutoka nchi za kigeni 25.
Rais Raul Castro alitangaza hayo wakati alipo kuwa akihutubia baraza la sheria la nchi hiyo na hii itakuwa mara ya kwanza kwa rais Raul kutoa msamaha tangu kuchukua madaraka kutoka kwa kaka yake Fidel Castro.
Kwa mujibu wa wachunguzi wa mabo ya kigeni ya Kuba walisema " uamuzi wa serikali ya Kuba kutoa msamaha kwa wafungwa hao ni katika mpango wa kujiaanda na ziara ya Papa Benedikt XVI ambayo anatarajiwa kuifanya hapo mwakana."
Uamuzi huu wa kuachia wafungwa wa kisiasa na wengine nchini Kuba kumekuja wakati nchi nyingi za Ulaya ya Magharibi na Amerika bado zinawasiwasi na serikali ya Kuba kutokana na msimamo wake wa kisiasa.
Maafisa usalama wa Nigeria wapambana na kundi la Boko Haram.
Abuja, Nigeria - 24/12/2011. Watu wapatao 61 wamepoteza maisha na makazi kuharibiwa kutokana na mashambulizi yanayo endelea kati ya jeshi serikali na kundi la Boko Harama.
Mashambulizi hayo ambayo yameaanza baada ya milipuko ya mabomu katika jimbo la Borno na Yobe na kuleta huharibifu mkubwa.
Kwa mujibu wa habari kutoka heneo hilo simasema " mashambulizi hayo yamesababisha vifo vya wakuu wawili wa polisi wakati wapambano hayo."
Kundi la Boko Haram limekuwa likipambana na serikali ya Nigeria kutokana nambishano wa tofauti wa siasa.
Na kutokana na vurugu za kisiasa nchini Nigeria watu wapatao 450 wameshapoteza maisha yao.
No comments:
Post a Comment